Mwl. Nyerere Marathon kuzinduliwa Oktoba Mosi, 2022

Apr 9, 2022
66
32
Na. Mwandishi wetu,

IMG-20220815-WA0007.jpg


Wadau mbalimbali kwa kushirikiana na Makumbusho ya Taifa kwa pamoja wanaandaa mbio za hiari kwa kushirikiana na Wadau zijulikanazo kama Mwalimu Nyerere Marathon ikiwa Mbalimbali inaandaa mbio za hiari zijulikanazo kama Mwalimu Nyerere Marathon ikiwa ni sehemu ya program ya miaka kumi ya kuenzi na kutangaza, Urithi wa Mwalimu Nyerere ambaye ni muasisi wa Taifa letu.

Hayo yamezungumzwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Nchini Dkt Noel Lwoga wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea umma namna mbio hizo zitakavyo fanyika.

Dkt Lwoga amesema kwamba mnamo Aprili 13 mwaika huu Watnzania waliadhimisha miaka 100 ya kuazaliwa kwa baba wa taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ,maadhimisho hayo yalifanyika kwenye maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Butiama katika Kijiji alichozaliwa na maeneo mengine ambapo yatafanyika matamasha ya kuenzi na kutangaza Urithi wake.

Aidha ameendelea kufafanua kuwa mbio za hiari za Mwl. Nyerere(Mwl.Nyerere Marathon) ni sehemu ya Mpango wa miaka 10 ya kuenzi na kutraqngaza Urithi wa Mwl.Nyerere uliozinduliwa na Waziri Mkuu mstaafu Mheshimiwa Mizengo Pinda apiri 13 mwaka huu Butiama.

“Mbio hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika tarehe 01 oktoba 2022,zinalenga kutangaza Urithi wa Mwl.Nyerere kitaifa na kimataifa , pia mbio hizi zinalenga kuanzisha zao jipya la utalii kupitia michezo na kukusanya michango ya fedha za hiari kwea ajili ya kuboresha miundombinu ya makumbusho na vivutio vya malikale vya kumbukizi ya Mwl. Nyerere ambao unaratibiwa na Makumbusho ya Taifa.”amesema Dkt Lwoga

Aidha ameongeza kuwa lengo ni kukusanya kiasi cha fedha Tzs 300,000,000 kutokana na gharama za usajili wa wakimbiaji na wafadhili mbalimbali watakaojitokeza kuchangia.

Mbio nizo ni za kipekee kwqasababu zinahusisha siku mwezi na mwaka aliozaliwa Mwl.Nyerere yaani tarehe 13 April 1922, hivyo kutakuwa na mio za kilometa 22 zenye washiriki 300,mbio za kilometa 13 zenye washiriki 300, mbio za kilometa 4 zenye washiriki 200,ambao ni viongozi na watumishi mbalimbali na washiriki wengine 200 ambao ni wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.
 
Back
Top Bottom