My confession

My confession

The iron batterfly

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Posts
1,952
Reaction score
2,527
Za asubuh wana jukwaa.Mungu ni mwema Kila wakati.

Wakati nasoma chuo,about 10 years ago,nikiwa mwaka wa kwanza.Nikiri i was virgin and still naive.Basi nikakutana na bazazi moja likanishawishi tukaanza mahusiano ya mapenzi.Tulikuwa wote first year sema course tofauti.Nakumbuka ilikuwa second semester,katika mahusiano hayo nikabeba ujauzito.

Nikatafuta wasaa nikamweleza mhusika,akanijibu,we waulize wanawake wenzio huwa wanafanyaje,akaondoka zake.Niliumia Sana,then jioni nikakutana na room mate ambaye yeye alikuwa kanitangulia miaka miwili nikamweleza akanambia umepima nikamjibu nope,ila Nina mwezi nimemiss period.Akanambia nenda kapime kwanza,next day nikaenda dispensary ya chuo nikapima majibu yakawa positive.

Nakumbuka nilirud room nalia Sana,hata lecture za sikuhiyo sikuingia.Niliwaza mengi ikiwemo nitawaambiaje nyumbani.Muda wa lunch akaja room,huyo roommate,akanambia majibu vipi nikampa karatasi ya hospital.Akaniuliza mhusika umemwambia,nikajibu ndiyo.Akaniuliza tena kasemaje,nikamwambia kanambia niulize wanawake wenzangu huwa wanafanyaje na since then hata simu zangu hapokei.Akanambia usihofu kesho ntakupeleka sehemu.Kweli kulipopambazuka akanipeleka maeneo ya makumbusho,kulikuwa na kihospital flan bubu,akaongea na dokta,tukalipa,then nikaandaliwa nikapigwa nusu kaputi.Yaliyoendelea sikumbuki,ila ikawa the end of my precious first baby that day.

Nikakata mahusiano na yule bazazi na sikuwahi date tena hadi nagraduate.Ila nilipata depression kwa kile kitendo,niliteseka semester nzima GPA yangu ilishuka vibaya Sana.

Kila nikikumbuka moyo waniuma,huenda saivi ningekuwa na vidume vyangu vitatu manake saivi ninao wawil.Baby wherever you're am sorry,i was young,naive and stupid.Hiyo ni mistake nilifanya nikiwa undergraduate lakini hadi leo yanitafuna consious yangu.
 
Pole sana dada huyo mtoto amesikia kitubio chako na hatokuzuia kupita kwenye mlango wa paradiso

Na wanaume wa namna hiyo wako wachache sana ila huaribu wanawake wengi kwa maana wanaume wapole hawapendwi na wanawake wengi

RIP bazazi popote ulipo
 
Cousin wangu tumeishi naye nyumbani... siku za siku akampa mimba mtoto wa mzee mkali mimba akiwa shule.

Akaenda kutafuta dawa akapewa...akapewa hakuna ajuaye zinavyotumika. Alimchukua msichana akamwingiiza hii guest iliyopo Shivas upande wa kushoto. Akamnyesha bhana....

Katoto kakaanza kupiga kelele tumbo linataka kupasuka limekuwa la moto saana. Akakimbia akamwacha akajua anafariki... nakutana naye anahema nikamwambia twende...

Kufika msichana anavunja jasho alimfungia chumbani kuna joto hajampa hata chakula kipindi cha kummezesha dawa..inshort ilibaki kidogo afariki... alikaa hapo siku tatu... sijui waliimalizaje kesi na baba yake ila alikaa central masaa 12.

Kademu nako hakakumwaachaa kakazidi kumpenda.
 
Inawezekana mzazi au mlezi wako hakuwahi kukaa na wewe akakupa elimu kwa kina juu ya tahadhari za kuzingatia hasa unapokuwa umevunja ungo, hili jambo wazazi / walezi wengi tunafeli sana.

Mtoto /watoto wanapokua ni vema kukaa nao na kuwaelimisha kwa kina sana juu ya mabadiliko ya ukuaji wa miili yao na utendaji wa viungo vyao vya uzazi.

Unakuta mzazi / mlezi unaogopeka kwa watoto kiasi ambacho hawawezi hata kuelezea shida zao. Mathalani mtoto wa kike anapovunja ungo anafikia hatua ya kujificha na kuficha hali hiyo kwa hisia kwamba ataonekana hafai ( kuvunja ungo / kubalehe ) sio dhambi ni jambo la kawaida kwa binadamu.

Mzazi anafanya kukisia kisia tu kwamba bintiye au kijana wake kakomaa, matokeo yake anabaki tu kumwelezea maneno ya vitisho kama vile; ukikutana na mwanaume utapata mimba (how??????.....mfafanulie mtoto aelewe kila kitu kwa uwazi) au ukitembea na mwanaume wazazi wako wanakufa (really!!!!!...... seriously!!!!!!!......)

