Hakika kazi ya kuondoa ujinga ni ngumu sana katika mazingira kama haya, just chukulia mtu yupo kwa ajili ya kukusaidia uondokane na ujinga, wewe unakataa mbinu anazkupa mwalimu kisha unaona ni kero sana kwa mwalimu kukufuatafuata unaamua kuua. Je tutafika????
Sio siri,sasa hivi moja ya watu ambao huenda hawaaminiki na walio katika maisha magumu sana kwa sasa na tunakokwenda ni waalimu. Naposema waalimu simaanishi wa shule za msingi tu la hasha bali wo kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu japo wao hujiita wahadhiri.Kutokana na mfumo wetu mabaya wa elimu usiorekebishwa mara kwa mara kwa maslahi ya taifa, wanafunzi wamekuwa hawajui wajibu wao,wengi hawajui kwa nini wamo humo mashuleni,hawajui kazi ya mwalimu ni ipi,na hata waalimu wenyewe kutokana na kutokana na mfumo huohuo wa uanafunzi wamekuwa nao hawajui wajibu wao saa nyingine ni upi kwa wanafunzi,matokeo yake kila kitu kimekuwa kikifanya kwa uzoefu na expediency tu.
Sasa hivi mwalimu akisahisha mtihani wa mwanafunzi na kumkosehs ajapo kwa haki kabisa basi mwalimu huyo atachukiwa sana,mwalimu akimuonya mwanafunzi kwa jambo la haki kabisa mf,utoro au ulevi, bangi nk mwalimu huyo atachukiwa kabisa.Kutokana na kuwa walimu nao kama vile hawana mtu wa kuwatetea hasa wanapopata vipigo toka kwa wanafunzi,migomo,na hata kuuawa kama hivyo,Waalimu wetu hao baadhi yao wameishi a kusema nifanye hivi kwa faida ya nani wakati watu wenyewe hawaelewi.
Kutokana na hilo wengi sasa wanafundisha tu,mwanafunzi aelewe asielewe potelea kokote sio wajibu wangu,wengine kuepuka mtatizo wanaamua kustandardise tu maksi kwa kuwafaulisha wanafunzi wote hata kama wajinga basi,wengine wao ni lesser fair tu,na hawa ndio hupendwa sana na wanafunzi.Hii ndio elimu yetu iendako sasa.