My Best friend ameoa

Habari yako Gaga,unaendeleaje kwanza na ile ishu iliyopita????

Nafikiri kulipaswa kuwe na mipaka kati yako na huyo kaka baada ya yeye kuoa.....yes nyie ni ma-best friend lakini,wote tuna wivu na tuwapendao na hatupendi ku-share attention na wanawake wenzetu kwa mwanaume tunayempenda,kumtunza na kumjali sana......

Usiwe kikwazo cha ndoa ya watu kwa ku-value sana u-best friend wenu,have some boundaries,it takes two kuwa katika strong bond kama uliyo nayo wewe na huyo kaka,nakushauri keep a distance,waache wawe na sababu nyingine ya kutofautiana na sio wewe.....kama ni rafiki wa kweli huyo kaka ataheshimu mawazo yako kwakuwa una roho safi na unawatakia mema......

Muite huyo msichana uzungumze nae na si vibaya mumewe na muwe wako wakawepo mkaweka mambo wazi na si kwa staili ya kusutana just kueleweshana......all the best!!:coffee:

Hapo umenena, Michelle.
Hii ndio best piece of advice. Nakuzimia sana kila wakati unapochangia hoja kwenye threads za hapa jamvini. Do keep up doing the good job!:clap2:
 
Lady Gaga oops sorry ni Gaga anyways tuendelee, Ushauri wangu kwako na kwa rafiki zako wote wawili pamoja na mume wako. Liweke wazi mbele yao ili mke afahamu kabisa kama mume wako anaridhia urafiki wenu kwa maana kwamba hakuna baya linaloendelea. Kipe roho kitu inapenda. Usimwache rafiki yako jaribu kueleweshana na kuelimishana ataelewa naye ni binadamu. Mkumbushe rafikiyo uliyemtafutia mume kwamba 'Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki' ulimfaa kwa kumpatia mume na best wako ulimfaaa kwa kumpatia mke. Mwambie wivu haujengi mara nyingi unabomoa. Tena atambue hili ni nafuu kuwa na rafiki wa kiume kuliko wanawake, wanawake midomo imetuzidi kutwa kucha kuongea habari za watu lakini wanaume wana reserve. Bottom line usimwache best wako dumisha urafiki kitaeleweka.
 
mumewe ana tatizo gani? Mbona nje anachapa kama kawaida!! Ni yeye tu ndo anayeshindwa kumfanya! Ndo maana hii story haijatulia! Huo urafiki wako na huyo mwanaume ulishamharibu kisaikolojia mme wako. Sasa inaenda kumharibia mwenzio. game over...

Yawezekana kweli unavyosema, ile story yake inachanganya sana.
 
Lady Gaga, tazama, yaja siku huyo mwanamke naye ataamua kuwa "best friend wa mumeo". Usiendelee kujilazimisha pale usipotakiwa. Please, back off!! :first:
 
Daaa kuna kitu huwa nakiamini mtu anapokuwa rafiki yangu wa kawaida tu katika furaha na matatizo, vile unapokuwa kabla ya kuoa sivyo utakavyokuwa baada ya kuoa. Na hilo naliheshimu sana. Na ninatambua kabisa sasa umeoa unahitaji muda zaidi na mke wako, yeye ndo mtu wako wa karibu kuliko mimi, hata kama urafiki utakwisha ni sawa tu kwa sababu umepata mtu wa kuziba nafasi yangu, ambaye utakuwa nae karibu zaidi kuliko mimi.

Ndoa na iheshimiwe na watu wote. Kwa hiyo dada angu wala usione kama unampoteza ila tu wakati ndo umeamua kwa sasa mshauri wake wa kwanza awe mke wake.
Jitaidi na Mungu akusaidie uwe na hekima ya kufanya huyu jamaa atambue kuwa mshauri wake wa kwanza ni mke wake, hata kama kuna jambo la kukushirikisha wewe ni baada ya kuwa limepita kwa mkewe kama inawezekana.

Usikubali kabisa kupenda kusikia habari za ndoa yao bila sababu za msingi, Tena angalia manake unawezakuta hata siri zake na mke wake anakuambia kitu ambacho ni very wrong. Naomba usichukulie kwamba wewe ndo uliwaunganisha, hata kama unaona hivo amini labda ni Mungu alikutumia tu na kazi yako imeisha. Hata kama usingekuwepo wewe kama Mungu alimwandikia huyo ndo mke wake angewakutanisha tu. Tafadhali zingatia na liamini hivo. Then utakuwa na furaha na amani nafsini mwako.

Ubarikiwe.
 
Gaga na mwenzio...jamani jamani....how is it possible mkawa marafiki na wanaume hao tangu utotoni hamjawahi ku do kweli?:coffee::coffee:
 
Gaga na mwenzio...jamani jamani....how is it possible mkawa marafiki na wanaume hao tangu utotoni hamjawahi ku do kweli?:coffee::coffee:

Hatujawahi kabisa Kaizer wala sijawahi hata kumtamani hata siku moja:twitch::twitch:
 
Lady Gaga, tazama, yaja siku huyo mwanamke naye ataamua kuwa "best friend wa mumeo". Usiendelee kujilazimisha pale usipotakiwa. Please, back off!! :first:

Mhhh urafiki wa kulazimishia au wa malipizo? Yule kaka ni rafiki yangu tu hakuna jingine
 
Back
Top Bottom