Mwongozo wa Namna ya Kuanzisha na Kuendesha Biashara ya Mini Supermarket

Sio location pekee, hii biashara zinachangamoto zake kubwa sana kwa Tanzani na zinasababishwa na kuwepo vijiduka vya wakina Masawe vingi sana mtaani, na hizi supermarket ni kwa Middle income, ila kwa watu wa kawaida ni ngumu sana. Hata supermarket kubwa kama Nakumat wanakumbana na changamoto kubwa sana, ndo maana ukifanya utafiti Minsupermarket ndo zinaongoza kwa kufungwa, unaweza shangaa leo imefunguliwa supermarket mahali baada ya miezi 6 hutaliona.

Kwa Dar kuwepo masoko ya bidhaa kama Kariakoo na masoko mengine ni changamoto kwa supermarket, na changamoto kubwa kabisa ni kuwepo maduka ya rejareja mengi mtaani.
 
Kiongozi naomba uweke utofauti kwani Supermarket ni neno as it is na lina maana pana zaidi..ikishakua "Mini" haiwezi kuwa supermarket inakua Minimarket.
Watu wengi sana huwa wanachanganya haya maneno. Mimi kwa somo la commerce nililofundishwa o-level niliambiwa kuna Mini Market, Super Market, na Hyper Market.There is NOTHING like Mini SuperMarket!
 
Watu wengi sana huwa wanachanganya haya maneno. Mimi kwa somo la commerce nililofundishwa o-level niliambiwa kuna Mini Market, Super Market, na Hyper Market.There is NOTHING like Mini SuperMarket!!!
Hapana mkuu neno mini supermarket lipo sana na linatumika sana na ni sahihi kabisa. Inawezekana kwenye taaluma huku kwetu halijaingia na hata ukizingatia utamaduni wa supermarket hauna mizizi sana huku kwetu. Lakini kwa Uingereza ambako Kiingereza kinakotoka convenience store au mini supermarket linatumika na zipo sana na zinaeleweka hivyo: The rise, fall and rise of the mini-supermarket - BBC News unaweza soma hiyo link kwa maelezo ya upana Zaidi.

Nafikiri huyu bwana mwenye uzi tumsaidie kuhusu kuanzisha mini supermarket, mjadala wa maana ya neno sidhani kama unashika hapa.
 
Hakuna kitu duniani kinaitwa MINI SUPERMARKET.

Superior haiwezi kuja kuwa mini inferior tena.

English sahihi ni MINIMARKET au SUPERMARKET tu.

Au ni sawa na kusema SMALL LARGE MARKET does it sound?
Hapa kinacho hitajika ni msaada wa ushauri wa hiyo biashara na sio usahihi wa lugha, umeleweka mtaalam katika ubora wako.
 
Naombeni ushauri,

Nina mil 5 je naweza fungua mini Supermarket. Nipo Arusha, pia naomba kujua kama nikifungua bidhaa nachukulia wapi?

Mawazo yenu please!
 
Unaweza dumbukiza pesa kwa kuuza biskuti ikaja kukupa asala tu,swala siyo kua na ofisi yenye kung'aa viyoo,swala zima ni kupata pesa na hyo hela ni ndogo kwa biashara hyo.

Cha kufanya nenda mahala penye vyanzo vya maji kalime bustani ukuze kwanza huo mtaji ndo uje ufungue ukipendacho, hyo hela ni hela kweli kufanyia kazi ila bado ni ndogo, pango tu lenyewe linakula hiyo hela yote, bado TRA, bado jiji na leseni ya biashara, hujaweka mzigo wenyewe.nenda kapige bustani kwa huo mtaji.
 
