My Dad's Legacy!

My Dad's Legacy!

Aliniambia niwaheshimu wazazi wangu nakuwapenda kuwajali kwa maana wao ndio wanaupendo wa kweli wengine watakusaliti kukuabisha kukutesa kukuchora unafiki ila wazazi wako hawako hivyo.
Ukiolewa olewa na mtu anayejituma .
Anayependa maendeleo naanakutambua kukuheshimu nakukujali.
Nikakumbuka yesu alikaribia kuzaliwa wazazi ndio walirisk maisha yao ili azaliwe.
Naaliposulubishwa walimuacha wote hadi wanafunzi wake ila alibaki na mama yake .
So unaona hakuna atakayekujua nakukujali kama wazazi pekee.
 
mwanangu nahofia ukiondoka nani ataniosha miguu yangu(nilikua napend san kumuosha miguu baba hasa siku zake za mwisho hapa duniani ukizingatia ni mtot mdogo kuliko wote na alikua haoni sabb ya kisukari na presha) lakini nenda kapambane na maisha Ipo siku utafanikiwa toka hapo sikuwai kuisikia tena sauti yake mbaka leo safari ya maisha yake iliishia tareh 9 mwez 9 2018 pumzik baba yangu umeteseka san umekufa ukiwa umeshikilia rufaa yako ya kwend muhimbili ila sababu ya umaskini umeikumbtia mbak unakufa ach niishie hapa wakuu ila bado nadhalilka haswa kwa matajiri apa mjini ila sikati tamaa
pole sana mkuu mungu amrehemu uko alipo...
 
mungu ailaze roho yake mahali pema pole sana dadaa
''Wewe ni mimi"
Sijawahi kuacha kuhisi yuko pembeni, na nikihisi hayupo ndo moment ninakuwa weak hasa, nikihisi yupo nakuwa JASIRI mara alfu"
24 YRS toka nimekuaga,huwa sijawahi kuhisi umeshafariki!
 
mkuu maneno yako yanasikitisha sana kidogo nilie..sema nimejikaza kikondoo
Nimepitia hoja za wengi katika uzi huu...ikabidi niinamishe tu kichwa changu kwa uchungu baada ya kuona kwamba wanaume tuna maisha mafupi sana hapa duniani.
 
pole sana inaonesha haikuwa rahisi kwako
Hongereni mliopata malezi ya baba wengine tulikuwa kama kama kunguru kwa kukosa baba ila maisha yanasonga
Huwa nataman hata kujua sura yake how waz it but it still in vain
 
Yangu ni stori ndefu kidogo.

Advance nilisoma wilaya tofauti na tuliyokua tunaishi na familia. Baba alikua na kawaida kila nikirudi nyumbani kwa likizo ananipa hela ya ada na matumizi mapema mwanzoni kabisa likizo ikiwa inaanza ili isije ikatokea natakiwa kwenda shule kukawa na shida ya pesa. Kwa mzee, mimi ni kijana mpole, mwenye nidham ya matumizi ya pesa, mwenye busara na mwenye akili na uwezo binafsi wa kujiguide mwenyewe. Bahati mbaya kipindi hicho mimi nilikua kinyume kabisa na alivyonifikiria! Alikua kinipa hiyo hela mi naanza matanuzi, zitanunuliwa brands kali za nguo nlizokua nazitaman zikanipita nikiwa school, nitatafuta mitoko ya hapa na pale na visichana vyangu so mpaka kufika wakat wa kwenda shule mi nakua nimebaki na nauli tuu! Nikifika shule nakaa wiki mbili au tatu namchek kuwa nimepata tatizo fulani nina shida na hela basi anatuma.

Sasa siku moja kama kawaida akawa amenipa hela, round hii alinipa hela ndefu zaidi ya siku zote. Nikafanya kama desturi yangu, nilipofika shule wiki mbili tuu nikamuandikia sms kwamba nilipokua naenda shule nilidondosha wallet so hapa nilipo sina hela. Dakika mbili nyingi mzee akapiga simu, sikupokea..akapiga kama mara tatu hivi nikaacha kupokea mana nilikua sina cha kumwambia. Basi kukaa kidogo nikaona txt ya MPESA imethibitishwa nimepokea kiasi kadhaa...nikaogopa hata kumtumia msj ya kumshukuru, akanitxt "..usiogope mi nimekuelewa, huwa inatokea. Jitahidi usijiingize kwenye mambo yatakayokufanya ushindwe kujiandaa vizuri na mitihan yako ya mwisho. Unasalimiwa". Sijawahi kujisikia hatia kama siku ile, Nilijiona fala sana.

