My confession

My confession

Mie nililelewa mazingira ya kidini sana
Kwahiyo hawakuwa na hofu kwani hadi naenda chuo nishajua jema na baya na still nilijitunza
Basi tu shetani akiamua kukuwinda atahakikisha anakupata kwenye angle yake
Unamaanisha nini ukisema ulilelewa kwenye mazingira ya kidini na ulishajua jema na baya?

Una maana kwamba ulijua kuwa ukit*mbwa bila kinga utapata mimba ukaamua kupuuzia tu au?
 
Za asubuh wana jukwaa.Mungu ni mwema Kila wakati.

Wakati nasoma chuo,about 10 years ago,nikiwa mwaka wa kwanza.Nikiri i was virgin and still naive.Basi nikakutana na bazazi moja likanishawishi tukaanza mahusiano ya mapenzi.Tulikuwa wote first year sema course tofauti.Nakumbuka ilikuwa second semester,katika mahusiano hayo nikabeba ujauzito.

Nikatafuta wasaa nikamweleza mhusika,akanijibu,we waulize wanawake wenzio huwa wanafanyaje,akaondoka zake.Niliumia Sana,then jioni nikakutana na room mate ambaye yeye alikuwa kanitangulia miaka miwili nikamweleza akanambia umepima nikamjibu nope,ila Nina mwezi nimemiss period.Akanambia nenda kapime kwanza,next day nikaenda dispensary ya chuo nikapima majibu yakawa positive.

Nakumbuka nilirud room nalia Sana,hata lecture za sikuhiyo sikuingia.Niliwaza mengi ikiwemo nitawaambiaje nyumbani.Muda wa lunch akaja room,huyo roommate,akanambia majibu vipi nikampa karatasi ya hospital.Akaniuliza mhusika umemwambia,nikajibu ndiyo.Akaniuliza tena kasemaje,nikamwambia kanambia niulize wanawake wenzangu huwa wanafanyaje na since then hata simu zangu hapokei.Akanambia usihofu kesho ntakupeleka sehemu.Kweli kulipopambazuka akanipeleka maeneo ya makumbusho,kulikuwa na kihospital flan bubu,akaongea na dokta,tukalipa,then nikaandaliwa nikapigwa nusu kaputi.Yaliyoendelea sikumbuki,ila ikawa the end of my precious first baby that day.

Nikakata mahusiano na yule bazazi na sikuwahi date tena hadi nagraduate.Ila nilipata depression kwa kile kitendo,niliteseka semester nzima GPA yangu ilishuka vibaya Sana.

Kila nikikumbuka moyo waniuma,huenda saivi ningekuwa na vidume vyangu vitatu manake saivi ninao wawil.Baby wherever you're am sorry,i was young,naive and stupid.Hiyo ni mistake nilifanya nikiwa undergraduate lakini hadi leo yanitafuna consious yangu.
pole sana mmi nilipokuwa undergraduate nilikutana na katoto kapo form two kazuri nilikatia mimba zisizopungua tisa sasa kameolewa na jamaa namwonea huruma mana yule sio wa kuoa
 
Ni kweli usemalo mkuu. Katika kuchagua twawasihi dada zetu wawe makini. Wasitizame sifa za mtu za kidunia,
Watizame mwanaume wake kweli ana hekima na upendo kwa binadamu wote.

Wasichana mimi niwaambie kitu, ukiona bwana wako mwepesi kugombana na fulani na ni mwepesi kutukana kwa hasira, jua ipo siku ukiishiwa thamani atakufanyia hayo na wew.

So, fikirini moyo wa mtu zaidi kuliko muonekano wake kabla ya kumpenda awe mpenzi.
Pole sana dada huyo mtoto amesikia kitubio chako na hatokuzuia kupita kwenye mlango wa paradiso

Na wanaume wa namna hiyo wako wachache sana ila huaribu wanawake wengi kwa maana wanaume wapole hawapendwi na wanawake wengi

RIP bazazi popote ulipo
 
Inawezekana mzazi au mlezi wako hakuwahi kukaa na wewe akakupa elimu kwa kina juu ya tahadhari za kuzingatia hasa unapokuwa umevunja ungo, hili jambo wazazi / walezi wengi tunafeli sana.
Mtoto /watoto wanapokua ni vema kukaa nao na kuwaelimisha kwa kina sana juu ya mabadiliko ya ukuaji wa miili yao na utendaji wa viungo vyao vya uzazi.
Unakuta mzazi / mlezi unaogopeka kwa watoto kiasi ambacho hawawezi hata kuelezea shida zao. Mathalani mtoto wa kike anapovunja ungo anafikia hatua ya kujificha na kuficha hali hiyo kwa hisia kwamba ataonekana hafai ( kuvunja ungo / kubalehe ) sio dhambi ni jambo la kawaida kwa binadamu.
Mzazi anafanya kukisia kisia tu kwamba bintiye au kijana wake kakomaa, matokeo yake anabaki tu kumwelezea maneno ya vitisho kama vile; ukikutana na mwanaume utapata mimba (how??????.....mfafanulie mtoto aelewe kila kitu kwa uwazi) au ukitembea na mwanaume wazazi wako wanakufa (really!!!!!...... seriously!!!!!!!......)
Wazazi na walezi tuseme na watoto, ikishindikana tutumie hata marafiki zetu tunaowaamini.

Upo sahihi
 
pole sana mmi nilipokuwa undergraduate nilikutana na katoto kapo form two kazuri nilikatia mimba zisizopungua tisa sasa kameolewa na jamaa namwonea huruma mana yule sio wa kuoa
Utubu na wewe kwani nawe hiyo dhambi itakutafuna one day.
 
Mauaji kama haya wamefanya watu wengi sana.

Na inawaumiza sana haswa ikitokea anashindwa kupata mtoto wa pili au hapati kabisa
 
Niliwahi kutana naye kwenye semina Arusha likataka leta mazoea,nikamwambia kama unataka nikudhalilishe jaribu hata kunisogelea,akaondoka akaenda ungana na wengine.
huna haja ya kuwa na hasira nae.....inawezekana ndio maana inakutesa...futa delete....songa mbele...hata yeye anajuta huko aliko....hajajua were to confess.......na je mbele za Mungu ulilisogeza na kulifuta huko......???
 
Yes wakati natafuta mwanangu wa kwanza nilitubu,manake ilinichukua miaka Kama mitatu nikawa siconcive,ila Mungu alisikia kilio changu akanijalia kijana wangu wa kwanza baada ya toba hiyo.
 
Hongera mpendwa..kukosea sio kitu kibaya cha kukufanya ujihukumu..
Bila kufanya makosa tungejifunza vipi?
Bila funzo ulopata ungekuja kuwafunza na kuwashauri nini wanao au hata vijana wengine?
Hakuna dhambi iliyosalia msalabani..Mungu amekusamehe kuwa na amani!
 
Za asubuh wana jukwaa.Mungu ni mwema Kila wakati.

Wakati nasoma chuo,about 10 years ago,nikiwa mwaka wa kwanza.Nikiri i was virgin and still naive.Basi nikakutana na bazazi moja likanishawishi tukaanza mahusiano ya mapenzi.Tulikuwa wote first year sema course tofauti.Nakumbuka ilikuwa second semester,katika mahusiano hayo nikabeba ujauzito.

Nikatafuta wasaa nikamweleza mhusika,akanijibu,we waulize wanawake wenzio huwa wanafanyaje,akaondoka zake.Niliumia Sana,then jioni nikakutana na room mate ambaye yeye alikuwa kanitangulia miaka miwili nikamweleza akanambia umepima nikamjibu nope,ila Nina mwezi nimemiss period.Akanambia nenda kapime kwanza,next day nikaenda dispensary ya chuo nikapima majibu yakawa positive.

Nakumbuka nilirud room nalia Sana,hata lecture za sikuhiyo sikuingia.Niliwaza mengi ikiwemo nitawaambiaje nyumbani.Muda wa lunch akaja room,huyo roommate,akanambia majibu vipi nikampa karatasi ya hospital.Akaniuliza mhusika umemwambia,nikajibu ndiyo.Akaniuliza tena kasemaje,nikamwambia kanambia niulize wanawake wenzangu huwa wanafanyaje na since then hata simu zangu hapokei.Akanambia usihofu kesho ntakupeleka sehemu.Kweli kulipopambazuka akanipeleka maeneo ya makumbusho,kulikuwa na kihospital flan bubu,akaongea na dokta,tukalipa,then nikaandaliwa nikapigwa nusu kaputi.Yaliyoendelea sikumbuki,ila ikawa the end of my precious first baby that day.

Nikakata mahusiano na yule bazazi na sikuwahi date tena hadi nagraduate.Ila nilipata depression kwa kile kitendo,niliteseka semester nzima GPA yangu ilishuka vibaya Sana.

Kila nikikumbuka moyo waniuma,huenda saivi ningekuwa na vidume vyangu vitatu manake saivi ninao wawil.Baby wherever you're am sorry,i was young,naive and stupid.Hiyo ni mistake nilifanya nikiwa undergraduate lakini hadi leo yanitafuna consious yangu.

Pole kwa yote.
Halafu umepotea sana.
 
Jirani yangu kijana wake alifaulu kwenda form V ya bweni na ni ya wavulana watupu. Ni moja ya shule za vipaji inasifika sana.

Headmaster na familia yake wanaishi ndani ya shule. Headmaster ana binti mrembo anasoma form IV day.

Huyu mtoto wa jirani yangu sijui alimuimbisha nini yule binti, binti akawa anamuingiza chumbani kwake usiku. Siku moja saa kumi na moja asubuhi anakutana na headmaster kwenye corridor.

Kesi ilifika nyumbani, wazazi waliitwa. Yule headmaster alivyokuwa mkali hakutegemea kitendo kile kifanyike chini ya pua yake.
Bibi kwa hutu tuvisa na mikasa haujambo,
Haya na wewe leo hebu tukomfisie basi hata zambi moja uliyofanya katika kipindi chako cha uchakaramu.
 
I lost my niece kwa huo upumbavu wa kutoa mimba. A grown up girl decides to abort lakini hata hajui athari za utoaji mimba, angefuata basi njia sahihi akawaona madaktari apewe prescription zinazoeleweka.

Upumbavu wa hali ya juu, ila wahamasishaji wakiwa vijana wa kiume, unamtia mtoto wa watu mimba wakati huna hata uwezo wa kununua kijiko..
 
Yes wakati natafuta mwanangu wa kwanza nilitubu,manake ilinichukua miaka Kama mitatu nikawa siconcive,ila Mungu alisikia kilio changu akanijalia kijana wangu wa kwanza baada ya toba hiyo.
pia msamehe yule jamaa,,, mfute kabisa kama hujawahi (hamjawahi kuzini) muone like young bolibo broken by insects, so u need kupulizia dawa angalau likaliwe sokoni.....pole sana.....wengi mnapitia huko na wangine ni michezo yao.....
 
Back
Top Bottom