Wazazi na walezi tuseme na watoto, ikishindikana tutumie hata marafiki zetu tunaowaamini.
 
Jirani yangu kijana wake alifaulu kwenda form V ya bweni na ni ya wavulana watupu. Ni moja ya shule za vipaji inasifika sana.

Headmaster na familia yake wanaishi ndani ya shule. Headmaster ana binti mrembo anasoma form IV day.

Huyu mtoto wa jirani yangu sijui alimuimbisha nini yule binti, binti akawa anamuingiza chumbani kwake usiku. Siku moja saa kumi na moja asubuhi anakutana na headmaster kwenye corridor.

Kesi ilifika nyumbani, wazazi waliitwa. Yule headmaster alivyokuwa mkali hakutegemea kitendo kile kifanyike chini ya pua yake.
 
Ujana maji ya moto, kwenda kulala ndani ya nyumba ya headmaster wake tena kumlala bintiye sio kazi rahisi! Kichwa cha chini kikishika hatamu ni hatari sana hiyo.

Japo kuna walimu/ wakufunzi wanawake huwahadaa wanafunzi wavulana pia. Speaking from experience
 
Jirani yangu kijana wake alifaulu kwenda form V ya bweni na ni ya wavulana watupu. Ni moja ya shule za vipaji inasifika sana.

Headmaster na familia yake wanaishi ndani ya shule. Headmaster ana binti mrembo anasoma form IV day.

Huyu mtoto wa jirani yangu sijui alimuimbisha nini yule binti, binti akawa anamuingiza chumbani kwake usiku. Siku moja saa kumi na moja asubuhi anakutana na headmaster kwenye corridor.

Kesi ilifika nyumbani, wazazi waliitwa. Yule headmaster alivyokuwa mkali hakutegemea kitendo kile kifanyike chini ya pua yake.
Huyu utakuwa ni ww tu huyu, baba yako alikusamehe kwa kumuingiza kiduke chumbani kwakoo au alikuadhibu? Malizia story
 
Ungewashauri na wadogo zako basi wafanyeje ikitokea wamezipa nafasi naivete, stupidity na youthfulness nafasi nao wakatiwa mimba kizembe na wanaume wasiojielewa.

Je wafanye kama wewe ulivyofanya alafu baadae walete confessions?
 
No ikitokea wazae tu,kutoa mimba ni experience mbaya sana
Nina 10 years hili jambo linaumiza moyo
 
Inawezekana mzazi au mlezi wako hakuwahi kukaa na wewe akakupa elimu kwa kina juu ya tahadhari za kuzingatia hasa unapokuwa umevunja ungo, hili jambo wazazi / walezi wengi tunafeli sana.

Mtoto /watoto wanapokua ni vema kukaa nao na kuwaelimisha kwa kina sana juu ya mabadiliko ya ukuaji wa miili yao na utendaji wa viungo vyao vya uzazi.

Unakuta mzazi / mlezi unaogopeka kwa watoto kiasi ambacho hawawezi hata kuelezea shida zao. Mathalani mtoto wa kike anapovunja ungo anafikia hatua ya kujificha na kuficha hali hiyo kwa hisia kwamba ataonekana hafai ( kuvunja ungo / kubalehe ) sio dhambi ni jambo la kawaida kwa binadamu.

Mzazi anafanya kukisia kisia tu kwamba bintiye au kijana wake kakomaa, matokeo yake anabaki tu kumwelezea maneno ya vitisho kama vile; ukikutana na mwanaume utapata mimba (how??????.....mfafanulie mtoto aelewe kila kitu kwa uwazi) au ukitembea na mwanaume wazazi wako wanakufa (really!!!!!...... seriously!!!!!!!......)

Wazazi na walezi tuseme na watoto, ikishindikana tutumie hata marafiki zetu tunaowaamini.
Mie nililelewa mazingira ya kidini sana
Kwahiyo hawakuwa na hofu kwani hadi naenda chuo nishajua jema na baya na still nilijitunza
Basi tu shetani akiamua kukuwinda atahakikisha anakupata kwenye angle yake
 
Pole sana dada huyo mtoto amesikia kitubio chako na hatokuzuia kupita kwenye mlango wa paradiso

Na wanaume wa namna hiyo wako wachache sana ila huaribu wanawake wengi kwa maana wanaume wapole hawapendwi na wanawake wengi

RIP bazazi popote ulipo
Niliwahi kutana naye kwenye semina Arusha likataka leta mazoea,nikamwambia kama unataka nikudhalilishe jaribu hata kunisogelea,akaondoka akaenda ungana na wengine.
 
Back
Top Bottom