My Confession - Nimepima UKIMWI

My Confession - Nimepima UKIMWI

Joined
Jan 20, 2013
Posts
53
Reaction score
34
Wadau,

Kwa kuanza tu niseme nimefanya mapenzi yasiyo salama na wanawake wengi sana na mnamo mwaka 2006 nilikutana na mmoja wa ma-ex wangu ambaye tulikuwa hatujaonana kwa kadri ya mwaka mmoja hivi...huyu ex alikuwa mwenye hali mbaya kiafya akiwa na dalili zote za ''Gonjwa hili''.Nilipata wakati mgumu sana kimawazo kwani nilijua kuwa nimeshaambukizwa ukizingatia kwamba tulikuwa tunakulana peku peku halafu sana tu.

Hali hiyo ilinifanya kukata tamaa na tangu hapo nilikuwa mvivu sana wa kutumia Condom na nilikuwa na hofu kubwa ya kwenda kupima hivyo zaidi ya aslimia 80 ya wanawake niliokutana nao baada kipindi hicho nilikwenda peku peku huku nikisubiri siku yangu ifike.Nilikuwa mtu nayechukia sana stori zozote zinazohusiana na UKIMWI kwa hio nilishajihisi ni mmoja wa waathirika...nakumbuka nilikosa ajira moja kisa tu niliambiwa moja ya masharti ni kupima UKIMWI.Hili suala lilinifanya hata nisifikirie kuingia katika maisha ya ndoa licha ya kuwa na umri mkubwa tu sasa.

Hivi karibuni nilimpata mwanamke ambaye nastahili kumwita mwanamke wa shoka hasa...huyu tumekuwa marafiki kwa kadri miezi sita na muda wote huu amekuwa akiniambia ananipenda pia ila papuchi akawa mgumu sana kuitoa kwa masharti ya kwamba yeye si mpenzi wa Condom na kama ninahitaji papuchi basi twende hospitali tukapime ndipo anipe mzigo.Kwa masharti hayo nilikuwa tayari kumwacha aende zake hasa nikizingatia historia yangu isiyopendeza.Nilianza kumkwepa kukutana naye na mara nyingi alikuwa akinipigia simu na kuniita mtoto wa kiume coz kaniambia tupime mi nikakimbia.Nakumbuka siku moja nilivaa ujasiri tukaenda mpaka TMJ hospital tukiwa naye akaomba kuwa tupime then tupewe majibu tukiwa pamoja...nilitoka nje kama naenda kupokea simu nikatimka mbaya then nikampigia kuwa kuna dharura nyumbani.

Baada ya hapo akawa mchokozi sana na kuanza kuniambia kila asubuhi kuwa vipi umeshatumia dozi tayari akimaanisha ARV na hapo nilikosa raha sana ukizingatia na historia yangu.Leo nimeamua kupiga moyo konde nikaenda mwenyewe Agha Khan nikajisalimisha na kuamua kama noma na iwe noma...na nikaomba nipimwe kwa Elisa kabisa.Nilienda kwa mshauri kwa ajili ya counselling na hata sikumbuki alikuwa anaongea vitu gani kwani akili yangu haikuwa hapo kabisaa.Niliambiwa nisubiri kwa nusu saa baada ya kutoka maabara ambayo kwangu ilikuwa ni kama mwaka mzima hasa nikiangalia viruka njia niliopita nao peku peku...dah kufikia mida ya saa saba hivi nikaitwa na daktari na baada ya kuingia sikumwona kama ni mtu mchangamfu sana kitu kilicho nifanya nijue nimeshaharibu.

Daktari akaniambia kuwa damu yako iko negative....nimeruka humo ofisini kwake kama mwenda wazimu vile nikatoka mbio kwenda AAR kupima tena kama vipimo viko vile vile nikapewa jibu hilo hilo yaani hapa naandika bado natoa machozi maana siamini kilichotokea.Niko na huyu mtu hapa Sanitas tunaenda kupima niko na full confidence nikikuta tu hana leo hii hii namla.
 
wakati tunaogopa huo ugonjwa tusisahau kuna magonjwa mengine ya hatari nayo. dk Riwa njo huku.
 
Last edited by a moderator:
hapo unafurahia!! lkn ucje ukasahau yaliyokukuta

penda penda uachee japokuwa binadamu

sio wakamilifu
 
Pole kwa kuish kwa waswas na hongera kwa kupata majibu mazuri

Anza maisha upya na umshukuru sana Mungu
 
Dah mimi ntapata wapi huo ujasiri?? Miaka yenyewe 24 tu lakini sijiamini. Ex wangu ambaye nilipga kapa amepima yupo poa na alinambia kama angekuwa ameukwaa ningemtambua!! Bado sina ujasiri ngoja nisubiri.
 
Unaweza kulala na bundi ukamka mwenye bahati, ila usijaribu tena kumtembeza kamanda bila gwanda kwenye pori la pamba, utakuje ulie bahati hiyo huwa haijirudii..all and all big up nazani maisha unayona mtamu kweli..
 
Ingekuwa positive ungekuja kutusimulia? Just thinking aloud.
Go n sin no more, rehema ya Mungu imekuponya!
amen .. ujue kweli hata mimi nilipotoka angaza kama nilizaliwa upya ! ukimwi unatisha jamani..ila mungu ni mwema mnooo! nampenda sana yesu kusema kweli kweli msalabani alituponya na mengi
 
Kuna ile Blood group gani sijui, kitaalamu inasemekana kuwa ngumu sana kwa wao kupata Ukimwi. Ndugu labda upo group hilo, ongera.
 
Hata kama huna ngoma kufa kupo pale pale,Sema leo umeipania hiyo nyapuu itakutoa udenda
 
Dah mimi ntapata wapi huo ujasiri?? Miaka yenyewe 24 tu lakini sijiamini. Ex wangu ambaye nilipga kapa amepima yupo poa na alinambia kama angekuwa ameukwaa ningemtambua!! Bado sina ujasiri ngoja nisubiri.

Hujakosea mkuu kupima ngoma kipaji,mwenyewe kama wewe tu najipimiaga kwa niiowagegeda wotee negative basi najiona kidumee
 
Kuna ile Blood group gani sijui, kitaalamu inasemekana kuwa ngumu sana kwa wao kupata Ukimwi. Ndugu labda upo group hilo, ongera.

huku uswazi tunawaita makeria.
Hivi jamani si tunaambiwa kupima urudi baada ya miezi 3 tena wanakuandikia kabisa nyuma ya kikadi tarehe ya kurudi.
Huyu mwenzetu vipi haelewi hilo?
 
Aaaaa kweli elimu ya ukimwi ni ngumu
 
Mungu ni mwema, hata hivyo wapigaji sana unakuta hawana halafu wasiopiga siku anaonja mambo yanaharibika same day.hata hivyo kupima ni muhimu mara kwa mara siku hizi mwanamke anayejitambua hupigi bila kupima.
 
Wadau,

Kwa kuanza tu niseme nimefanya mapenzi yasiyo salama na wanawake wengi sana na mnamo mwaka 2006 nilikutana na mmoja wa ma-ex wangu ambaye tulikuwa hatujaonana kwa kadri ya mwaka mmoja hivi...huyu ex alikuwa mwenye hali mbaya kiafya akiwa na dalili zote za ''Gonjwa hili''.Nilipata wakati mgumu sana kimawazo kwani nilijua kuwa nimeshaambukizwa ukizingatia kwamba tulikuwa tunakulana peku peku halafu sana tu.

Hali hiyo ilinifanya kukata tamaa na tangu hapo nilikuwa mvivu sana wa kutumia Condom na nilikuwa na hofu kubwa ya kwenda kupima hivyo zaidi ya aslimia 80 ya wanawake niliokutana nao baada kipindi hicho nilikwenda peku peku huku nikisubiri siku yangu ifike.Nilikuwa mtu nayechukia sana stori zozote zinazohusiana na UKIMWI kwa hio nilishajihisi ni mmoja wa waathirika...nakumbuka nilikosa ajira moja kisa tu niliambiwa moja ya masharti ni kupima UKIMWI.Hili suala lilinifanya hata nisifikirie kuingia katika maisha ya ndoa licha ya kuwa na umri mkubwa tu sasa.

Hivi karibuni nilimpata mwanamke ambaye nastahili kumwita mwanamke wa shoka hasa...huyu tumekuwa marafiki kwa kadri miezi sita na muda wote huu amekuwa akiniambia ananipenda pia ila papuchi akawa mgumu sana kuitoa kwa masharti ya kwamba yeye si mpenzi wa Condom na kama ninahitaji papuchi basi twende hospitali tukapime ndipo anipe mzigo.Kwa masharti hayo nilikuwa tayari kumwacha aende zake hasa nikizingatia historia yangu isiyopendeza.Nilianza kumkwepa kukutana naye na mara nyingi alikuwa akinipigia simu na kuniita mtoto wa kiume coz kaniambia tupime mi nikakimbia.Nakumbuka siku moja nilivaa ujasiri tukaenda mpaka TMJ hospital tukiwa naye akaomba kuwa tupime then tupewe majibu tukiwa pamoja...nilitoka nje kama naenda kupokea simu nikatimka mbaya then nikampigia kuwa kuna dharura nyumbani.

Baada ya hapo akawa mchokozi sana na kuanza kuniambia kila asubuhi kuwa vipi umeshatumia dozi tayari akimaanisha ARV na hapo nilikosa raha sana ukizingatia na historia yangu.Leo nimeamua kupiga moyo konde nikaenda mwenyewe Agha Khan nikajisalimisha na kuamua kama noma na iwe noma...na nikaomba nipimwe kwa Elisa kabisa.Nilienda kwa mshauri kwa ajili ya counselling na hata sikumbuki alikuwa anaongea vitu gani kwani akili yangu haikuwa hapo kabisaa.Niliambiwa nisubiri kwa nusu saa baada ya kutoka maabara ambayo kwangu ilikuwa ni kama mwaka mzima hasa nikiangalia viruka njia niliopita nao peku peku...dah kufikia mida ya saa saba hivi nikaitwa na daktari na baada ya kuingia sikumwona kama ni mtu mchangamfu sana kitu kilicho nifanya nijue nimeshaharibu.

Daktari akaniambia kuwa damu yako iko negative....nimeruka humo ofisini kwake kama mwenda wazimu vile nikatoka mbio kwenda AAR kupima tena kama vipimo viko vile vile nikapewa jibu hilo hilo yaani hapa naandika bado natoa machozi maana siamini kilichotokea.Niko na huyu mtu hapa Sanitas tunaenda kupima niko na full confidence nikikuta tu hana leo hii hii namla.

Aisee hongera mkuu! mimi yalinikuta maana kila nilipokuwa nakatiza mtaa nilikuwa nakuta story za kutisha za mdada niliye mla kavu! baada ya miezi kama saba ilinibidi niamke asubuhi hata chai sikunywa huwezi amini nilitembea kwa mguu na usafiri ni nao hadi Maria Stopas nikapima! majibu yakaja NEGATIVE! nikarudia kupima mara nne! aisee papuchi nazila kwa akili sana sasa hivi!
 
Back
Top Bottom