Mwl Nyerere na misamiati yake

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,867
8,282
Wandugu namkumbuka sana Mwl Nyerere kwa kuibua maneno mapya kama anaelezea mambo fulani ,
Kwa mfano
1.Iddi Amini alibatizwa jina la Nduli(joka) wakati alipovamia Tanzania,Mwl alisema tutalitoa kwenye nchi yetu Nduli llililo vamia nchi yetu.
2.Wakenya waliitwa manyang'au walipovunja EAC na kutaka kuleta za kuleta
3.Alitumia neno kung'atuka alipotangaza kustaafu uongozi wa taifa
4.Alitumia neno kuchafua hali ya hewa wakati Aboud Jumbe alipotemeshwa uongozi huko Idodomya
5.Alianzisha neno vigogo( wasioguswa) wakati wa mapambano ya wahujumu uchumi wakiwa na marehemu Sokoine,vigogo walikuwa wale wenye nafasi katika utumishi wa umma wenye nafasi za juu ambao walijiona wao hawaguswi,
6.CCM sio mama yangu....
7.Kama mnampenda kampikieni chai,hayo aliyatamuka alipokuwa anawaambia wapambe wa mngombea uraisi mla rushwa enzi hizo(huyo jamaa aliulizwa kijana fedha za kujengea hayo mahekalu umepata wapi wakati hufanyi biashara pale walipotaka kujua kwa nini Mwl anamkataa kijana wao,aliwaambia wazee fulani
Hayo ni baadhi tu ya maneno ambayo Mwl Nyerere aliyatumia wakati akiwananga akina HAKUNAGA,maneno mengine panapo majaliwa
 
Back
Top Bottom