My Wedding Anniversary

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810



attachment.php
attachment.php



Leo hii mimi na my wife wangu, tumetimiza miaka kumi na mbili (12) ya ndoa yetu. Na tunamshukuru Mwenyezi Mungu kutujaalia Watoto wenye Afya na siha njema.

Nadiriki kusema kuoa kwangu si kuwa nilichukua tu mke, bali kuoa kwangu ilikuwa ni kukabidhi ulimwengu wangu mzima, uhuru na matamanio yangu yote juu yake. Kuanzia siku ya ndoa yangu mpaka maisha yangu yote.

Mke wangu ndiye mwenzi wangu, mwandani wangu, na rafiki yangu mpenzi, msiri wangu, mshauri wangu, na ndiye mama wa watoto wetu mimi na yeye.

Nadiriki kusema kuwa, my waifu wangu ndiye mke wa ujana wangu na anashiriki katika nyakati zangu nzuri, siku zangu za maisha yangu na miaka yangu. Amekuwa pamoja nami,

nami nimekuwa pamoja naye katika furaha na shida, katika mafanikio na tabu, amekuwa ndiye liwazo langu, maudhi ninayo yapata uko nje yeye ndiye anayenituliza na kuniliwaza na katika kunitia moyo wakati wa hofu na kunitia hamasa za kimaisha.

Tukiudumiana wakati wa ugonjwa na uzima, na diriki kusema kuwa siku zote nimekuwa nikipata huduma bora kabisa kutoka kwake.

Wakati ninapohitaji msaada wa kimawazo yupo karibu yangu. Siri zangu anazitunza na anaendelea kuzitunza, wakati nahitaji ushauri, ananipa na anaendelea kunipa ushauri mzuri kabisa.

Yupo na mimi ninapoamka asubuhi, kitu cha kwanza ambacho macho yangu yanaona ni wajihi na sura yake jamali, na macho yake yenye kuvutia na tabasamu lake linalo amsha hamasa ya kimapenzi, baina yetu wawili.

Wakati wote yupo na mimi, kama kuna wakati mchache ambao hayupo na mimi kimwili, basi nina uhakika kabisa atakuwa ananifikiria, nami namfikiria yeye, tukiombeana dua kwa nyoyo na akili zetu, ili siku ihishe mapema ili tupate kuwa pamoja tena.

Nikienda kulala usiku, kitu cha mwisho macho yangu kuona ni yeye, na hata nikilala bado ninamuona katika ndoto zangu.

Kwa ufupi yeye ndio ulimwengu wangu mzima na yeye ndiye ulimwengu wake mzima.

Hakika sikujua thamani ya kupenda kabla sijaingia kwenye ndoa, leo hii ile thamani ambayo sikuijua, wala kuithamini, nimekuja kuijua miaka kumi na mbli iliyopita, siku ambao nilitamka mbele ya mashaidi, kuwa tutakaa kwa wema na kuchunga mipaka iliyowekwa na Mwenyezi Mungu. Hakika sikujuwa kuwa nimekabidhiwa lulu yenye thamani isiyo kadirika.

Lulu ambayo imeendelea kuangaza ndani ya moyo wangu kila siku ziendazo kwa Mungu.

Ushauri wangu kwa wana ndoa haswa zile zilizo changa ni kwamba: Kamwe usidharau umuhimu wa vitu vidogo vidogo kama vile kulishana chakula, kumsaidia mkeo hata kuosha vyombo na kufua nguo, kupika, kufagia na kumfungulia mlango wa gari, na kadhalika... Kubwa kabisa ni kutabasamu.

Kama ni watu wa dini, basi jaribuni kutafuta wakati ili nyote wawili muweze kuswali pamoja kama nyumbani au kwenye majumba ya ibada.
Kuimarisha uhusiano kati yenu na Mwenyezi Mungu ni hakikisho kubwa kuwa uhusiano wenu wa kindoa utabaki madhubuti. Kuwa na amani kati yenu na Mwenyezi Mungu daima kutapelekea ndani mwenu kuwa na amani zaidi.

Daima jaribu uwezavyo kuwa mtu mzuri kwa mkeo/mmeo kwa njia ya maneno na vitendo. Ongeeni na mcheke, peaneni ushauri, muulizane juu ya mawazo yenu, tumia wakati maalum na yeye na daima kumbuka kwamba mtu aliye bora ni yule ambae ni m'bora kwa familia yake.

Mwisho, ni kawaida kwa wanandoa kuahidi kuwapenda na kuwaheshimu wanandoa wenzao mpaka mauti yawatenganishe. Naamini kwamba ahadi hii ni nzuri au ni bora kabisa, lakini haitoshi! Haitoshi kumpenda mkeo/mmeo tu. Lazima upende anachokipenda pia. Upende familia yake, uwapenda marafiki wema anaowapenda yeye nawe uwapende pia.

Jambo kubwa kabisa ni kuvumiliana na kusameheana pale mnapokoseana.

Nakumbuka kisa kimoja kutoka kwa rafiki yangu, ambaye hakufurahiwa kuja kwa wazazi wa mke wake kukaa kwa wiki chache. Alimwambia mkewe "Mimi siwapendi wazazi wako". Bila ya kusita mkewe alimtazama machoni kwa hasira na kusema, "Na wako pia siwapendi"... unaweza kufikiria mwenyewe baada ya hapo nini kilitokea.



attachment.php




Na katika Ishara zake ni kuwa Amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo ishara kwa watu wanaofikiri.
Ar-Ruum :21





 
Miaka 12 sio mchezo. mi nina miaka 5. Vipi upande wa pili wa ndoa unauongeleaje?, mana kwenye ndoa kuna mabonde na milima wakati mwingine, sio kila siku furaha tu, umepita vipi huko kwa hiyo miaka 12.

Once again Hongera sana mjomba.
 
Hongereni sana, nawaonea raha sana! Mungu azidi kuwajalia maisha marefu yenye upendo, amani na furaha tele katika siku zote za maisha yenu hata kifo kitakapowatenganisha! Amen
 
Miaka 12 sio mchezo. mi nina miaka 5. Vipi upande wa pili wa ndoa unauongeleaje?, mana kwenye ndoa kuna mabonde na milima wakati mwingine, sio kila siku furaha tu, umepita vipi huko kwa hiyo miaka 12.

Once again Hongera sana mjomba.
Mkuu kama utakuwa umenisoma nimedokeza siri ya mafanikio, "Jambo kubwa kabisa ni kuvumiliana na kusameheana pale mnapokoseana."
Na kwa nyongeza muwe tayari kuepuka yale ambayo yatamuuzi mwenzio, maana nyote nyinyi ni wanadamu na mnapenda jinsi vile mnavyopendwa.
 
Hongereni sana, nawaonea raha sana! Mungu azidi kuwajalia maisha marefu yenye upendo, amani na furaha tele katika siku zote za maisha yenu hata kifo kitakapowatenganisha! Amen
Evarm, shukrani sana sana kwa maombi na dua hii njema, iwe pia kwako Evarm.
 
Daaaa hongera sana tena sana mkuu naamini kuna mafanikio mengi sana ndani ya nyumba endapo mtakaa na kuelewana.......
 
ndoa yenu ni mfano wa kuigwa hiyo.
Lakini pia kuna watu ndoa zao ziko kama zina nuksi, mkosi na mabalaa.zimejaa chuki, ghadhabu na kukasirikiana.
 
Back
Top Bottom