kedekede
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 5,298
- 7,646
Wakuu nawasalimu!
Moja Kwa moja naandika.
Nilizaa na dada mwaka 2006 kama sikosei, nikiwa na ndoa, mke wangu alijua yakaisha. Nilitunza mtoto na kulipa huduma ila baadaye tukagombana tukatulia nikawa nimemute. 2009 akajirudi Kwa ajili ya mtoto akiwa na kama 3 yrs nikaendelea kumtunza ila baada ya muda tukagombana nikapigwa block kumuona Mtoto.
Nilikubali block maisha yakaendelea. Sikumuona mtoto hadi Leo. Juzi mama mtoto amenitafuta Kwa kushinikizwa na binti yangu huyo. Amenitafuta kupitia rafiki yangu maana mimi nilibadilisha namba na yake siijui. Binti huyu yupo boarding sijui yupo shule ipi Wala darasa la ngapi. Nimetumiwa picha za mwanangu amekuwa binti mkubwa ambaye simjui Wala kumfahamu.
Hakika najiskia vibaya mno kutomlea binti yangu Hadi yeye amenitafuta. Sikupaswa kumsikiliza yule mwanamke ili niwe na ukaribu na mwanangu. Najiuliza nitaongea Nini na mwanangu Kwa mara ya kwanza tukionana? Kuna mtu ashawahi kukutana na hali hii? Am very emotional sijui what will happen between us? Binti yangu ananifikiriaje?Ana yapi yakunieleza? Nimjibu Nini akiniuliza nilikuwa wapi miaka yote?Nimjibu Nini akiniuliza Kwa Nini niliachana na mamaake? Nimjibu Nini ndugu zangu? Av missed birthday zake nyingi, nimemiss so many things between us sijui naanzia wapi. Sijui ameambiwa Mangapi ya uongo na mamaake.
Note /sikumbuki mwaka exactly aliozaliwa sijui ni 2006 au 2007, sijui tarehe yake ya kuzaliwa. Nimeongea na mamaake amekataa kudisclose any more information Hadi April nikienda kuonana naye. Nimechanganyikiwa sijui naanzia wapi nipeni ushauri utakaonifaa. Kwa sasa sihitaji lawama.
Asanteni.