Mzazi mwenzangu ameolewa, nifuate hatua gani nimchukue mwanangu?

Mtoto mwenyewe ndo kafikisha miaka minne, ila nilikuwa na mpango kwamba akifikisha miaka saba hadi kumi hapo niende nimchukue kijana wangu, nipo tayari kulipa fidia zote. Vipi hili mahakama inalichukuliaje???
Mtoto sio maembe kuwa yakikomaa tu unayakuta yanauzwa.

TUMIA BUSARA NA MBINU YENYE AKILI UJENGE MAHUSIANO BORA KWANZA NA MWANAO. MTOTO AKUKUBALI KAMA BABA.

Miaka saba hadi kumi umchukue unadhani ni rahisi kwake kutengana na mama yake aje kwa stranger ampende ghafla tu amuite baba?

Hatua ya kwanza tuma wazee wenye busara kwa binti wakaipiganie damu yenu kwa kufuata taratibu huku wewe ukiangalia namna angalau kila weekend upate hata dk 5 za kumuuliza mwanao kama hajambo. USIANZISHE VITA YA WAZI WAZI MAANA HUTASHINDA. VITA IWE YA KIMYA KIMYA SANA NA UWE NA SUBIRA.
 
Asante mkuu..
Usisubiri miaka 8. Tumia wazee uangalie namna ya kuwa na ukaribu na mwanao kuanzia sasa.

una vita mbili.
Moja mama wa mtoto mwenye mwanao ambaye huenda ana na wadogo zake mwanao ambao si wanao.

Mbili mwanao ambaye yupo karibu na mama yake na baba yake wa kambo na ndugu zake kuliko wewe.

TUMIA BUSARA.
 
Wakuu habarini A muda huu, nina jambo moja linalonitatanisha.

Hapo nyuma, miaka mitano iliyopita, nilikuw katika mahusiano na mdada mmoja kipindi nipo shule, ila yeye alikuwa hasomi, mahusiano yetu yalikuwa ya wazi pande zote mbili (kwa wazazi wake na wazazi wangu).

Hamna chuki yoyote iliwahi kutokea, kwa kweli tulipendana sana..
Utani ulikuwepo kati ya wazazi wetu mara ooh, mwanangu atamuoa mwanao😃, mara ooh.. ko ndo kama hivyo.
Katika safari yetu ya mahusiano, TULIFANIKIWA KUPATA MTOTO WA KIUME.

ko mambo yaliendelea vizuri tu..
Kulingana na mie kupangiwa shule mbali ma nyumbani, tulikuwa mbali kwa kweli, kiasi kwamba kuonana kulikuwa vigumu.

Baada ya muda tu, kitu kama miaka miwili baada ya mie kuenda shule, nilipewa taarifa kwamba huyo mdada kaolewa, kitu ambacho kiliniumiza sana, kwa kuwa nilikuw shule na mtihani ukikaribia, nilijikaza kisabuni na kuvumilia kikondoo..
Siku baada ya siku, mawasiliano yalianza kufifia kwa maana sikutaka kumharibia ndoa yake.

Mamkwe naye alikuwa anakata simu yangu kila nilipompigia..
Kwa kuwa yule mtoto alibaki pale kwa bibi yake, nilitaka nitume matumizi madogo madogo, lakini kila nilipompigia yule Mamkwe simu, alikuwa hapokei.. siku zilienda mpaka mtoto kafuatwa na mamaake, hadi saa mtoto yupo na mamaake na babaake huyo mpya.

Swali langu,
Je! kisheria naweza kuchukua mwanangu hata kama mama yake hayupo tayari kunipa mwanangu???
Na vipi, kama ndiyo, hatua gani za kufuata??
MSAADA wenu wakuu..
Natanguliza shukran

Unampeleka Wapi? Bora akae Kwa Bibi wa mke au Kwa Mama yako ; hawezi Kaa kwako "huna mke" Na Ni hatari Sana kukaa huko! Ukishajua pa kumpeleka kumchukua sio shida!
 
Mtoto sio maembe kuwa yakikomaa tu unayakuta yanauzwa.

TUMIA BUSARA NA MBINU YENYE AKILI UJENGE MAHUSIANO BORA KWANZA NA MWANAO. MTOTO AKUKUBALI KAMA BABA.

Miaka saba hadi kumi umchukue unadhani ni rahisi kwake kutengana na mama yake aje kwa stranger ampende ghafla tu amuite baba?

