My Best friend ameoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

My Best friend ameoa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Gaga, Feb 1, 2011.

 1. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Mimi nina best frend wangu sanasana ni mwanaume na mimi ni mwanamke. ni rafiki yangu wa siku nyingi kiasi kwamba ndugu zangu wote wanamjua na mume wangu anamjua na wanapatana sana sometime tunatoka wote out sometimes tunafanya nyama choma kwake au kwangu tunaita rafiki zetu wengine tunakunywa pombe na kufurahi pamoja.

  Kwa urafiki huo utakuta kila anachofanya lazima ataniambia, akiwa na mwanamke mpya ataniambia akiwa anataka kununua kiwanja tutaenda wote nimpe ushauri akitaka kubadili gari lazima atanishirikisha hata picha atanitumia nione ili nimshauri kama ni zuri au baya. Ikiwa bday yangu ni yeye atakumbuka na kuniletea zawadi hata kama mume amesahau, na sikukuu zingine pia, akisafiri lazima aje na zawadi yangu pia.

  Kwa urafiki wetu ulivyo hata nikipata tatizo labda usiku nimeharibikiwa na gari nitampigia yeye simu aje kunisaidia, nikiwa na matatizo na mume wangu yanayosumulika huwa namwambia anipe ushauri, hata kuna kipindi tuko safarini mtoto aliumwa ni yeye tulimuomba ampeleke hospital. naeleza yote haya ili muelewe ni rafiki wa aina gani ili iwe rahisi kunishauri badae.

  Rafiki yangu huyu ni playboy fulani hivi anapenda sana wanawake ,kila mara ana dem mpya nimempigia kelele sana mpaka mwaka juzi nikamuunganisha na msichana mmoja hivi,alikuwa nje kimasomo ni ndugu wa rafiki yangu mwingine, badae mwaka jana wakafunga ndoa. yule dem alikuwa ananipenda sana wakigombana nitawasuluhisha na mambo mengine.

  Tatizo lililojitokeza sasa hivi mwanamke ananichukia sana nahisi ni sababu rafiki yangu ananijali sana kiasi hata mimi mwenyewe ningekuwa mke wa rafiki yangu ningesikia kawivu flani hivi. Sasa rafiki yangu kanambia wanagombana sana na mkewe kuhusu mimi kwa nini nilimtafutia mke ambae haelewi uhusiano wetu?Kanambia anampenda sana mkewe ila pia ana value urafiki wetu cause tupo kama ndugu.

  Pia Kanambia nimwite nimueleweshe sasa mnafikiri nikimwita atanielewa? na nikimwita nimwambie nini? ni vizuri nimwite nikiwa na mume wangu? Mimi nimemwambia rafiki ndoa yake ni muhimu zaidi kuliko mimi rafiki tuwe tunaonana kwenye mambo ya muhimu kama sherehe msiba na kadhalika mnafikiri huu ushauri ni mzuri? Naomba ushauri wanajamvi am about to loose my very best friend
  naomba kuwakilisha
   
 2. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Habari yako Gaga,unaendeleaje kwanza na ile ishu iliyopita????

  Nafikiri kulipaswa kuwe na mipaka kati yako na huyo kaka baada ya yeye kuoa.....yes nyie ni ma-best friend lakini,wote tuna wivu na tuwapendao na hatupendi ku-share attention na wanawake wenzetu kwa mwanaume tunayempenda,kumtunza na kumjali sana......

  Usiwe kikwazo cha ndoa ya watu kwa ku-value sana u-best friend wenu,have some boundaries,it takes two kuwa katika strong bond kama uliyo nayo wewe na huyo kaka,nakushauri keep a distance,waache wawe na sababu nyingine ya kutofautiana na sio wewe.....kama ni rafiki wa kweli huyo kaka ataheshimu mawazo yako kwakuwa una roho safi na unawatakia mema......

  Muite huyo msichana uzungumze nae na si vibaya mumewe na muwe wako wakawepo mkaweka mambo wazi na si kwa staili ya kusutana just kueleweshana......all the best!!:coffee:
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Lady Gaga itabidi upunguze urafiki wako na huyo rafiki yako ili unusuru ndoa ya mwenzio
  Kwa vile wewe una kwako na mmeo na maisha yako endelea na family yako
  Urafiki wenu uwe wa kawaida kabisa ,vizawadi na mazoea mangine ya karibu punguzeni,
  Katika hali ya kawaida yule mwanamke mwingine anashindwa kuamini labda mko karibu saaaaaaaaaaaaana
   
 4. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Hahahahahaahh! ile issue iko vilevile mwali! ila nasali sana siku hizi, namwona kawa mpoleeee ila mambo yaleyale
   
 5. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  unaweza umuache best friend wako,na bado wakashindwana wakatemana baadae....
  mie nahisi cha kufanya,uwe best friend wa wote wawili,kama ni zawadi ukinunua nunua za wote wawili,ukiwaalika waje wote wawili,mwambie na best yako awe anafanya hivyo,akinunua zawadi ahakikishe na ya mkewe ipo,pia mkialikikana kny sherehe au misiba shirikishaneni wote,muhakikishe huyo dada hafeel isolated,lastly mwambie huyo best friend wako arelax a-let nature takes its course kama kuachana aachane salama...la kuvunda halina ubani...labda hio ndio njia pekee itakayowafanya wawe na furaha!!!:coffee:
   
 6. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Jaribu to keep a distance kidogo isiwe kama zamani na kuanzia sasa unless its really necessary mkutane mkiwa wanne.., wewe, boyfriend wako, yeye na boyfriend wake.

  You dont want to be the cause of your best friends separation...., as I can see wivu is not good for relationship and if they carry on this way their marriage might break... and you dont want to be in the middle of this drama
   
 7. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  kilichobaki urafiki nadhani sasa uhamie zaidi kwa mwanamke mwenzio,kama wanaume wenu pia wana common interest pia watakuwa marafiki vinginevyo itabidi muwavute.
  Vinginevyo ndoa itakuwa ya mashaka na kwa baadae hata mumeo ataanza kutilia mashaka ubest wenu
   
 8. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  sawa mami,subira kidogo akishaanza kuwa mpole ndo anaanza kujielewa.....yote yatakuwa sawa,nina imani.....keep praying and keep up the faith!!
   
 9. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  urafiki wa mwanamke na mwanaume wa kihivyo?, mbona balaaa, ina maana na wewe ulikuwa kama mwanaume ama, maana kama alikuwa anakupa story zake za kungoa mizigo na wewe ukawa unachangia, mhh
   
 10. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  kama unampenda rafiki yako na unajali ndoa yake, weka distance . It is very sisturbing hata ingekuwa mimi nisingekubali. Jaribu kuweka umbali nao ili wa konsentrate kwenye kujenga familia yao changa.
   
 11. M

  MONALISA Member

  #11
  Feb 1, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 41
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 25
  habari wana jf, samahani sijabisha hodi manake nimejoin in leo leo na katika kuperuzi nikakutana na hii thread, NIKASHINDWA KUJIZUIA..HODI HODI.. I have been in a similar situation na my best friend who also happended kua mwanaume. tulikutana wakati tuna miaka 5 na tukawa marafiki sana mpaka primary, then secondary na chuo nikaenda nje kusoma na yeye alikuja huko huko so tukaendeleza urafiki wetu,na nilivyoamua kurudi home baada ya chuo naye alirudi home mize 6 baadae. Huu urafiki wetu ukawa kama ndugu manake tulikua kama kumbikumbi, yaani hatuachani, yalisemwa mengi ila watu waliouelewa urafiki wetu ni familia zetu tu, coz they were there from the beginning.
  Sasa mshkaji wangu alipata jiko, na alimleta kwangu siku ya 4 baada ya kukutana nae, alikua ni msichana poa sana,ila nayeye alikua na wasiwasi sana na urafiki wetu. Nilichokifanya ni kumuita mshkaji wangu na nikashinda nae na kuongea nae kwa mda mrefu sana, ilibidi nimwambie that itabidi for the 1st time in our over 2O year friendship tuweke mipaka, nilijua that she was the right girl for him na nilijua nikiendekeza urafiki wetu kama tulivyozoea hawatakua na chance nzuri ya to make it work. Nilikua nimeandika mipaka, we meet only once a week to catch up, badala ya almost evryday. kulala kwenye chumba changu cha wageni kama alivyokua amezoea is out, na biashara ya kuspend weekend nzima kwangu tukizurura au kufanya hili na lile is also out. Simu mimi kumpigia mwisho saa moja usiku, na mengineyo mengi.
  Alikua mgumu sana kukubali hali ile ila nilimwambia that he has met a great girl na I have to give them space, na atazoea tu. Huu ni mwaka wa tatu sasa na alimuoa huyo demu na wamebarikiwa kupata mtoto, bado tunakutana once a week to catch up, na mke wake hana tatizo na Hilo coz hua tunafanya around lunch time mchana.
  Mwaka jana mke wake alikuja jua that I had written rules for him ili awe na a better chance na rafiki yangu na Alikuja home kwangu kunishukuru sana because alisema mwanzoni alikua insecure na urafiki wetu.
  Kwa hio mimi ushauri wangu is lazima uwape space hao wanandoa, mke wake bado hajauelewa vizuri urafiki wenu and that can lead her to be insecure kidogo na mahusiano yenu.
   
 12. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  You said it all pretty well!
   
 13. makandokando

  makandokando JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ndoa na urafiki ni vitu viwili tofauti, na kwa sababu ni tofauti, basi kwenye list ya umuhimu lazima vitofautiane......always kinachokuja kwanza ni NDOA, urafiki badae.

  Kwa hiyo mpotezee huyo njemba. Huna hata haja ya kuongea na jamaa....hata kama nyie ni ndugu.....kama we ni mkristu, basi biblia inasema.....mume atachana na mama yake na baba yake na ataambatana na mkewe....na mke ataachana na mama yake na baba yake na ataambana na mumewe.

  mume ndio NDUGU mpya na RAFIKI mpya....na mke ndio NDUGU mpya na RAFIKI mpya.

  wewe kawe rafiki wa mumeo, na yeye muache awe rafiki ya mkewe.
   
 14. Dinnah

  Dinnah JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duh! mimi naona ningekuwa nalia tu! gaga itabidi uweke mipaka aisee maana hata mimi ningependa mume wangu kushare nae vitu vyake muhmu mimi tu sio rafiki yake tena wa kike! kama walivyosema wengine peaneni mipaka mtafanikiwa na urafiki wenu utadumu
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  nimeupenda huu ushauri.
  Gaga usimpoteze huyo rafiki.
  Wengine tunatamani tungekuwa na marafiki wa hivyo.
  Fata ushauri wa rose
   
 16. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Live and Let Others (Them) Live!
   
 17. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #17
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Yaani ndio hivyo story zote atanipa. sikuwa kama mwanaume kwani mwanamke huwezi ukawa na rafiki best wa kiume?
   
 18. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #18
  Feb 1, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Ahsante kwa ushauri wako
   
 19. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #19
  Feb 1, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapo ndo mie huwa nachoka kabisa kwanini watu hatukubali urafiki wa mwanamke na mwaume unawezekana bila kudo?
  Haya dada vunja urafiki ila mie nisingekubali kabisa UMETAFUTIA MUME KAKUGEUKA YALE YALE SHUKRANI YA PUNDA MATEKE
   
 20. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #20
  Feb 1, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,641
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  ila huo urafiki wenu umezidi bana... lool

  kinachomsumbua huyo dada ni wivu wa kawaida kabisa its just human instincts hata kama huna uhusiano wa hivyo na huyo jamaa ye atapata wivu fulani tu wala sishangai its involuntary
   
Loading...