Mwongozo wa Namna ya Kuanzisha na Kuendesha Biashara ya Mini Supermarket

Duh hahahah najicheka koz siku mbili nyuma nilikua nawaza vitu halafu hii ni kama imenipa mwanga kwa upande fulani
 
Duh hahahah najicheka koz siku mbili nyuma nilikua nawaza vitu halafu hii ni kama imenipa mwanga kwa upande fulani
Hongera sana kwa kuwaza, usingewaza usingepata mwanga (dots are always connected backward). Besides,first creation starts with the mind
 
Wakuu leo naomba tuzungumzie hii biashara kwa wale walioifanya na tunaoendelea kuifanya au hata wale wanaotegemea kuifanya.

Kwanza kabisa hii ni biashara ambayo inahitaji mtaji mkubwa kidogo kwa sababu lazima uwe na friji ya display (hapa hata kama unazo za makampuni lazima uwe na yako moja au mbili). Freezer pia ni lazima uwe nayo moja au mbili kwa ajili ya frozen foods kama saucages,kuku,samaki au hata icecream.

Pili mashelfu (shelves) ambapo hapa zipo aina nyingi kulingana na mtaji wako. Unaweza kuweka za special unafunga na kufungua tu ambazo ni ghali au ukaamua kuchongesha kwa mafundi wetu wa alluminium na ukazipaka rangi ukasave gharama kubwa (hii hata supermarkets kubwa siku hizi wanafanya na unaweza usigundue kama ni za kibongobongo)

Tatu ni bidhaa ambapo hapa ni wewe kuzingatia unaweka bidhaa aina nyingi na tofauti tofauti hata kama ni same brand. Hii inasaidia sana mtu kuhamasika kununua zaidi maana tabia za wateja za kununua zipo kwenye macho. Mtu anaweza toka home anakuja kununua lotion lakini akajikuta kanunua na vitu vingine baada tu ya kuviona. Ndio maana supermarket unaweza kuwa unauza sana japo unawateja wachache sababu mtu akija hakosi kuacha elfu 50 au laki sababu ya saikolojia ya kuvutiwa na bidhaa anazokutana nazo uso kwa uso tofauti na duka la kawaida.
Pia kwenye bidhaa muhimu kuliko vyote ni expiry date ya bidhaa. Zingatia sana,bidhaa zingine utakuta zimebakiza mda mfupi wa kuexpire usipoangalia itakula kwako. Pia bidhaa zingine unaweza chukua zimetoka kiwandani karibuni na bado zikaexpire uko nazo. Hapa kuzingatia ni bidhaa zipi ni fast moving na zipi slow moving kulingana na eneo ulipo. Zile zinazotoka taratibu ni kuchkua kidogo tu,sio kujaza duka mradi kupamba tu na watu hawanunui.
Pia kuna baadhi ya bidhaa ukiwa na supplier wakuaminika wanaweza kukubadilishia bidhaa zikiexpire..hawa ni wachache sana.
Pia kuna baadhi ya supplier wanaweza kukupa bidhaa on credit. Unapewa bidhaa unaweka kuuza bila kuwalipa cash,hii ni nzuri ila kuwa nayo makini inaweza kukuathiri au ikawa mwanzo wa kukuangusha maana unaweza kudivert fund kufanyia mambo mengine na kusahau liability uliyonayo kwa supplier. Ni vizuri ukalipa cash kwa bidhaa unazonunua.

Nne ni location
Kimsingi hili ndio jambo la kwanza kuzingatia kabla ya vyote kabla hujaanza biashara. Hili lipo wazi,good location,good sales. Usiombe ukafungua sehemu ambako hakuna wanunuzi utajuta.
Parking pia ni lazma uzingatie maana wengi wanaoshop kwenye supermarkets ni watu wa maisha ya kati na kuendelea na wengi huja na magari.

Tano ni huduma
Hapa namaanisha hudma kwa wateja lazima iwe nzuri na hata umsaidie kuchagua kinachomfaa zaidi.
Unaweza kukaa mwenyewe dukani na ukaweka wasaidizi ili ku-monitor sales na service. Pia hapa zingatia biashara nyingi hufa sababu ya usimamizi mbovu,kama unaweza tafadhali simamia mwenyewe au mkeo/mmeo kama anajielewa.(wenzetu wahindi hukaa wenyewe na hata akitoka dakika tano yupo radhi afunge).

Sita ni usalama
Hapa namaanisha usalama wa bidhaa,pesa,na vingine. Funga cctv camera zitakusaidia kuona blind spots zote. Hapa inasaidia kudhibiti wizi pia.
Pia kwa kudhibiti mauzo weka computer yako yenye program ya mauzo na bar code scanner ili kurahisisha mahesabu na kukeep records za mauzo. Uzuri wa computer itakupa report zote za mauzo kwa siku,wiki,mwezi na hata mwaka utaona hadi graph za mauzo kama zinapanda na kushuka. Hizi program zipo nyingi tofautitofauti na uzuri zote zinalengo moja ya kukeep record na kurahisisha mahesabu.

Saba ni bei (pricing)
Weka bei za kawaida ambazo ni common, usiwe na ile dhana ya kwamba bidhaa za supermarket ni ghali hapo utakimbiwana utajuta kurudisha wateja. Advantage ya mini-supermarket ni mauzo mengi sasa ukirogwa kuweka bei juu zaidi ya zilizozoeleka hutauza

Changamoto
Changamoto kubwa ni mtaji. Angalau milioni 10 unaweza anza nayo kwa sehemu yenye frame ndogo kitu ambayo wengi wanaweza wasimudu tofauti na duka la kawaida ambalo hata milioni tosha kuanza

Pili ni kodi sababu utahitaji eneo kubwa kiasi au kuchukua frame mbili uziunganishe. Kwa hiyo kama mauzo hayatakua mazuri utahaha kwenye ulipaji kodi

Tatu gharama ya umeme itakua juu kidogo sababu utajitaji angalau friji mbili au tatu (pamoja na za makampuni) pamoja na freezer na taa za kutosha kumulika ndani muda wote. Jitahidi sana kama unaweza nunua friji na freezer mpya maana hazili sana umeme kama za mtumba.

Nne ni TRA maana hapo efd machine lazima ihusike..hapo hakuna namna hasa kwa usawa huu.

Tano ni bidhaa kama nilivyosema expiry date. Utahitaji kukagua bidhaa mara kwa mara kuepusha kukutwa na bidhaa iliyoexpire kwenye shelf.

Sita ni muda
Hii ni biashara ambayo utahitajika kufungua muda wa kawaida wa saa mbili au saa tatu ila kufunga ni lazima iwe usiku wa angalau saa tatu maana jioni ndio mda wengi hutoka kazini na kufanya manunuzi. Pia utapaswa kufanya kazi jumatatu hadi jumatatu. Hii ndio maana halisi ya ujasiliamali si lelemama.

Faida
Ukipata location nzuri hii ni biashara moja tamu mno na yenye faida nzuri kila siku iendayo kwa Mungu. Kama nilivyosema wateja wengi wa supermarket hupenda kununua in stock kwa hiyo kwa mteja mmoja unaweza uza bidhaa za watu 10 au 20 anazouza mangi.
Pili hii biashara inakibali cha kuweka bidhaa aina nyingi kama pombe,matunda,vegetables,vipodozi, stationeries, clothes,nafaka,etc kwa hiyo uwezekano wa kuuza vizuri ni mkubwa.

Naomba niishie hapa,nakaribisha uzoefu na changamoto toka kwa wengine
Kwenye upande wa kodi inaweza daiwa kias gani.. ??
hii ni lengu langu nlilonalo kichwan
Ila cjui lini nita ianza..
 
mimi nimepanga fast food restaurant , vifaaa nimenunua kama 12 million kutoka china sasa hivi natafuta sehemu ya kufungua naona labda ntapata 50000 kwa siku. mawazo yoyote yanakaribishwa
 
Wadau naombeni msaada wenu wa mawazo. Nahitaji kufungua mini market capital na location ninayo.

Tatizo ni how ya kupata good suppliers, system za mauzo,where to get shelves na vinginevyo sijawahi fanya hii biashara I am new to it.

Naomba kuwasilisha.
 
damax shelves ni laki 4 kwa double single laki 3, ukichukua nyingi wanakupunguzia ukitaka no yao njoo pm vitu unafata kitumbini na kariakoo , kuhusu system Don Clericuzio atakusaidia
 
damax shelves ni laki 4 kwa double single laki 3, ukichukua nyingi wanakupunguzia ukitaka no yao njoo pm vitu unafata kitumbini na kariakoo , kuhusu system Don Clericuzio atakusaidia

Hahaha, ujue hapo anahitaji kupata uzoefu kwa walioko field.

damax ukiweza jaribu kutembelea mtu mwenye kitu kama unachotaka kukifanya, omba uzoefu wake, ushauri kuhusu suppliers, system strength na changamoto zote.

Ukifanya visit kama store 5, haikosi mbili zitakupa majibu stahiki.
 
Hahaha, ujue hapo anahitaji kupata uzoefu kwa walioko field.

damax ukiweza jaribu kutembelea mtu mwenye kitu kama unachotaka kukifanya, omba uzoefu wake, ushauri kuhusu suppliers, system strength na changamoto zote.

Ukifanya visit kama store 5, haikosi mbili zitakupa majibu stahiki.
Huo mbichwa wako mkubwa nauaminia sana, hauniangushagi
 
Mbona sijaelewa hapa, naona hajataja location lakini mmeshasema vitu atachukulia kitumbini...vipi kama yupo Babati?
 
Hivi huwa zina faida wakuu? Ni jambo kuna mdau huwa analisema sema kuhusu kufungua najiwazia inafaida kweli ukizingatia viduka ni vingi kila baada ya mtaa kuna kiduka cha mangi cha basic needs...
 
Hivi huwa zina faida wakuu? Ni jambo kuna mdau huwa analisema sema kuhusu kufungua najiwazia inafaida kweli ukizingatia viduka ni vingi kila baada ya mtaa kuna kiduka cha mangi cha basic needs....
Location ndio kila kitu, ukibugi location imekula kwako. Shida/changamoto ipo kwa sababu ya uwepo wa viduka/maduka kila baada ya mita kumi. Hivyo ni lazima location yako iendane na "mini super market"!!!
 
Habari wadau? Ni matumaini yangu kwamba hamjambo kabisa.

Nafikiria kuanzisha mini super market hapa mjini. Sasa kikubwa nachoomba kwa wenye uzoefu na uelewa wanipe abcd kidogo kuhusu biashara hii.

mfano;

1. Changamoto zake na uzuri wake
2. Namna bora ya kuiendesha biashara hii
3. Suppliers wa bidhaa za biashara yenyewe n.k

4. Makadirio ya mtaji na ziada. (Ingawa tayari nimejipanga na 20M+)

Tafadhali naomba mawazo mazuri na ya kusaidiana ili tujenge taifa.

Asanteni sana.

~Jodeo ~
 
Back
Top Bottom