Mwongozo wa ufugaji wa kisasa wa Mbuzi wa nyama na maziwa

Wadau habari za humu, nipo na mpango wa kufuga mbuzi pembeni ya mji wa Dar Es Salaam. Kuna mdau yeyote mwenye clue ya hii shughuli?
Wapi naweza kupata mbegu nzuri za mbuzi wa kienyeji wa kuanzia?
 
mkuu Malila na wengine ni vyema kuwe na group la whatsapp au kama lipo ili wageni tupate kujua kinachoendelea,mi nnafuga wa kawaida ila natafuta Boer breed. #Malila
 
Talic, mbuzi wana soko kubwa Tanzania. Ukiwa na idadi yoyote jaza kwenye Fuso peleka Pugu au Vingunguti utauza wote, UTAONDOKA NA CASH YAKO MFUKONI.
 
Mkuu Aman Ng'oma,

swali langu ni hivi, je ukianza na majike 50 na kila mmoja wao akizaa, si unaweza kuanza kukamua maziwa? Na ukikusudia kufanya hivyo unaweza kupata maziwa yake kwa siku ngapi ndani ya mwaka mzima, ukizingatia muda wakati wanakuwa dry kabla ya kuzaa, kama vile kwenye ng'ombe?

Asante in advance..
 

Rashiditanz

Nashukuru kwa swali lako zuri.

Kimsingi, mbuzi mia wakizaa utaweza kuwakamua maziwa ingawa hutopata mengi kama yanayozalishwa na mbuzi wa kisasa wa maziwa, kwasababu mbuzi hao si pure wa maziwa ni chotara na uwezo wake wa kutoa maziwa ni mdogo. Kwa mantiki hiyo utakapowakamua maziwa, kwasababu ni mbuzi wengi waliozaa, utaweza kupata maziwa mengi ukiyachanganya pamoja na hivyo kukupatia kipato cha ziada kutokana na mauzo ya maziwa.

Maziwa ya mbuzi yana Virutubisho vingi ukilinganisha na maziwa ya ngombe na kwa msingi huo inashauriwa sana watu wazima na watoto waweze kuyatumia maziwa hayo. Pia maziwa ya mbuzi yanapunguza cholestro. Faida ni nyingi nimetaja kwa uchache tu.

Changomoto ya maziwa ya mbuzi ni kutozoeleka na watu kwa ajili ya kufanya matumizi kama ilivyo kwa maziwa ya ng'ombe

Ukamuaji wa maziwa ya mbuzi unaaza mara tu baada ya mbuzi wako kuzaa na utaendelea hadi siku 27 +/- 4 kabla ya kuzaa.

Kumkausha mbuzi kunasaidia kuyafanya yale maziwa ya mwanzo ya mbuzi kuwa bora zaidi.

Asante.
 
Na vip hii biashara ya mbuzi, mfano kuchukua huko Dom na vijijini, then kuwaleta hapa dsm, biashara inalipa? Ushauri
 
Na vip hii biashara ya mbuzi, mfano kuchukua huko Dom na vijijini, then kuwaleta hapa dsm, biashara inalipa?? Ushauri

Renyo,

Hiyo biashara inalipa tu na wengi wanaifanya ila kitu cha msingi na muhimu ujue bei ya Sokoni DSM ili ikuongoze kwenye kuwanunua Dodoma
 
Hawa mbuzi ni mbuzi bora walioboreshwa, wanapatikana dodoma. Ni matokeo ya cross breed iliyofanyika kati ya mbuzi wa kienyeji wa dodoma na exotic breed.Hivyo wengi wa uzao wao huzaa mapacha. Mbuzi hawa huuzwa tsh elfu 50, wakiwa na umri wa miezi 5.
Sasa kama wanauzwa elfu 50 huko dodoma ukiwapeleka dar utawauza bei gani kwa kila mbuzi?
 
Kwa wale wajasiriamali wanaohitaji kujiunga na group ya WhatsApp kwa masuala ya kijasiriamali nicheki 0762600100
 
Mkuu nakuomba ujiunge nasi WhatSapp kwenye group la Biashara na Wajasiriamali Tangaza Business Solutions utatufaa nakutusaidia juu ya elimu ya ujasiriamali.

Namba yetu ya WhatSapp ni 0785-074040
Karibu sanaaaa Mkuu
 
Mkuu ningenda kujua ni majani ya aina gani ambayo mbuzi au kondoo akila yanampa afya tele? Pia kama kuna vyakula vingine ambavyo anayumia naomba unieleze ili nipate uzoefu kabisa. Maana hujaongelea chakula chao na gharama zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…