My ebay buying experience... (with images)

My ebay buying experience... (with images)

So sometime back nilipost kwenye jukwaa la "Matangazo Madogo" kuwa nilikua nahitaji kama kuna mtu mwenye miwani za 3D za Anaglyph ( Red & Cyan ) aweze kuniuzia... Lakini kwakwel sio hapa tu bali hata FB sikuweza kupata mtu mwenye nazo, au kama walikuepo basi walipiga kimya...

Kwa miezi ya juzi hapa niliamua kuchek the Product EBAY and zilikuepo nyingi sana zenye bei tofauti... Kwasababu ilikuwa mara yangu ya Kwanza nikaamua kuchagua yenye Bei ndogo ili hata kama haitofika, basi hasara haitokua kubwa kihivyo...

Kuna seller mmoja nikamuona anaitwa "Right2Save" alikua anauza miwani hyo for 1$ making it a total of 1.33$ with shipping, so nikaenda na huyo

Screenshot_133.png


So nikafanya purchase Kwa kutumia my Paypal Account (Linked with my Credit Card)... And the purchase was Confirmed... And wakati nipo kwenye page ile ya checkout, Nilimuandikia Seller a note kama inavyoonekana hapo kwenye picha...


Screenshot_116.png


Kwenye Dashboard yangu ya paypal baada ya kufanya payment wakaniambia kuwa watampa taarifa muuzaji (Right2Save) afanye shipping... So i waited.

NOTE : Hii ilikua Tarehe 24/04/2014 , Thursday.

Kwenye Tarehe 25/04/2014 nikapokea message kutoka kwa Right2Save mzigo umeshatumwa through airmail...


Screenshot_134.png


Basi kilichobaki ikawa nikusubiri nione kama huo mzigo utafika au nimepigwa changa la macho... Recently nimeenda kucheki kwenye sanduku la Posta huu mwezi wa sita ( I was School )... And nilifurahi kuona kuwa ule mzigo ulikua umefika... Kutokana na Mihuri iliyopo kwenye Postage, Mzigo ulitoka China tarehe 27 mwezi wa 4, ukafika Dar Es Salaam tarehe 9 mwezi wa tano, and Tarehe 10 mwezi wa tano ukawa umeshafika Tanga...

IMG_4354.jpg


Kucheki Ndani, My 3D Anaglyph glasses zilikuepo 3 kama ilivyoandikwa Ebay... So all went well.


IMG_4359.jpg


So kwa wale wote ambao walikua na mashaka, Msihofu sana, cha muhimu nikuangalia Positive Feedback ya anayeuza, Right2Save alikua na +ve feedback ya kitu 99.4%...

Sijui kwa ishu za Customs Processing inakuaje kama mzigo wako ukifika, kwahiyo kama kuna member mwenye idea, Anaweza akacomment.

:msela:HAPPY BUYING:msela:

Mkuu me naomba shule kuhusu kulink account na paypal..natumia bank ya CRDB..makato yao yakoje..!? Mfano wewe umebuy kiti cha dola moja na point.. Walikutata ela ngapi bank unayotumia wewe.!?
 
Back
Top Bottom