My love for kids imeniponza

Don Mangi

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,198
852
Kama kawaida yangu ambavyo situlii mahali pamoja nchi hii ya thelathini kwa ukubwa duniani, katika safari zangu za hapa na pale nikatumbukia wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, moja kati ya mikoa mikubwa Tanzania.
Ki ukweli Don Mangi napenda sana watoto, katika pitapita zangu za hapa na pale nikafika mahali nikaona nipumzike kutokana na jua kali la mchana, palikua na mti mdogo halafu chini yake kuna madereva wa bodaboda wamepaki, kwa pembeni hivi kulikua na watoto wadogo wanacheza nikawa nawaangalia huku nikiwachekea na ku-make faces. Kitoto kimoja katika lile kundi kilipenda ule mchezo, ghafla kikatoka kilipokua na marafiki zake na kuja kunikimbilia, kikaja magotini na kuanza kunivuta miguu huku kikicheka kwa furaha, vile nilikua nimesimama nikakiangalia kichwani kilikua na tetekuwanga kama ndo zinaishia kupona hivi, sikutilia maanani, karibu na pale palikua na kaduka, basi huyoo nikaenda kununua maji ya kunywa katoto kakanifwata nikakanunulia pipi basi kakaondoka na mie nikaendelea na kilichonipeleka kule.
Siku kama mbili zimepita toka niende huko na kurudi,Sasa cha kushangaza,jana usiku nilikamatwa na homa moja kali kweli yani mpaka ikanibidi kuamka. Nikajitahidi mpaka kufika asubuhi, nikahisi nina malaria, nikakamatia dawa zangu za malaria nikaendelea kuzunguka mjini, homa ikawa pale pale, doh! Yani usiku haufai, kitanda kinalowa jasho na huku nasikia baridi.
Sasa leo asubuhi naamka naanza kuona vipele vinanitokea sana sana usoni vinawasha na vinajaa maji. Kichwa kinagonga usipime kama vile watu wamefungua crusher ya kuponda mawe. Kuchukua kioo na kujiangalia fasta. . .Salaale! Tetekuwanga zimetambaa uso mzima hata naogopa kujiangalia.Dah! Akili ikacheza fasta nikamkumbuka yule dogo aliyekua anacheza miguuni pangu.
Bahati nzuri ninapokaa si mbali na duka la dawa(maana hospitali huku ni kitendawili, hiyo foleni nmb mara mbili) ndo nikaenda pale akanishauri ninunue calamine lotion na vidonge ninywe pen v., Kiufupi sijawahi kuugua hii kitu toka nimezaliwa. niko ndani tu kama mzazi vile, hamu ya kula sina, ni kusikia baridi na kuvuta shuka.
Jamani kwa anayejua kama hiyo prescription niliyopewa ni sawa au kama kuna maboresho.
Dah. . .dogo lakini kanitenda.
Thanx,
 
Pole Don, mie niliuugua juzi juzi
Ni noumer, aisee ni noumerer

HAkuna cha calamine lotion wala PNV, it's a viral disease, na mwili huwa unapigana nao wenyewe

Madoa sasa na utu uzima, una kazi aisee

Mie nilipungua kilo za kutosha, nikawa naona watu wananinyanyapaa, wenye kusema hili wenye lile

Pole, jitahidi kula na kunywa zaidi
 
Pole xana, lakini usije ukawachukia watoto kwa sababu ya ugonjwa wa kuambukizwa!!!!!!!!!!!!!!!!! Jitahidi kpata ushauri na utapona tu. Mungu akupe moyo wa uvmlivu
 
Teenx Konnie. . .sema hii siyo kama ndui, makovu yake yanapotea haraka. Ndui ndo yanabaki. Yani hamu ya kula haipo kabisaa, nakunywa maji tu na chai kidoogo.
 
Pole xana, lakini usije ukawachukia watoto kwa sababu ya ugonjwa wa kuambukizwa!!!!!!!!!!!!!!!!! Jitahidi kpata ushauri na utapona tu. Mungu akupe moyo wa uvmlivu

Thenx maby. . .ah. . .siwezi wachukia watoto, I still love em. . .ni alert tu kuna vitu vidogo hua navipuuza vinanicost
 
Mi sijaelewa, kumnunulia mtoto pipi kunaambukiza tetekuwanga? Kwanini nisiamini kuwa ulizipata sehemu nyingine? Labda kwa watoto wakubwa, LOL!
 
Mi sijaelewa, kumnunulia mtoto pipi kunaambukiza tetekuwanga? Kwanini nisiamini kuwa ulizipata sehemu nyingine? Labda kwa watoto wakubwa, LOL!

the contact. . .mind you, alinishika suruali, hata ukikaa tu room moja, it is transmitted by air.
 
endelea kuwapenda sana, na sasa umegundua jinsi watoto wadogo walinavyopata shida na magonjwa mbalimbali ila bado unakutwa wanatabasamu na kucheza, pole sana kaka Mungu akuponye na amponye yule mtoto pia.
 
Hayana dawa,yatapona yenyewe tu,kunywa dawa za kupungunza maumivu na muwasho,niliugua ndani ya wiki mbili nikawa nimepona.DR aliniambia ukiuguwa tetekuwanga siku ukipata HIV ni rahisi sana kupata mkanda wa jeshi
 
Amen and thanx a lot friend!
 
Pole Don, mie niliuugua juzi juzi
Ni noumer, aisee ni noumerer

HAkuna cha calamine lotion wala PNV, it's a viral disease, na mwili huwa unapigana nao wenyewe

Madoa sasa na utu uzima, una kazi aisee

Mie nilipungua kilo za kutosha, nikawa naona watu wananinyanyapaa, wenye kusema hili wenye lile

Pole, jitahidi kula na kunywa zaidi

heheheheheheheee Kongosho sikupatii picha na tetekuwanga........

Sipati picha majirani walikuwa wanagunaje.......
 
Last edited by a moderator:
Chai ya rangi eeh? Mie ndio iliniokoa.

Pole sana, afu kuwashwa sasa, pole kwa kweli

Teenx Konnie. . .sema hii siyo kama ndui, makovu yake yanapotea haraka. Ndui ndo yanabaki. Yani hamu ya kula haipo kabisaa, nakunywa maji tu na chai kidoogo.
 
Pole Bint yangu aliugua mwez uliopita nilimuonea huruma yani uso kama alowekwa vidoti vyeusi kwa wanja,usiku silali homa
vinamuwashaaa nikampaka hiyo calamine cream na baada ya week ndio nikampa cream flani yakutoa hizo alama na kweli hazichelewi kupotea kwa mtoto sijui kwako.........
 
Hayana dawa,yatapona yenyewe tu,kunywa dawa za kupungunza maumivu na muwasho,niliugua ndani ya wiki mbili nikawa nimepona.DR aliniambia ukiuguwa tetekuwanga siku ukipata HIV ni rahisi sana kupata mkanda wa jeshi

Dah, wiki mbili?? Yenyewe hii siku ya tatu sishikiki.
 
He he he he he, nina picha nilipiga za kutosha

Nitakutumia siku moja

Ilikuwa, mmemuona mama havintishi, ndo basi kaisha yule

Wanasingizia tetekuwanga, inaweza kuwa hata mkanda wa polisi

heheheheheheheee Kongosho sikupatii picha na tetekuwanga........

Sipati picha majirani walikuwa wanagunaje.......
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom