Mzazi mwenzangu wangu mvivu

Mzazi mwenzangu wangu mvivu

Iko hivii, binti anapotaka kuolewa huwa anawekwa ndani na wanawake watu wazima sana tu anafundishwa juu ya maisha mapya, majukumu na wajibu katika familia anayoenda anzisha.
Sasa wewe umefanya shortcut umemweka ndani kabla, hivyo inaonekana binti hajajiandaa kuyakabili majukumu yake na kama hana uzoefu wa asili wa kutoka kwao lazima iwe changamoto kubwa.
 
Uzi wa tatu huu ndani ya wiki moja wakilalamikiwa wadada tabia za uchafu, uvivu na kutokuwa waaminifu.
Huyo bila shaka ni Bonge, mademu mabonge ni wavivu sana.
Kaoe Mbeya wadada wachapakazi. Wife wangu kila nikimwambia nikuletee house girl hataki anasema kama nina pesa nyingi nimlipe yeye. Anapiga majukumu yote kila siku bila malalamiko.
Huyo huenda utoto unamsumbua au alilelewa vibaya kwao.
Mvumilie
Duh aiseeee
 
Habari zakupotezana ndugu zangu Wana jf wenzangu....

Mwezi wasita mwaka huu mzazi mwenzangu aliniomba aje aishi kwangu maana haileti picha nzurii yeye kuendelea kuishi kwao hali yakuwa anamtoto namda huohuo mimi mzazi mwenzie nipo hajisikii vizuri. Nikaona nikweli alafu ukizingatia anamtoto wangu, nampenda, naninamalengo nae.,kwahiyo nikaona nivizuri aje tuishi tu.

Mwanzo mzuri kila mtu akawa anasimamia majukumu yake vyema. Ila nikagundua anaasili yauchafu, vilevile nimvivu sio kidogo.

Akaanza tabia yakuniwekesha net, nikaona sio mbaya ila hali ilipozidi siku moja nikamgomea, alichonijibu kuwa 'kila siku awe anaweka yeye tuu'. Hiyo kauli ilinikera sana ila aliweka tukalala kila mtu nahamsini zake.

Maisha yakaendelea ila kwakusumbuana sana kuhusu usafi wandani. Kwahiyo Amani haipo yakutosha maana akiambiwa kuhusu usafi, kupanga vitu vizuri anakuwa mbogo.

Sasa wiki iliyopita nimetoka zangu katika mizunguko yangu, akaniuliza unakunywa Chai nikamjibu ndio, maana toka aje hapa ishamwambia usiku chai awe anahakikisha inakuwepo kama sio maziwa yaani kati yahivyo viwili. Kumbe mda ananiuliza kuhusu kunywa Chai mda huo Chai hamna kwahiyo alichonijibu kuwa makazi yamemchosha amepika vingi. Kwahiyo akapika chai ila kwashingo upande.

Mda mwingi amekuwa analalamika makazi mengi, wakati tunaishi chumba kimoja na sebule namtoto tunaye mmoja tu! Sasa hizo kazi nyingi anazolalamikia najiuliza zipo wapi? Yaani anajihisi kama vile nimtumwa kufanya majukumu yahapa nyumbani wakati anashinda nyumbani. Nasio kusema ninamaisha mazurii labda ninahemeaga mboga 7 ila mara nyingi huwa nahemea mboga moja naukikuta tunakula mboga mbili ujue hiyo nyingine ilibakia mchana...... Sasa hapo kazi zipo wapi? Kama kufua huwa anafua mara moja kwawiki ila yeye nikaribia siku zote zawiki analalamika kuchoka.

Huyu nimwanamke wangu wakwanza kuishi nae na nilikuwa ninashauku yakuishi nae ila najihisi kukinai kuishi namwanamke. Imefikia hatua hata hisia nae zimekata kutokana navimanenomaneno, namigogoro yahapa napale maana hazipiti siku 3 bila kukwaruzana.

Kutokana natabia zake nimedhamiria/nahitaji kumswaga ila mara nyingi nikitaka kufanya hivyo amekuwa akigoma nakuomba msamaha ila mtaishije maisha yakuombana misamaha kila siku?

Ee Mungu niepushe nahuu msalaba. Nakama hayupo tayari kujirekebisha namuomba Mungu tuachane kwaamani yaani akubali matokeo arudi kwao maana mimi kwaupande wangu ishajipima kuwa siwezi kumvumilia na hizo tabia zake.

RIP Benjamin williamu mkapa.
Kaka hilo jipu timuaa
 
Wanawake wa hivyo wakiwa barabarani ni wasafi balaa ni wazuri kinoma ila sehem wanazolala Ni kama jalala,,,, naamin wakat unamtongoza mwanzo ulikutana nae kajiremba sana[emoji1] kumbe mchafu
Kuna kaka tunafanya nae kazi aliweka malengo haoi mpaka amalize kujenga nyumba. Alimaliza kujenga nyumba na ilikuwa nzuri safi sana. Tulikwenda kumtembelea akiwa anaumwa. Wote tulibaki tunasema atakaeolewa na yule kaka amepata.

Alitangaza ndoa, tulitoa michango, baada ya harusi tulikwenda kumuona bibi harusi. Kufika nyumba hovyo hovyo hata mwenyewe anajishtukia.

Baada ya uzazi tulikwenda kumuona mtoto, mwenyewe alisema ni mama yake ndiyo anajiongeza kusafisha nyumba mke na huo uzazi ndiyo ikawa sababu.

Lakini ameamua kumpenda na mapungufu yake. Ukimuona nje msafi ndani mh.
 
Kuna kaka tunafanya nae kazi aliweka malengo haki mpaka amalize kujenga nyumba. Alimaliza kujenga nyumba na ilikuwa nzuri safi sana. Tulikwenda kumtembelea akiwa anaumwa. Wote tulibaki tunasema atakaeolewa na yule kaka amepata.

Alitangaza ndoa, tulitoa michango, baada ya harusi tulikwenda kumuona bibi harusi. Kufika nyumba hovyo hovyo hata mwenyewe anajishtukia.

Baada ya uzazi tulikwenda kumuona mtoto, mwenyewe alisema ni mama yake ndiyo anajiongeza kusafisha nyumba mke na huo uzazi ndiyo ikawa sababu.

Lakini ameamua kumpenda na mapungufu yake. Ukimuona nje msafi ndani mh.
Huyu wangu kweli nae njee msafi sana ila sasa ndani ndio hivyo kwanza kwanjee nimpole sana
 
Iko hivii, binti anapotaka kuolewa huwa anawekwa ndani na wanawake watu wazima sana tu anafundishwa juu ya maisha mapya, majukumu na wajibu katika familia anayoenda anzisha.
Sasa wewe umefanya shortcut umemweka ndani kabla, hivyo inaonekana binti hajajiandaa kuyakabili majukumu yake kama na hana uzoefu wa asili wa kutoka kwao lazima iwe changamoto kubwa.
Kwahiyo itabidi nimrudishe kwao mkuu ila sasa hatakiiiiii
 
Mi nilidhani mzigo huupati kisawasawa, huku niliko makungwi wanawafunda mabinti kwa kuwaambia hata ukiwa hujui kupika ila ukiperform vyema kitandani mumeo atakupikia, atakuoshea vyombo, atadeki , atafua, kwa furaha zote
Ni wapi huko? Hawajui kuwa sikuhizi kuna mabinti wazuri, wasomi na wanaweza yote ya ndani!
 
Back
Top Bottom