Ikafika likizo ya mwisho kabla ya kuingia kwenye mtihan wa mwisho, ile ya mwezi wa tatu. Kurudi hom nakuta mzee anaumwa vibaya mnoo!! ameisha hatari, wamehangaika hospital zote kubwa hapa mkoani hakuna kilichobadilika, wamempeleka mpaka mjini Dar still hali yake ikawa inazidi kuwa mbaya, Mda ule walikua wameshakata tamaa wamemrudisha nyumban wakisubiri tuu lolote la kutokea litokee. kumbe aliwaambia wasiniambie mana watanipotezea concentration kwenye masomo.

Siku ya pili baada ya mimi kurudi, tulikuwa room kwa mzee. Tulikuwa mimi, mama, mdogo wangu na sister etu mkubwa. Mzee akawaomba watoke anataka kuongea na mimi.

Sijawahi kusahau yale aliyonambia hata mara moja, "..Jigga mwanangu, wewe ndo mimi mdogo. Huyo dada yenu tayar ana kwao kwingine. Nikiondoka mimi huyu mdogo wako anakua mtoto wako. Niliwambia wasikwambie kwa sababu sikutaka upoteze muelekeo kwenye masomo yako. Nina vitu nataka nikwambie,

Kwanza ni kuhusu ile hela, nina uhakika ile wallet hukuangusha ila uliibiwa. Uliibiwa kwa sababu ya uzembe! Hata siku moja usithubutu kutembea na kiasi kikubwa cha pesa, duniani kuna profession nyingi. Wapo walim, madaktari na wengine, pia kuna wezi...hiyo ni kazi yao na wapo makini nayo! Mtu akijua una hela yupo tayari kufanya chochote ili aipate..akishindwa kukuibia yupo radhi hata kukuua ilimradi hicho unachomiliki kiwe chake. Nilimshukuru Mungu walifanikiwa kukuibia kwani wangeshindwa wangefanya chochote kukudhuru ili wapate. (Japo kuwa ukweli ni kwamba sikuibiwa wala kupoteza wallet lakini hii ilinipa funzo kubwa sana, siku hizi huwa natembea na ile hela ambayo tuu nimepanga kuitumia kwa wakati huo na si zaidi). .."

Alinambia vingi mno, akaendelea "..najua saivi unaelekea kwenye mitihan, mimi sina tumaini lolote. Baada ya kuniona katika hali hii, na kujua kuwa akiba kidogo niliyokuwa nayo nimemaliza kwa ajili ya matibabu ambayo nayo yameshindikana, ulishawahi kujiuliza utaendelea vipi na masomo? Ikitokea umefanikiwa kwenda chuo kikuu na bahat mbaya ukose mkopo, utasoma vipi...
Mimi nina akiba ya pesa ambayo hakuna anaejua kuwa ninayo, hata mama yako hajui. Niliiweka ili ije ikusaidie wewe na mdogo wako kwenye masomo kama lolote likitokea, kanuni moja ya pesa ni kwamba hatakiwi mtu yyte kujua kiasi gani unamiliki. Hata mke wako!

Mama yako ni mwanamke mwema, mzuri. Lakini hata yeye tumewahi kukwaruzana mara kadhaa kuhusu pesa, kuna kipindi alikuwa akigundua nina hela mara atataka hiki atataka kile, atahitaji kwenda kusalimia kwao na vitu vingine. Ikitokea nimemkatalia basi anakasirika..hiyo yote ni kwa sababu anauhakika pesa ninayo, hata kama hajui nina matumizi gani nayo! hata kwenye maisha ya kawaida..mtu akijua kuwa pesa unayo lazima mtagombana. Watakuja ndugu wa kuomba uwakopee, watakuja wa kuomba uwasaidie kwa namna fulan. Ukisema huna na wanajua unayo lazima watakuchukia, lakini kama wasingekua wanajua kuwa unayo hata wasingekuchukia!! hizi hela mama yako au mtu mwingine angekua anajua ninazo wewe ungezikuta? unadhan ndugu zangu wangekubal mimi nisitibiwe zaidi akat pesa zipo?.." (Sisemi kwamba maneno exactly ni hayo lakini ujumbe alionipa 100% ni huo, siwez kukumbuka maneno yote).

