Amoeba
JF-Expert Member
- Aug 20, 2009
- 3,289
- 782
Nimekaa hapa nafunguafungua kurasa, kila nikijitahidi kutoka JF nashindwa, nimepitia forum zote nimesoma na kuchangia thread na post ninazoona zinavuta, Nikasema wacha niingie humu, kuingia tu nimejikuta mawazo yanabadilika kabisa, nimemkumbuka sana mke wangu, nimempigia simu nimeongea naye lakn bado namuwaza. KUsema kweli nampenda sana huyu mama, sina hata maneno ya kumfafanulia-ila kwa vitendo tu anajua nampenda!....ah na huu wimbo toka niuweke alfajiri umeloop mpaka sasa, unanifariji sana. Unajua ni wimbo gani mkuu?
Buy Me a Rose-LutherVandross!
Buy Me a Rose-LutherVandross!