Mzee azidiwa ujanja garini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mzee azidiwa ujanja garini

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by aduwilly, Sep 7, 2012.

 1. a

  aduwilly JF-Expert Member

  #1
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,182
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mzee mmoja alipanda kwenye daladala na kubahatika kupata siti, lakini baada ya muda akagundua kuwa simu yake aloiweka mfukoni imeibiwa, basi akaamua kumuomba jirani yake kwenye siti aibipu namba yake akiamini mwizi wake atakuwa hajashuka kwani daladala tangu iondoke alipopanda hakuna aliyeshuka. Kumbe yule jirani yake ndo alikuwa kamchomolea mzee simu yake na kuiweka kwenye kava jingine alilokuwa nalo, hivyo alipoombwa na mzee kuibipu namba yake, jamaa aliamua kumpa simu mzee ili abipu yeye mwenyewe kwa kuwa alijua dili lake lishawini. Basi ikawa kila Mzee alipojaribu kuibipu namba yake alisikia "Namba ya mteja unaempigia, inatumika kwa sasa tafadhali jaribu tena baadae"
   
 2. Root

  Root JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,173
  Likes Received: 12,880
  Trophy Points: 280
  nini.kilifuata?
   
 3. a

  aduwilly JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,182
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Ukichukua simu halafu ukapiga namba ambayo line yake iko kwenye hiyo simu unaambiwa "namba unayopiga inatumika kwa sasa" so mzee akawa anasubiri kila baada ya dk 5 anapiga zen anajibiwa the same hadi jamaa akafika kituo anachoshuka na kutambaa na simu ya mzee
   
Loading...