Unaweza kuanza but kma tayari una Shemu hiyo hela isiinhie kwenye jengo,mapato TRA wala TFDA. Iwe ya mzigo tu hapo unaweza .inalipa kwenye Shemu yenye mzunguko wa biashara na uuze bites and soft drinks kwanza ikijizungusha faster unaanza kuongeza bidhaaa usikate tamaa mapema ni kubwa San hy hela na mzigo ht Moshi town wanauza kwa jumla biscuits sema unatakiwa uende dar KITUMBINI ndiyo kuna Mali nyingine za supermarket. Hope imeelewa
 
Unaweza kuanza but kma tayr una Shemu hiyo hela isiinhie kwenye jengo,mapato TRA wala TFDA.iwe ya mzigo tuuu hapo unaweza .inalipa kwenye Shemu yenye mzunguko wa biashara na uuze bites and soft drinks kwanza ikijizungusha faster unaanza kuongeza bidhaaa usikate tamaa mapema ni kubwa San hy hela.na mzigo ht Moshi town wanauza kwa jumla biscuits sema unatakiwa uende dar KITUMBINI ndiyo kuna Mali nyingine za supermarket.. Hope imeelewa
Asante sana kwa ushauri nimepata kitu hapo
 
Super-market huwezi labda market utaweza kwani pale utavibeba vitu vyao upeleke nyumbani. M5 si kitu kwani hiyo kodi tu na leseni utaweza zimia. Chezea mengine usiiguse Tra mkuu.
 
Haitoshi usidanganywe.

Labda kidoogo kwa lindi, mtwara, sikonge, singida n.k
 
MAHITAJI, HUDUMA, ENE, CHANGAMOTO NA FAIDA

Wakuu leo naomba tuzungumzie hii biashara na vitu vya kuzingatia kwa wale walioifanya na tunaoendelea kuifanya au hata wale wanaotegemea kuifanya.

Kwanza kabisa hii ni biashara ambayo inahitaji mtaji mkubwa kidogo kwa sababu lazima uwe na friji ya display (hapa hata kama unazo za makampuni lazima uwe na yako moja au mbili). Freezer pia ni lazima uwe nayo moja au mbili kwa ajili ya frozen foods kama saucages,kuku,samaki au hata icecream.

Pili, mashelfu (shelves)

Ambapo hapa zipo aina nyingi kulingana na mtaji wako. Unaweza kuweka za special unafunga na kufungua tu ambazo ni ghali au ukaamua kuchongesha kwa mafundi wetu wa alluminium na ukazipaka rangi ukasave gharama kubwa (hii hata supermarkets kubwa siku hizi wanafanya na unaweza usigundue kama ni za kibongobongo)

Tatu ni bidhaa ambapo hapa ni wewe kuzingatia unaweka bidhaa aina nyingi na tofauti tofauti hata kama ni same brand. Hii inasaidia sana mtu kuhamasika kununua zaidi maana tabia za wateja za kununua zipo kwenye macho. Mtu anaweza toka home anakuja kununua lotion lakini akajikuta kanunua na vitu vingine baada tu ya kuviona. Ndio maana supermarket unaweza kuwa unauza sana japo unawateja wachache sababu mtu akija hakosi kuacha elfu 50 au laki sababu ya saikolojia ya kuvutiwa na bidhaa anazokutana nazo uso kwa uso tofauti na duka la kawaida.

Pia kwenye bidhaa muhimu kuliko vyote ni expiry date ya bidhaa. Zingatia sana,bidhaa zingine utakuta zimebakiza mda mfupi wa kuexpire usipoangalia itakula kwako. Pia bidhaa zingine unaweza chukua zimetoka kiwandani karibuni na bado zikaexpire uko nazo. Hapa kuzingatia ni bidhaa zipi ni fast moving na zipi slow moving kulingana na eneo ulipo. Zile zinazotoka taratibu ni kuchkua kidogo tu,sio kujaza duka mradi kupamba tu na watu hawanunui.

Pia kuna baadhi ya bidhaa ukiwa na supplier wakuaminika wanaweza kukubadilishia bidhaa zikiexpire..hawa ni wachache sana.
Pia kuna baadhi ya supplier wanaweza kukupa bidhaa on credit. Unapewa bidhaa unaweka kuuza bila kuwalipa cash,hii ni nzuri ila kuwa nayo makini inaweza kukuathiri au ikawa mwanzo wa kukuangusha maana unaweza kudivert fund kufanyia mambo mengine na kusahau liability uliyonayo kwa supplier. Ni vizuri ukalipa cash kwa bidhaa unazonunua.

