tol
JF-Expert Member
- Apr 18, 2014
- 256
- 170
Leo tarehe 05/08/2018 nimeshangazwa sana na kusikitishwa na kauli iliyotolewa na aliyekuwa mbunge wa ukonga Bw mwita waitara wakati akihojiwa na Leonard Mapuli mtangazaji wa Startv Tanzania kuwa anashangaa sana kwa mh Lisu kuumia mguu wa kulia ili hali risasi zilitoka upande wa kushoto
Najua Bw waitara ni msomi na anajua ni nini anaongea na ni kwa faida ya nani. Napia anajua kwa undani kabisa ni kwa nini mh Tundu Antiphas Lissu aliumizwa mguu wa kulia ila kwa makusudi anataka kuupotosha umma na kuwafanya watanzania ni wajinga na wavivu wa kufikiri
Mbaya zaidi Mwita Waitara pia kamtuhumu driva wa lisu kuwa ndio muhusika mkuu kwa shambulio LA Lisu
Kwa faida ya wengine ni kwamba baada ya Lisu kuona watu #wasiojulikana wameshuika kwenye gari huku wameshika silaha za moto Lisu alikilaza kiti na KULALA KWA TUMBO na hiyo ndio ikawa salama yake. sasa tumuulize huyu mnafiki mwta waitara aliyejiondoa ufahamu mtu akilala kwa tumbo kwenye kiti cha mbele cha abiria mguu wa kulia utakuwa upande gani?
Itawezekana vipi Lisu aliyeumizwa amtetee adui yake aliyetaka kumuuwa?
Watanzania tuna uchungu mkubwa sana na kusikitishwa na shambulio la lisu anatokea mtu anatoa kauli za kejeli na kebehi kwenye maumivu na mateso ya mtu.. Mtu huyo lazima tutamlaani kwa nguvu zetu zote na kwa uwezo wetu wote
Kuhama chama ni utashi na uamuzi wa mtu binafsi kwa hilo hatuwezi mlaumu lakini pale anapotumia tamaa zake binafsi kupotosha umma tutasema na kumlaani kwa sauti ya juu
Njaa na tamaa yako Bw Waitara isikufanye ufikirie kwa tumbo badala ya kichwa
Mungu ibariki Tanzania........