Hatua ya kwanza tuma wazee wenye busara kwa binti wakaipiganie damu yenu kwa kufuata taratibu huku wewe ukiangalia namna angalau kila weekend upate hata dk 5 za kumuuliza mwanao kama hajambo. USIANZISHE VITA YA WAZI WAZI MAANA HUTASHINDA. VITA IWE YA KIMYA KIMYA SANA NA UWE NA SUBIRA.

Anamchukua Ni stage 1, anampeleka Wapi Ni stage 2; stage 2 is more important than 1
 
Mkuu pole sn kwa changamoto uliyonayo.

Lakini mm nataka nikupe code 1.
Nina 99% pengine huyo jamaa aliyeoa mama mtoto wako ,,ndy mwenye huyo mtoto unayelalama ni wako.

Wanawake sio watu wazuri.
Nimewaza hivyo hivyo. Jamaa anatakiwa apime DNA uenda mtoto si wake
 
True, na stage 3 ya kuzingatia ni huyo mtoto ana mahusiano gani na yeye kukubali hiyo stage 2 bila madhara ya kisaikolojia.
Mkuu, yaani ni hivi, huku kwetu kuna tabia fulani hivi, ikitokea mdada ameolewa akiwa na mtoto wa kike, huyo mtoto anapendwa sana na familia ya hapo alipoolewa kwa sababu baada ya siku huyo mtoto ataolewa..
Ikitokea mdada ameolewa akiwa na mtoto wa kiume, kuna mawili yanaweza kutokea; either kutokupendwa na baba yake huyo mpya, kiasi kwamba anaweza kutengwa na watoto wengine, au anaweza kuwawa kabisa kwa sababu wanajua mtoto wa kiume akishakuwa anaweza kuchukua maamuzi magumu baada ya kusikia skendo et hakuzaliwa katika hiyo familia,.
Kwa hiyo siwasumbui bure, ni vile tu namhurumia mwanangu..
Nyie niambieni kama mahakama inaweza ikasimama kati ili muda ukifika nije nichukue na kufuata hatua inayoeleweka.
 
mtoto sio wako mkuu ni wa uyo mzazi mwenzako kwa maana wewe hukumuoa kama hujaoa mtot anakuwa wa mwanamke ushauri tafuta mke oa zaa mwingine ndo atakuw wako.
 
Duu, mtoto si wangu kivip mkuu??
Umetumia kigezo gani boss??
 
Mkuu acha unyonge,peleka moto mabinti kibao wana vizazi utapata wengine,ukimchukua huyo mtoto unaweza kumlea wewe mwenyewe?
 
Wakuu habarini A muda huu, nina jambo moja linalonitatanisha.

Hapo nyuma, miaka mitano iliyopita, nilikuw katika mahusiano na mdada mmoja kipindi nipo shule, ila yeye alikuwa hasomi, mahusiano yetu yalikuwa ya wazi pande zote mbili (kwa wazazi wake na wazazi wangu).

Hamna chuki yoyote iliwahi kutokea, kwa kweli tulipendana sana..
Utani ulikuwepo kati ya wazazi wetu mara ooh, mwanangu atamuoa mwanao😃, mara ooh.. ko ndo kama hivyo.
Katika safari yetu ya mahusiano, TULIFANIKIWA KUPATA MTOTO WA KIUME.

ko mambo yaliendelea vizuri tu..
Kulingana na mie kupangiwa shule mbali ma nyumbani, tulikuwa mbali kwa kweli, kiasi kwamba kuonana kulikuwa vigumu.

Baada ya muda tu, kitu kama miaka miwili baada ya mie kuenda shule, nilipewa taarifa kwamba huyo mdada kaolewa, kitu ambacho kiliniumiza sana, kwa kuwa nilikuw shule na mtihani ukikaribia, nilijikaza kisabuni na kuvumilia kikondoo..
Siku baada ya siku, mawasiliano yalianza kufifia kwa maana sikutaka kumharibia ndoa yake.

Mamkwe naye alikuwa anakata simu yangu kila nilipompigia..
Kwa kuwa yule mtoto alibaki pale kwa bibi yake, nilitaka nitume matumizi madogo madogo, lakini kila nilipompigia yule Mamkwe simu, alikuwa hapokei.. siku zilienda mpaka mtoto kafuatwa na mamaake, hadi saa mtoto yupo na mamaake na babaake huyo mpya.

Swali langu,
Je! kisheria naweza kuchukua mwanangu hata kama mama yake hayupo tayari kunipa mwanangu???
Na vipi, kama ndiyo, hatua gani za kufuata??
MSAADA wenu wakuu..
Natanguliza shukran
Just mute and wait , after 10yrs
Good results will prompt you.
Wanawake wako hivyo.
 
Back
Top Bottom