MIDFIELD
JF-Expert Member
- May 27, 2013
- 1,944
- 701
Kimsingi lazima tuwe wakweli jamani, tunaheshimu sana imani za watu ila haya maspika yanayotumiwa ktk makanisa yanayoota kama uyoga ktk makazi ya watu, ni KERO kubwa sana kwa watu. Utakuta ibada inafanyika kuanzia asbh mpaka jioni ni makelele mpaka vichwa vinauma mnaokaa karibu hapo. wakati mwingine unalazimika kuondoka nyumbani kwako kupisha hiyo mitetemo ya maspika mpaka wamalize ndo urudi. sasa ya nini kutesana hivi???
Kuna haja ya kutungwa sheria juu ya mambo haya, vinginevyo tutaendelea kuumizana bila sababu za msingi. Na mabar ambayo yapo karibu na makazi hali kadhalika ambayo music unapigwa utadhani hall la music. Kama vp haya majumba yao wawe wanaweka sound proof ili kutokuwaathiri wenzao