Goodrich
JF-Expert Member
- Jan 29, 2012
- 2,091
- 1,179
Usizunguke mbuyu!
Kuna Wayahudi wa kabila; mitume wengi katika Uislamu wametokea katika kizazi cha wana wa Israel kwa hiyo ikitokea kwa mfano Jesus ni kutoka katika kabila la Yuda basi yeye anakuwa ni Myahudi wa kabila, na ni Muislamu kwa dini.
Kuna Waislamu wengi tu wa namna hii ambao kabila lao ni Uyahudi (lakini hatutumii kuwaita Wayahudi kwa vile haipendezi).
Halafu kuna Mayahudi wa dini; hawa ndio wale waliobakia katika dini ya Kiyahudi hata ulipokuja Ukristo na baadaye Uislamu.
Au walioiingia katika dini ya Kiyahudi, mfano Maashkenaz (ambao kwa sasa ndio walioiteka dini ya Kiyahudi) ,Waafrika, Waarabu n.k
Inawezekana sana kuwa katika Saudi Arabia na Iraq kuna Waislamu ambao damu zao ni za Kiyahudi.
Kumbuka walikuwepo Madina, baada ya ukorofi wao wakafukuzwa kwenda Khobar mpaka wakati wa Khalifa wa pili Umar bin Khattab akawafukuza kwenda Iraq.Sehemu zote hizi walizokaa kuna ambao walisilimu hivyo ni wazi kuwa damu zao zipo.
Baadhi ya Wasaudi wanadai kuwa Wafalme al-saudi ni kutokana na vizazi hivi.
Hizi sasa ndio siasa !
... hapa umechanganya dini na siasa