Mzalendo ni Nani?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,462
39,928
Hili suala la Darwin's Nightmare na mwitikio wa viongozi wetu, umenilazimisha kujiuliza swali, "mzalendo ni nani?". Kama ulisikiliza mahojiano yangu na Waziri M. S. Khatib (MB)nilimuuliza kwa nini serikali imechukua karibu miaka minne tangu filamu itoke ndio ionyeshwe kutokufurahia kwake na iweje wabunge wadandie behewa la kuilaani filamu hiyo lililoanzishwa na JK. Jibu lake ni kuwa walifanya hivyo ili kumuunga mkono Rais "wao" na pia kuonyesha uzalendo.

Baadaye vikundi kadhaa vimerukia suala hili kiasi kwamba sauti yoyote inayoonekena kupinga au kuonyesha upande mwingine inadaiwa kuwa sauti hiyo si ya kizalendo. Kinachonitia hofu zaidi ni kuwa mtu yeyota anaye au atakaye ikosoa serikali ya Mhe. Kikwete au kuonyesha mapungufu fulani basi ana hatari ya kubandikwa jina la "si mzalendo"! Wote tunatakiwa tujipange mstari, tupige makofi na kusema ndio mzee kwa kila anachofanya mhe. Rais.

Na zaidi ya yote, wale ambao tuko nje ya nchi kwa sababu fulani, basi tunatakiwa tusitoe maoni yetu kabisa kwani "hatujui kinachoendelea nyumbani" na kwa sababu "tuliondoka". Imefikia wakati baadhi ya watu kwenye serikali hii tukufu (sijui utukufu wake unatoka wapi?) na bunge letu takatifu (hata hilo sijui imelipataje?) wako tayari kunyamazisha sauti za Watanzania walioko nje kwa kisingizio cha kuwa hawa si "wenzetu". Kwa mujibu wa watu hao, wazalendo wa kweli ni wale waliobakia Tanzania ambao wanajua kila kitu kinachoendelea. Wale walioko nje hawaelewi kuwa watanzania hawali mapanki, n.k

Sijui sasa, mzalendo ni nani? Ni yule ambaye anakaa kimya wakati nchi yake inavunjwa vunjwa au ni yule anayepiga kelele kukataza watu kuivunja nchi yake? Je ni yule ambaye amekaa karibu na JK na viongozi wengine na kuwaambia wale "watakayo kuyasikia" badala ya kuwaambia yale "yaliyotukia"? Mzalendo ni nani basi? Je ni yule ambaye baada ya kuchaguliwa au kuteuliwa na kupewa nafasi ya kuitumikia nchi yake anaanza kujichumia mali za kila aina, kuuingiza serikali kwenye mikataba bomu, kufuja fedha kulia na kushoto akijua hakuna mwenye ubavu wa kumgusa? Nauliza mzalendo ni nani? Ni yule ambaye kwa sababu anazozijua anaogopa au hataki kuwafungulia mashtaka wale wote waliofuja fedha za umma, walioiingiza serikali kwenye mikataba bomu, na waliotumia nafasi zao kujitajirisha pasipo halali? Kama mtu anayeamka asubuhi na wazo la kwanza kichwani mwake ni Tanzania na siyo tumbo, mtu ambaye anajaribu kutekeleza majukumu yake kwa nguvu zake, badala ya kufikiria ni jinsi gani apinde sheria fulani ili yeye au mtu fulani anufaike, au ambaye anasimama kidete na kusema kuwa kitu fulani si sahii licha ya wakubwa kutokumuunga mkono. Kama mtu huyo si mzalendo.. mniambie mzalendo ni nani basi?
 
Mzee Mwanakijiji

Umeuliza swali kwamba Mzalendo ni nani ?

