Mwizi na Mlegezo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwizi na Mlegezo

Discussion in 'Celebrities Forum' started by papag, Mar 16, 2012.

 1. papag

  papag JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 688
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  [h=2][/h][​IMG]Mtindo wa Kata K


  Mwizi mmoja hapa London aliyekuwa akijaribu kukimbia baada ya kufanya wizi wake, aliuhisi mkono wa sheria ukimkamata baada ya kuanguka, kwa kuwa alikuwa amevaa suruali yake katika mtindo uitwao mlegezo, au kata K.
  Gazeti la Metro limesema John O'Dell alisimamishwa na polisi katika eneo la harringey, kaskazini mwa London siku ya Jumapili, lakini badala yake akaamua kukimbia.
  Hata hivyo, kwa kuwa alikuwa amevaa suruali yake bila mkanda na katika mtindo wa mlegezo, suruali hiyo iliteremka na kumfanya adondoke na kukamatwa na polisi mara moja. Tukio hilo lilishuhudiwa na wapita njia. Mpita njia Harry Robbins aliyeshuhudia sakata hilo amesema, kwa kuwa hakuwa amevaa mkanda, ilikuwa ni kichekesho jinsi suruali yake mwenyewe ilivyomuangusha na kusababisha kukamatwa. Wote tuliokuwepo tulibaki tukicheka, amesema Robbins. Mwizi huyo baada ya kukamatwa alikiri kuiba laptop ya karibu dola mia tano.
   
Loading...