Baada ya hapo akanipa kadi yake ya bank nikatoe kiasi cha kunitosha kutumia shule mpaka nitakapomaliza. Na kadi nibaki nayo, niliumia mno!! kuanzia hapo nidham yangu ya matumiz ya pesa ilijengeka upya.

Nina mengi, lakin fortunately mzee bado tunae na afya njema kabisa. My dad's my hero
Asante mkuu apa kuna mengi ya kujifunza
 
Baba yangu aliniambia niogope wanawake kama ukoma....!

Mpaka leo nina mika 39, cjaoa.. naogopa wanawake kuliko ukoma😳😳😳
hahaaa mimi baba yangu alishawahi kuniambia kuwa .. MWANANGU NATAKA UFAHAMU KWAMBA WALIMWENGU WANAPOSEMA MWALIMJ WA WANAWAKE NI KIPOFU ".. BASI NAOMBA UTAMBUE KUWA MWALIMU WAO NI UJINGA ... NA NINAPOSEMA HIVI MSEMO HUU UNA MAANISHA HATA MAMA YANGU MIMI AMBAYE WEWE NI BIBI YAKO PIA NA YEYE MWALIMU WAKE NI KIPOFU (ujinga )

Tafadhali Kuwa makini na wanawake ..

mpaka leo huwa najiuliza kwanini dady aliniambia maneno yale kwa sababu sijawahi kuona hata siku moja akikwaruzana na mama "... kubwa zadi aliishi na mama yetu vizuri mnoo na huwa na muhesabu mama yangu ni baadhi ya wanawake wachache wenye UTU wenye kuziheshimu ndoa zao ". katika huu ulimwengu


R.I.P DADY
 
Baba yangu ana roho mbaya sana, sina cha kujifunza mpaka leo nimeishi nae miaka mingi sana ndani ya familia lakini ninachokijua kutoka kwake ni ikatiri, roho mbaya, kutokua na huruma, kutenga baadhi ya watu, dharau n.k. na ninashukuru sijaiga na wala sina chembechembe za tabia yake hata kidogo.
Zaidi ya kitu kimoja tu, alisisitiza na kutupigania tusome sana tu. Na hilo nashukuru limenisadia mpaka nimepiga shule yangu. Nina degree 1, masters 1, nasoma phd, na nina mpango wa kupata masters mbili kuanza kusoma mwakani.
 
Baba yangu ana roho mbaya sana, sina cha kujifunza mpaka leo nimeishi nae miaka mingi sana ndani ya familia lakini ninachokijua kutoka kwake ni ikatiri, roho mbaya, kutokua na huruma, kutenga baadhi ya watu, dharau n.k. na ninashukuru sijaiga na wala sina chembechembe za tabia yake hata kidogo.
Zaidi ya kitu kimoja tu, alisisitiza na kutupigania tusome sana tu. Na hilo nashukuru limenisadia mpaka nimepiga shule yangu. Nina degree 1, masters 1, nasoma phd, na nina mpango wa kupata masters mbili kuanza kusoma mwakani.
Una cha kujifunza, KUWAHIMIZA WANAO WASOME!
Mzazi ni mzazi tu, hata aweje ni lazima kuna jambo la maana utaiga/kujifunza kutoka kwake.
 
Mungu aeendelee kumlinda mshua tu aisee, sikuwahi kudhani kama tuna mitizamo ya kufafana katika mambo mengi kiasi hiki.
 
Legacy wanayoacha wazazi wengi wakiafrica ni maneno peke yake, na sio makampuni au mali zitakazo tumiwa na watoto wa watoto, kampuni kama macdonald, cocacola zilikuwa za mababu zao
 
Baba yangu ana roho mbaya sana, sina cha kujifunza mpaka leo nimeishi nae miaka mingi sana ndani ya familia lakini ninachokijua kutoka kwake ni ikatiri, roho mbaya, kutokua na huruma, kutenga baadhi ya watu, dharau n.k. na ninashukuru sijaiga na wala sina chembechembe za tabia yake hata kidogo.
Zaidi ya kitu kimoja tu, alisisitiza na kutupigania tusome sana tu. Na hilo nashukuru limenisadia mpaka nimepiga shule yangu. Nina degree 1, masters 1, nasoma phd, na nina mpango wa kupata masters mbili kuanza kusoma mwakani.
daaahh pole sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom