Wakuu Salamaa? Naombeni muongozo wa kisheria juu ya jambo lifuatalo;
Kunashamba ambalo mmiliki anashida na anahitaji kuniuzia ila shamba lenyewe kuna mtu analima (kawekewa rehani mpaka afanye marejesho ya hela husika). Aliyewekewa rehani kafariki kama miezi mitano iliyopita.
Huyu muuzaji kanifuata kwamba anataka kuliuza nikamwambia mbona shamba lenyewe lipo kwenye rehani? Akaniambia atamalizana na familia ya marehemu sisi tuuziane tu; nikamwambia siwezi nunua angali kuna mtu anayelima kwa rehani.
Huyu muuzaji aliniita nimsindikize siku ya arobaini ya aliyewekewa rehani ili nijue kiasi gani anadaiwa, nikaenda na nikaambia anadaiwa 1M, ila marehemu anawake wawili, lakini nikadokezwa mke mdogo ndiye aliyekuwa analima shamba lile na marehemu.
Maamuzi ya siku ya arobaini kuhusu shamba hilo ni kwamba familia itaendelea kulilima hilo shamba (hata ninapoandika hapa shamba lishaoteshwa mahindi) mpaka watakaporudishiwa hela yao.
Nikamkomalia muuzaji kwamba nataka awarudishie hela familia ya marehemu na nitalinunua shamba baada ya malipo hayo kurejeshwa ila muuzaji anang'ang'ania kwamba anashida na hela na anahitaji hela mara moja na mambo ya kurudisha hela ya rehani atafanya taratibu kwani familia yenyewe ya mtu aliyemwekea rehani hawana uelewano ya nani apewe hiyo hela (ukumbuke nilipohuzuria arobaini ya marehemu kuna kijana wake wa kwanza kachaguliwa kuchukua nafasi ya baba yake chini ya usimamamizi wa baba yake mkubwa na kiongozi wa ukoo wao).
Wakuu nimekwama nifanyaje? Sheria inasemaje katika hali kama hii?
NB: Shamba nalihitaji kwani ni zuri sana