Mzazi mwenzangu wangu mvivu

Mzazi mwenzangu wangu mvivu

Habari zakupotezana ndugu zangu Wana JF wenzangu,

Mwezi wasita mwaka huu mzazi mwenzangu aliniomba aje aishi kwangu maana haileti picha nzurii yeye kuendelea kuishi kwao hali yakuwa anamtoto namda huohuo mimi mzazi mwenzie nipo hajisikii vizuri. Nikaona nikweli alafu ukizingatia anamtoto wangu, nampenda, na nina malengo naye, kwahiyo nikaona nivizuri aje tuishi tu.

Mwanzo mzuri kila mtu akawa anasimamia majukumu yake vyema. Ila nikagundua anaasili yauchafu, vilevile nimvivu sio kidogo.

Akaanza tabia yakuniwekesha net, nikaona sio mbaya ila hali ilipozidi siku moja nikamgomea, alichonijibu kuwa 'kila siku awe anaweka yeye tuu'. Hiyo kauli ilinikera sana ila aliweka tukalala kila mtu nahamsini zake.

Maisha yakaendelea ila kwakusumbuana sana kuhusu usafi wandani. Kwahiyo Amani haipo yakutosha maana akiambiwa kuhusu usafi, kupanga vitu vizuri anakuwa mbogo.

Sasa wiki iliyopita nimetoka zangu katika mizunguko yangu, akaniuliza unakunywa Chai nikamjibu ndio, maana toka aje hapa ishamwambia usiku chai awe anahakikisha inakuwepo kama sio maziwa yaani kati yahivyo viwili. Kumbe mda ananiuliza kuhusu kunywa Chai mda huo Chai hamna kwahiyo alichonijibu kuwa makazi yamemchosha amepika vingi. Kwahiyo akapika chai ila kwashingo upande.

Mda mwingi amekuwa analalamika makazi mengi, wakati tunaishi chumba kimoja na sebule namtoto tunaye mmoja tu! Sasa hizo kazi nyingi anazolalamikia najiuliza zipo wapi? Yaani anajihisi kama vile nimtumwa kufanya majukumu yahapa nyumbani wakati anashinda nyumbani. Nasio kusema ninamaisha mazurii labda ninahemeaga mboga 7 ila mara nyingi huwa nahemea mboga moja naukikuta tunakula mboga mbili ujue hiyo nyingine ilibakia mchana...... Sasa hapo kazi zipo wapi? Kama kufua huwa anafua mara moja kwawiki ila yeye nikaribia siku zote zawiki analalamika kuchoka.

Huyu nimwanamke wangu wakwanza kuishi nae na nilikuwa ninashauku yakuishi nae ila najihisi kukinai kuishi namwanamke. Imefikia hatua hata hisia nae zimekata kutokana navimanenomaneno, namigogoro yahapa napale maana hazipiti siku 3 bila kukwaruzana.

Kutokana natabia zake nimedhamiria/nahitaji kumswaga ila mara nyingi nikitaka kufanya hivyo amekuwa akigoma nakuomba msamaha ila mtaishije maisha yakuombana misamaha kila siku?

Ee Mungu niepushe nahuu msalaba. Nakama hayupo tayari kujirekebisha namuomba Mungu tuachane kwaamani yaani akubali matokeo arudi kwao maana mimi kwaupande wangu ishajipima kuwa siwezi kumvumilia na hizo tabia zake.

RIP Benjamin williamu mkapa.

Mungu anakuonya kwamba anaweza kuwa siyo chaguo sahihi.pia tabia za kuchukuana kama mbuzi bila utaratibu ndiyo kitu cha hovyo kabisa.tafuta mwwanamke anayefaa na uoe kabisa

Pili wazazi tuwafundishe watoto wetu kufanya kazi.siyo kila kitu wanafanya watoto wa kazi
 
Huyo sio mwanamke bali ni mtu mwenye jinsia ya kike, mteme kabla jua halijazama
 
Mungu anakuonya kwamba anaweza kuwa siyo chaguo sahihi.pia tabia za kuchukuana kama mbuzi bila utaratibu ndiyo kitu cha hovyo kabisa.tafuta mwwanamke anayefaa na uoe kabisa

Pili wazazi tuwafundishe watoto wetu kufanya kazi.siyo kila kitu wanafanya watoto wa kazi
Nikweli mkuu maana vipo vingi ambavyo sijaviandika
 
Kama vile unaishi mfumo wa babu zako. Siku hizi men wanafanya more nyumbani Na ke wanafanya less sasa we mpaka uwekewe net kila Siku umekuwa king Muswati? Jitathimini pia kabla ya kurusha ngumi hewani Bro
Yaani uoe harafu uanze kufanya kazi za nyumbani acha umama boya wewe
 
Pole sana,
Kama umeoa katoto especially cha 97-20's utateseka sana,wengi wamelelewa na wadada wa kazi hivyo walifundishwa uvivu na wana maisha ya sinema,wachache sana utawakuta ni wawajibikaji.
Niliwahi kumuonya mke wangu mapema kabisa kabla ya ndoa,nikamwambia kuwa ndoa sio guarantee ya wewe kuwa na mimi ,muda na wakati wowote lolote laweza kutokea
 
Pole sana, inawezekana alifikiri mkianza kuishi pamoja maisha yatakua full kushinda 'kitandani' sasa amekuta ni vice versa.
Usichoke kumrekebisha au ongea na watu wazima wamuelekeze ili muishi kwa amani maadam mna mtoto tayari sio vizuri kuanza kuhangaika na watu wengne wakati bado mnaweza kurekebishana na mambo yakaenda vema.
Ushauri mzuri sana huu
 
Hapo anakupima akuone utachukua hatua gani. Ni kawaida ya watu wasio na home training nzuri.

Sasa fanya hivi, tafuta beki tatu mzuri ambaye akivaa anapendeza. Halafu kaa nae pembeni bila mkeo kuwa karibu. Mpe utaratibu wa vitu unavyotaka vifanywe hapo ndani kuanzia usafi, chakula, kutandika ndani, na kadhalika. Kisha kubaliana nae kiasi cha mshahara.

Then mpeleke nyumbani kwako hapo na mkeo mpe taarifa tu bila kutaka maoni wala ushauri au ridhaa yake.

Mwambie tu kuanzia sasa huyu dada ndie atakuwa anatusaidia kazi za ndani kwasababu nimeona kwako ni nyingi sana zinakuelemea. Akileta ligi mwambie haupo tayari kufanya mazungumzo yoyote wala negotiations zozote zile na hautabadili maamuzi akubaliane na huo uamuzi wako maana ni wa mwisho.

Kisha house girl aanze kazi mara moja. Utaona kama huyo mkeo hajaomba poo. Katika kitu mwanamke hapendi kuona ni mwanamke mwenzake akifanya shughuli za nyumbani kwake kwa umakini na kwa ufanisi kumshinda hadi mume wake anafurahia na kuridhika.

Utaona anaanza kuleta ligi na huyo dada, ukiona analeta ghubu kwa huyo dada mvute pembeni umseme kwa kumkemea kuwa huo upuuzi anaoleta ni utoto sababu yeye ndie amesababisha hadi mnafikia hatua hiyo ya kuleta msaidizi wa kazi hapo ndani sababu ya uzembe na uvivu wake.

Akisema basi atajirekebisha mwambie Hapana. Hapo huyo dada wa kazi atakaa hadi mwaka uishe ndipo haya mazungumzo yatakuwapo wakati wa kurenew mkataba.
 
Back
Top Bottom