Nakujibu mimi Murangira ndiye mzalendo ambaye natembea nalilia Nchi yangu kuliwa , ambaye ninasema kwamba sinema ile ya Mapanki ni ya kweli na sasa Serikali iamue kutumia pato la samaki kunyoosha maisha ya watanzania wa Kanda ya ziwa na wapiga kura wa CCM, ambaye nasema kwa uwazi wewe Lowasa na JK si wasafi mna mchezo ambao bado haujajulikana lakini mimi Murangira nimesha jua kwamba kuna magarini kwenye sirikali hii ya awamu ya 4 , mzalendo ni mimi ambaye nasema Watanzania wako nyuma na watabaki nyuma kwa maendeleo maana kasi mpya ya JK na Lowasa ni ya maneno na maeneo wanayofika ili kuficha ukweli , mzalendo ni mimi ninasema kwamba JK usitagawe kwa tabia zako za urafiki na uwapendao kikanda , kidini na hata katika mission zako za totozi , mzalendo ni mimi ninasema kwamba sirikali inatumia nguvu kubwa kuuzima sinema ya mapanki inaficha nini ? Mzalendo ni mimi nauliza kwa nini Magazeti ya Tanzania yako kimya hayasemi maovu ya sirikali ya JK nandoa yao itadumu hadi lini?Mzalendo mimi nahoji DCI kwa nini hajatueleza juu ya skando la ku foji vyeti na watu kuitwa Dr.Bungeni kwa nini wewe DCI unakali habari hizi na kwa nin magazeti hayaulizi ?Mzalendo nini nahoji uhalali wa kufikiria Waziri kupewa uwezo wa kuteua madiwani 3 kila wilaya kwa Nchi nzima badala ya kuchaguliwa .

Mzalendo ni mimi nasema inatakiwa elimu ya Uzalendo ili watot wetu wawe watanzania wa kweli na mwisho nasema mzalendo ni wewe na mimi ambao tunaikosoa serikali ikikosea na kuipa pongezi ikipatia na kuipa chalenji kutenda zaidi maana ni wajibu wake , mzalendo ni mimi nasema hapa kununua ndege mpya ya Rais ila zahati ziwe nyingi , ondoa malaria, lipieni watoto wasome Vyuo Vikuu .

Mimi Murangira ndiye mzalendo .
 
  • Thanks
Reactions: C.K
Tatizo kubwa sana tulilo nalo pale nyumbani ni kwamba watu wameweka maslahi binafsi mbele at the expense of wananchi. Kila mtu anapogombea cheo, anatoa ahadi nzuri sana ambazo hazitekelezwi hata siku moja.

Hii inatokana na system yetu ya utawala kukosa mechanisms for checks and balance. Hapo nina maana kuwa kuna watu ambao wako kwenye high positions ili hali wana very serious conflict of interests, the likes of Karamagi & Mwasha. With all fairness how can Karamagi make a very strong decision against TICTS/whatever if need arises? Hapa UK Deputy PM aliwashiwa moto mkali sana baada ya kugundulika kuwa alikirimiwa na tycoon wa US ambaye anataka kuwekeza kwenye casino. This makes politicians in a democratic country always to be on their heels na kuaacha longolongo.

Tutapata mabadiliko tu kama tutapata kiongozi kwenye highest position ambaye hakutoka kwenye inner circle ya CCM (unfortunately opposition is still very weak). Kila nikikaa chini na kuimagine situation ambapo JK analetewa file/tuhuma za ufisadi from one of the vigogo wa chama/serikali ambao ndio wamemlea kichama/kiserikali mpaka akafika hapo alipo, je anaweza kumchukulia hatua za kisheria? it needs someone with very strong guts like Fidel Castro ambaye aliidhinisha adhabu ya kifo kwa jamaa yake waliepigana naye bega kwa bega msituni kwa kuwa alitiwa hatiani kwa kushiriki biashara ya madawa ya kulevya which carries death penalty.

In short I don't see a very bright future with the current trend, wananchi walio wengi wataendelea kupigika tu!

All in all wazalendo lets keep on shouting, sauti zikiongezeka watatusikia and hopefully things will change, its better than sitting idle
 
mTz hivi maelezo yako yanajibu swali na muuliza swali ama ni mimi sielewi? Hebu nisaidie tuone tafadjali. Naomba ueleze Mzalendo ni nani ? Ni mtu wa aina gani ? Ana sifa gani ? Au mimi ndiye sijaelewa ?
 
Mzeeshughuli Bwana,

Suala la uzalendo kwa mtizamo wagu linakuwa reflected na system ya uongozi. Ideal uzalendo ni kwamba unasimama kwa nchi yako no matter what! Mfano mzuri ni waisraeli, nilikuwa nikifuatilia mgogoro wa Israel na Lebanon, Kila mwisrael popote duaniani alipohojiwa alikuwa anatetea nchi yake na kubondea sana Hizbolah, Iran na Syria regardless kama nchi yao ilikuwa inatumia nguvu kupindukia na kuua raia wasio na hatia. Wanajua nini matunda yake, kuwa ile nchi ndio wanaita nyumbani na wakiamua kwenda wanakaribishwa na waziri mkuu wa nchi na kupewa almost mahitaji yote.

Ideally, huo ndio ni uzalendo ambao mimi na wewe tulitakiwa kuwa nao hata kuitetea nchi yetu katika saga ya mapanki. Sasa tatizo linakuja hata ukitetea hali ya nyumbani inakusuta. Leo hii nasikia serikalia inataka kununua ndege kadhaa ili zisaidie kufika kusikofikika, huku kunaishi ndugu zetu, mimi na wewe tukitaka kwenda kusalimia watatupa hiyo ndege? kwa nini wasitumie hiyo pesa kujenga barabara ya lami ili kufikike na wananchi wote kama mimi na wewe? nusu ya budget tunategemea pesa za wafadhili halafu wakati huo huo tunatoa misamaha ya kodi lukuki kwa makampuni ya nje. Mbona serikali haijafikiria kumsamehe kodi mfanyakazi wa Tanzania hata kwa mwezi mmoja tu? kila mwisho wa mwezi lazima PAYE ikatwe!
 
Hivyo swali linaendelea kubakia.. mzalendo ni nani? Yule anayesimama kumtetea Rais wake kwenye masuala ya mapanki au yule anayesima tusinunue ndege zisizo za lazima, tutumie fedha hivyo vingine? Au wote ni wazalendo kwa namna tofauti?
 
Wanabodi,

Mzalendo ni mtu mwenye uchungu na kilicho chake (mwenye mapenzi ya kweli na muwazi), hatotaka kilicho chake kipotee (atalinda), bali kiwe na maendeleo mazuri (atajenga), na atafanya kila juhudi kuhakikisha hilo linakuwa (atadumisha).

sasa hapo weka jina lolote, halafu angalia na hata ktk safu ya viongozi wetu, kama wana-fit.

Nikiangalia humu ndani ya bodi hii, watu wengi ni wazalendo.
 
Hivyo mzalendo siyo anayeshabakia nchi yake na kusema.. "iwe vita au amani hii nchi yangu"?
 
Binafsi nionavyo mimi, mzalendo ni mtu ambaye ana moyo wa dhati katika jambo fulani ambapo yeye atahakikisha anasimamia na kulinda maslahi ya kila mdau kuhusiana na jambo husikka,mathalani viongozi wetu ambao tumewapa jukumu la kuhakikisha wanatuongoza sisi kama taifa katika mchakato mzima wa kajiletea maendeleo yetu wanatakiwa kutokuwa na chembe ya ubinafsi,hata kidogo.lakini kitendo chao cha kuyatumia madaraka vibaya kama vile kukubali kusaini mikataba mibovu pamoja na ufujaji wa mali za umma, hii inatuonyesha viongozi tulionao hakuna hata mmoja ambaye ni mzalendo wa kweli,

