MotoYaMbongo
JF-Expert Member
- Jan 7, 2008
- 2,146
- 886
Mwl wa nidhamu wa shule ya sekondari Chemchemi mkoani Singida ameuwawa kwa kuchomwa na kisu kifuani. Mwl huyo amechomwa kisu na wanafunzi wake hao, kwa sababu alikuwa anamfuatilia mmoja wa wanafunzi hao aliekuwa mtoro wa kupindukia. Wanafunzi hao walimvizia mwl huyo alipokuwa anatoka kilabuni na ndipo walipomvamia na kumtendea ukatili huo. Hadi sasa wanafunzi hao wametiwa mbaloni na jeshi la polisi na watafikishwa mahakamani siku yoyote kuanzia kesho.