My Life, My Purpose by Benjamin W. Mkapa

Ngareroo

JF-Expert Member
Aug 11, 2019
2,049
2,249
Wasalaam Ndugu zangu, I hope mko salama.

Huu uzi sitaandika kwa Ngareroo slangs maana nna jambo la muhimu la ku'share nanyi, hii ni kutokana na watu wengi hasa wale wasio wa Arusha kutoielewa.

Rais wa awamu wa Tatu wa Tanzania Mzee Benjamin William Mkapa katoa kitabu chake kinachozungumzia maisha yake pamoja na Nia yake kiitwacho "My Life My Purpose". Sasa nilikua naomba mliokiwahi kitabu hiki naomba mtufahamishe kama kazungumzia maisha yake kama mwandishi wa habari na baadae uhusiano wake na waandishi wa habari mala baada ya kuwa Rais.

Nakumbuka nilimsikia akihojiwa na Riz Khan wa CNN na Kuulizwa kuhusu msimamo wake wa kutoshirikiana na Media za Tanzania. Alijibu kwamba hajagomea vyombo vyote vya habari na ndio maana alikua anaongea na CNN wakati huo ispokua media za Tanzania alisema zilikua "Too Primitive!".

Kabla ya hapo magazeti yaliyokua yameandika kuhusu ufisadi katika serikali aliyajibu kwa kuyauliza "Kwani nyinyi mitaji ya kuanzisha magazeti mliipata wapi?".

Na at that time private media ndo zilikua zikichanua kwa habari na makala nzitonzito chini ya waandishi mahiri na wabobezi kabisa kuwahi kutokea Tanzania.

Na lengo la uzi huu ni kutaka kujua je, katika hiki kitabu chake ameandika maoni yake kuhusu huo msimamo wake kwa media za Tanzania chini ya waandishi kama Jenerali Ulimwengu, James Mpinga, Wenceslaus Mushi na wengine aliziona "Primitive" anavionaje hivi vya sasa chini ya Uanaharakati Huru kama Musiba?
 

Attachments

  • ah.jpg
    ah.jpg
    15.2 KB · Views: 115
Wabongo bana naona iki kitabu toka kitoke watu wanakishobokea. Asili ya Watanzania tu wavivu wa kusoma, kwakua watu wanakiulizia sana basi na wengine wamefata mkumbo..Huwezi kufanya kitu kisa wengine wanafanya.

Bahati mbaya zaidi hata tukisoma vitu yale tuliyoyasoma tunaishia tu kuyasoma kama unavyosoma Subtitles za kichina..The same applies to Inspirational speeches. Watu wanakua motivated ila kuyaishi waliyoambiwa wanashindwa.Refer waliosoma vitabu vya Poor dad Rich Dad.

And for another Don't Judge me for my views, Napenda kua Different kimtazamo
 
Pambafff kunakili bandiko la mtu bila kum acknowledge...Chapisho hili limeandikwa na James Gayo kupitia ukurasa wake wa FB saa mbili zilizopita ni vyema kuheshimu kazi za watu nanina!
Hata me nmetilia mashaka, kwa mtazamo wangu namwona mtoa uzi ni kijana wa siku hiz tofauti na mambo aloyaandika.
 
Back
Top Bottom