Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,777
- 41,066
Hili suala la Darwin's Nightmare na mwitikio wa viongozi wetu, umenilazimisha kujiuliza swali, "mzalendo ni nani?". Kama ulisikiliza mahojiano yangu na Waziri M. S. Khatib (MB)nilimuuliza kwa nini serikali imechukua karibu miaka minne tangu filamu itoke ndio ionyeshwe kutokufurahia kwake na iweje wabunge wadandie behewa la kuilaani filamu hiyo lililoanzishwa na JK. Jibu lake ni kuwa walifanya hivyo ili kumuunga mkono Rais "wao" na pia kuonyesha uzalendo.
Baadaye vikundi kadhaa vimerukia suala hili kiasi kwamba sauti yoyote inayoonekena kupinga au kuonyesha upande mwingine inadaiwa kuwa sauti hiyo si ya kizalendo. Kinachonitia hofu zaidi ni kuwa mtu yeyota anaye au atakaye ikosoa serikali ya Mhe. Kikwete au kuonyesha mapungufu fulani basi ana hatari ya kubandikwa jina la "si mzalendo"! Wote tunatakiwa tujipange mstari, tupige makofi na kusema ndio mzee kwa kila anachofanya mhe. Rais.
Na zaidi ya yote, wale ambao tuko nje ya nchi kwa sababu fulani, basi tunatakiwa tusitoe maoni yetu kabisa kwani "hatujui kinachoendelea nyumbani" na kwa sababu "tuliondoka". Imefikia wakati baadhi ya watu kwenye serikali hii tukufu (sijui utukufu wake unatoka wapi?) na bunge letu takatifu (hata hilo sijui imelipataje?) wako tayari kunyamazisha sauti za Watanzania walioko nje kwa kisingizio cha kuwa hawa si "wenzetu". Kwa mujibu wa watu hao, wazalendo wa kweli ni wale waliobakia Tanzania ambao wanajua kila kitu kinachoendelea. Wale walioko nje hawaelewi kuwa watanzania hawali mapanki, n.k
Sijui sasa, mzalendo ni nani? Ni yule ambaye anakaa kimya wakati nchi yake inavunjwa vunjwa au ni yule anayepiga kelele kukataza watu kuivunja nchi yake? Je ni yule ambaye amekaa karibu na JK na viongozi wengine na kuwaambia wale "watakayo kuyasikia" badala ya kuwaambia yale "yaliyotukia"? Mzalendo ni nani basi? Je ni yule ambaye baada ya kuchaguliwa au kuteuliwa na kupewa nafasi ya kuitumikia nchi yake anaanza kujichumia mali za kila aina, kuuingiza serikali kwenye mikataba bomu, kufuja fedha kulia na kushoto akijua hakuna mwenye ubavu wa kumgusa? Nauliza mzalendo ni nani? Ni yule ambaye kwa sababu anazozijua anaogopa au hataki kuwafungulia mashtaka wale wote waliofuja fedha za umma, walioiingiza serikali kwenye mikataba bomu, na waliotumia nafasi zao kujitajirisha pasipo halali? Kama mtu anayeamka asubuhi na wazo la kwanza kichwani mwake ni Tanzania na siyo tumbo, mtu ambaye anajaribu kutekeleza majukumu yake kwa nguvu zake, badala ya kufikiria ni jinsi gani apinde sheria fulani ili yeye au mtu fulani anufaike, au ambaye anasimama kidete na kusema kuwa kitu fulani si sahii licha ya wakubwa kutokumuunga mkono. Kama mtu huyo si mzalendo.. mniambie mzalendo ni nani basi?