Nne, ni location
Kimsingi hili ndio jambo la kwanza kuzingatia kabla ya vyote kabla hujaanza biashara. Hili lipo wazi,good location,good sales. Usiombe ukafungua sehemu ambako hakuna wanunuzi utajuta.
Parking pia ni lazma uzingatie maana wengi wanaoshop kwenye supermarkets ni watu wa maisha ya kati na kuendelea na wengi huja na magari.

Tano, ni huduma
Hapa namaanisha hudma kwa wateja lazima iwe nzuri na hata umsaidie kuchagua kinachomfaa zaidi.
Unaweza kukaa mwenyewe dukani na ukaweka wasaidizi ili ku-monitor sales na service. Pia hapa zingatia biashara nyingi hufa sababu ya usimamizi mbovu,kama unaweza tafadhali simamia mwenyewe au mkeo/mmeo kama anajielewa.(wenzetu wahindi hukaa wenyewe na hata akitoka dakika tano yupo radhi afunge).

Sita, ni usalama
Hapa namaanisha usalama wa bidhaa,pesa,na vingine. Funga cctv camera zitakusaidia kuona blind spots zote. Hapa inasaidia kudhibiti wizi pia.

Pia kwa kudhibiti mauzo weka computer yako yenye program ya mauzo na bar code scanner ili kurahisisha mahesabu na kukeep records za mauzo. Uzuri wa computer itakupa report zote za mauzo kwa siku,wiki,mwezi na hata mwaka utaona hadi graph za mauzo kama zinapanda na kushuka. Hizi program zipo nyingi tofautitofauti na uzuri zote zinalengo moja ya kukeep record na kurahisisha mahesabu.

Saba, ni bei (pricing)
Weka bei za kawaida ambazo ni common, usiwe na ile dhana ya kwamba bidhaa za supermarket ni ghali hapo utakimbiwana utajuta kurudisha wateja. Advantage ya mini-supermarket ni mauzo mengi sasa ukirogwa kuweka bei juu zaidi ya zilizozoeleka hutauza

Nane, Kata bima
Hii itakusaidia sana kukuepusha na majanga ya kupoteza mtaji na kurudi square one

Changamoto
Changamoto kubwa ni mtaji. Angalau milioni 10 unaweza anza nayo kwa sehemu yenye frame ndogo kitu ambayo wengi wanaweza wasimudu tofauti na duka la kawaida ambalo hata milioni tosha kuanza

Pili ni kodi sababu utahitaji eneo kubwa kiasi au kuchukua frame mbili uziunganishe. Kwa hiyo kama mauzo hayatakua mazuri utahaha kwenye ulipaji kodi

Tatu gharama ya umeme itakua juu kidogo sababu utajitaji angalau friji mbili au tatu (pamoja na za makampuni) pamoja na freezer na taa za kutosha kumulika ndani muda wote. Jitahidi sana kama unaweza nunua friji na freezer mpya maana hazili sana umeme kama za mtumba.

Nne ni TRA maana hapo efd machine lazima ihusike..hapo hakuna namna hasa kwa usawa huu.

Tano ni bidhaa kama nilivyosema expiry date. Utahitaji kukagua bidhaa mara kwa mara kuepusha kukutwa na bidhaa iliyoexpire kwenye shelf.

Sita, ni muda
Hii ni biashara ambayo utahitajika kufungua muda wa kawaida wa saa mbili au saa tatu ila kufunga ni lazima iwe usiku wa angalau saa tatu maana jioni ndio mda wengi hutoka kazini na kufanya manunuzi. Pia utapaswa kufanya kazi jumatatu hadi jumatatu. Hii ndio maana halisi ya ujasiliamali si lelemama.

Faida
Ukipata location nzuri hii ni biashara moja tamu mno na yenye faida nzuri kila siku iendayo kwa Mungu. Kama nilivyosema wateja wengi wa supermarket hupenda kununua in stock kwa hiyo kwa mteja mmoja unaweza uza bidhaa za watu 10 au 20 anazouza mangi.
Pili hii biashara inakibali cha kuweka bidhaa aina nyingi kama pombe,matunda,vegetables,vipodozi, stationeries, clothes,nafaka,etc kwa hiyo uwezekano wa kuuza vizuri ni mkubwa.

Naomba niishie hapa,nakaribisha uzoefu na changamoto toka kwa wengine
 
Back
Top Bottom