Mzee atibua harusi akidai maharusi ni watoto wake

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
WAPENZI wawili waliokuwa tayari kufunga ndoa katika eneobunge la Bura, Kaunti ya Tana River walilazimika kusitisha harusi yao baada ya mwanamume kujitokeza ghafla harusini akidai yeye ni baba yao.

Anne Magwi na Jotham Munini, watoto waliolelewa na wazazi wa kambo, walikuwa wamefika kanisani Jumamosi kwa ajili ya harusi yao. Kabla wafunganishwe pingu za maisha, mzee mmoja alitokeza na dada zake kusimamisha harusi hiyo wakidai ilikuwa mwiko kwa mwanamume kumwoa dadake. Kulingana na mchungaji Festus Muli wa Kanisa la Holy Redemption Ministries, mwanamume huyo alidai alikuwa ametengana na mama za wawili hao zamani.
“Alieleza kuwa, alimzaa mtoto wa kiume katika mapenzi haramu na mwanamke mmoja, ambapo uhusiano wao haukuendelea, ilhali mtoto wa kike alikuwa tunda la uhusiano wake na ‘mpango wa kando’,” alisema kasisi huyo.

Mchungaji alielezea kwamba, mwanamume huyo alidai kuachana na mamake Jotham ilipofichuka alikuwa na uhusiano wa pembeni na mwanamke mwingine. Wakati huo mtoto alikuwa na umri wa mwaka mmoja.

Hapo ndipo alipoamua kujenga mahusiano na mpango wa kando, uhusiano ulioshindwa kustahimili mawimbi ya ufukara na kumfanya mwanamke kutoroka akiwa na mimba ya miezi minne. Anne, ambaye ndio tunda la uhusiano huo alilelewa na baba mwingine kwani mamake aliolewa mwaka mmoja baadaye na mwalimu.

Mchungaji Muli alielezea Taifa Leo kwamba, mwanamume huyo aliwaonyesha picha za wawili hao walipokuwa wadogo, ambazo alizipata kutoka kwa marafiki na jamaa waliokuwa wakiwasiliana naye. “Ni mtu na familia yake. Alipata ujumbe kutoka kwa rafiki zake ambao pia waliona ujumbe huo ukisambaa katika mitandao ya WhatsApp,” alieleza mchungaji huyo.

Kulingana na mpwa wa mwanamume huyo ambaye hakutaka kutajwa jina, mtu huyo amekuwa akiwatafuta watoto wake kwa miaka 10 bila mafanikio. Jitihada zake kufikia marafiki wa mke wa kwanza hazikuzaa matunda. Aliarifiwa kupitia marafiki kwamba, mwanamke huyo alikuwa amemzaa msichana anayefanana naye.

“Alimwona binti huyo mara moja katika shule ambayo watoto wake wanasoma. Alionyeshwa lakini hakujua jinsi ya kumfuata amweleze kwani baba mlezi alikuwa amekwenda kumtembelea wakati ule, hakumwona tena baada ya KCPE,” alisema. Mchungaji Muli alibaini kwamba, ilibidi asitishe harusi na kuwaita wazazi kwenye chumba cha faragha kwa mazungumzo.

Ilibainika kuwa mamake Bwana Harusi alimwarifu kuwa babake alikufa katika ajali ya barabarani akiwa mchanga sana, ilhali msichana huyo alifahamu kuwa babake aliyemlea ndiye baba mzazi.

“Wanawake hawakukanusha kuwa wanamjua mwanamume huyo, na wala hawakukanusha kuwa alikuwa baba yao. Ilikuwa hali ya kusikitisha ila ilibidi tukae chini kusawazisha mambo,” alielezea.

TAIFA LEO
 
Katika hali isiyotarajiwa, Ann Magwi na Jonathan Munini kutoka Tana River Kenya, wamelazimika kukatisha zoezi la kufunga ndoa, baada ya James Sidai kujitokeza kanisani na kusema yeye ndio Baba yao Mzazi, Baba huyo aliingia kanisani akiwa na Dada yake na kusema ndoa hiyo isifungwe kwa kuwa Maharusi ni Ndugu wa damu.

“Mama zenu nyie, mmoja aliniacha akaondoka na Mtoto akiwa na mwaka mmoja, mwingine aliona uchumi wangu umeyumba akaondoka akiwa na mimba ya miezi minne na akaolewa na Mwalimu, nikaamua kumuoa mwingine na tuna Watoto watatu, nimeona tangazo la harusi yenu WhatsApp zile picha nikasema hawa ni Wanangu nikachunguza kwa Watu mlioishi nao wakasema ni kweli” James

Bwana harusi ambaye ni Mfanyabiashara Katika mji wa Madogo aliondoka Kanisani kwa hasira akimuacha Mama yake akiwa analia huku Bibi Harusi akiondoka na Mama yake ambaye inadaiwa alikuwa amepoteza fahamu.
Shukrani kwa muungwana
 
Ilà wakenya wana visa vya ajabu sana hasa kwenye mahusiano. Wanaume tujifunze, hata ukizaa nje jaribu kufanya watoto wajuane, otherwise utaletewa mkwe "mwanao"!
 
Ilà wakenya wana visa vya ajabu sana hasa kwenye mahusiano. Wanaume tujifunze, hata ukizaa nje jaribu kufanya watoto wajuane, otherwise utaletewa mkwe "mwanao"!
Katika mahusiano unataka kunambia hao wapenzi hawakujuana na kuwajuza ndgu wengne mpaka siku ya harusi ndo kila kitu kinawekwa mezani? Wanayao hao Wakenya sio bure.
 
Kenya nchi ya vituko sana. Huna hela, mwanamke utamsikia kwenye redio tu. Wanavunja ndoa na kufundisha uadui. Yaani mwanamke hamwambii mwanae baba yake ni nani, inakuwa siri kisa mzee hana hela.

Kaka na dada wametinduana, ndoa imegoma.

Baba Atibua Ndoa ya Wanae (Kaka na Dada) Kanisani
Screenshot_20200910-083928.jpg
Screenshot_20200910-084045.jpg
 
Back
Top Bottom