Nikhil
JF-Expert Member
- Apr 16, 2013
- 361
- 120
Wakuu habari zenu!
Nimetupia thread hii kwenu as a 'GREAT THINKERS' mnisaidie kimawazo juu ya huyu Mpenzi wangu".
Mimi ni kijana wa miaka 19 nilikuwa na mpenzi wangu aitwaye Grace kiukweli nilimpenda sana na upendo wangu mi na yeye umeanzia tangia nikiwa kidato cha pili na kusababisha hata perfomamce yangu kimasomo kushuka juu ya upendo wangu kwake.
Tuliendelea na uhusiano wetu huku tukiwa tumejiwekea malengo kuwa one day tutakuja kufunga pingu za Maisha, nilikuwa mstari wa mbele kwa kumsadia kwa kila jambo kwa kipindi tulipo kuwa shuleni hii ikanifanya nijisahau kimasomo cha ajabu performance yake ikawa nzuri japokuwa na yeye alikuwa bize na mimi ' Marafiki zangu walinionya japokuwa sikuwaelewa huku nikiwatia moyo kuwa nitabadilika.
Mwisho wa yote tukafanya mtihani wetu wa kumaliza kidato cha nne " huku tukisubiri matokeo bado tulikuwa tunaendeleza uhusiano wetu kwa njia ya simu kwa kuwa yuko home kwao .
Matokeo yalivyo toka japokuwa yalikuwa si mazuri kwa darasa zima ila yeye alifaulu kwenda A- level ila kwa upande wangu mimi sikufanikiwa ila nilipata daraja la 4 point 26 .
Maskini mimi akajiona yeye ndo yeye nikimpigia simu hapokei ila sivunjiki moyo akipokea anadai niko bizze labda baadae .Baadae nikimtafuta hapatkani Nimechanganyikiwa sijioni kama mwanadamu wa kawaida kwani siku moja kanitumia meseji inasema " Achana na mimi niko bize nasoma sitaki unipotezee muda kwani ninamalengo yagu" jamani imeniuma sana kwa nini amekuwa hivi amenifanya hadi siioni thamani ya maisha yangu ! Wana jf kuna maswali najiuliza ambalo ni Nifanyeje ili kukikomesha hiki kiburi chake na pia hivi Malengo yangu juu yake ndo yayeyuka hivi hivi .
Wakuu nifanye nini juu yake im serious juu ya hili ?