Mzalendo anatakiwa kuwa na msimamo katika maamujzi yake na hata kuhakikisha anawahamasisha watu wengine kuwa misimamo sahihi haswa katika suala ambalo anaona lina manufaa kwa kila raia,mfano ni pale Mwl nyerere alipowakatalia wazungu kuchimba madini, na kuwaambia yatachimbwa na watanzania wenyewe watapokuwa na akili, sasa nyerere alifanya hivi makusudi ili,kila mwananchi aweze kufaidika na madini, lakini embu angalia leo watu wengine wamepewa madaraka wakatuingiza kwenye mikataba feki kabisa,

Mzalendo ni mtu ambaye anatakiwa awe ana mtazamo chanya kuhusiana na mustakabali wa jamii yake inayomzunguka, ni yule ambaye atakuwa yuko radhi kufanya kila jitihada ili aweze kuhakikisha anatafuta ufumbuzi wa busara jamiii yake kuhusiana na matatatizo yanayoikabili na sio kuwa kinara wa kuongeza matatizo katika jamii,mfano embu angalia viongozi wetu wanavyoutuongezea matataizo,wizi wa EPA,MEREMETA,RICHMOND, DOWANS,KIWIRA COAL MINES, nk

Mzalendo ni mtu ambaye yupo tayari kujitoa mhanga kupigania maslahi ya jamii yake pale anapoona jambo fulani au maaamuzi fulani yanaleta au yataleta shida kwa jamiii husika,kwahiyo ni mtu ambaye yupo radhi kuipigania jamiii yake hata kupoteza maisha yake mfano,Che Guavara,

Mzalendo anatakiwa awe mtu ambaye ana maono na mitazamo yenye kuleta tija katika jamii yake,anatakiwa awe mtu mwenye uwezo wa kufanya vitu kwa ubunifu zaidi na kujua vizuri mazingira ya jamiii yake na mabadiliko yanayotoke katika jamii hiyo kadri muda unavyokwenda,

Mzalendo ni mtu anayefanya mambo kwa vitendo na sio kwa maneno, yaani ni mtu ambaye anahakikisha anatekeleza kile anachokisema na kuwahamasisha watu wengine washirikiane nae katika kufankikisha lile ambalo kila mwanajamiii ataona kuwa lina manufaaa na linahitajika kufanywa kwa wakati huo,mfano kipindi cha mapinduzi ya Urusi watu wote wa kada ya chini ambao walikuwa wananyonywa walihamasishwa na walihamasika na kumuunga mkono bwana illyich na kufanikiwa kuleta mapinduzi ya kweli

Mzalendo anatakiwa awe objective yaaani value free hatakiwi kuwa bias, kwahiyo anatakiwa awe mwepesi kukubali kukosolewa na kukubali maoni na mitazamo ya wengine katika jamiii,anatakiwa awe mtu wa kujifunza kila siku mambo mabalimbali yanayoizunguka jamii yake.

lakini kwa hapa Tanzania tuliokuwa nao wengi wazalendo uchwara yaani feki kabisa,waliojitahidi kuonyesha uzalendo ni SOKOINE na NYERERE TU.
 
Pamoja na hoja duni zilizojengwa na Mukulu pamoja na serikali kuhusu filamu hii. This was the only time nilimuona JK akifoka na kuwa mkali kabisa. Jiulizeni kwa nini??????. Mbona haya mengine tunasimuliwa tu oooh! mkulu amekasirika sana na ameahidi kuchukua hatua kali........kinachobaki stori tu!!!!!!!!Sorry to go offline!!!!!!!
 
katika kitabu changu kinachoitwa "Adha ya Heri" nimejaribu kuzungumza mengi na pia kujaribu kugusia suala hilo la uzalendo. mzalendo si lazima awe na ngozi kama yetu kwa upande wetu ama yao kwa upande wao. uzalendo ni utamaduni. nikajaribu kusema kuwa mtu mzalendo ni yule mwenye sifa mbili kuu-kwanza dhamira iliyo hai na pili uwezo wa kujibainisha-empathy. ukiwa na vitu hivi hata utange vipi, hata uachiwe nini, hata uachwe na nani, bado utasimama katika ukweli tu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom