Davion Delmonte Jr.
JF-Expert Member
- Oct 27, 2013
- 2,149
- 1,721
Na kwa wewe mwenye mpenzi basi ufunue biblia yako kitabu cha wimbo ulio bora, nawe utapata kuona mashairi mazuri yanayomfaa mpenziwe.......... yanavutia mno... Unadhani ni kiasi gani utamvutia mpenzi wako kwa kumpa maneno mazuri yatokayo kwenye kitabu cha MUNGU?
1:15 "Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu! Tazama jinsi ulivyo mzuri Macho yako ni kama ya hua."
2:3 "Kama mti wa mtofaa miongoni mwa miti ya msituni ndivyo alivyo mpenzi wangu miongoni mwa wanaume vijana. Ninafurahia kuketi kivulini mwa mwanaume huyu, na tunda lake ni tamu kwangu."
2:4 "Amenichukua mpaka kwenye ukumbi wa karamu, na bendera ya huyu mwanaume juu yangu ni upendo.
2:5 "Nitie nguvu kwa zabibu kavu, niburudishe kwa matofaa, kwa maana ninazimia kwa mapenzi."
4:10 "Tazama jinsi pendo lako linavyofurahisha, dada yangu, bibi arusi wangu! Ni mara ngapi zaidi pendo lako linafurahisha kuliko divai, na harufu ya manukato yako zaidi kuliko kikolezo cho chote!"
4:11 "Midomo yako inadondosha utamu kama sega la asali, bibi arusi wangu, maziwa na asali viko chini ya ulimi wako. Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ile ya Lebanoni."....