figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,486
Mbunge Jimbo la Ukonga Mwita Waitara akifungua kongamano la wanawake BAWACHA ililofanyika Pugu Kigogofreshi ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani. Nyuma yake ni mama mzazi wa msanii wa Filamu na Miss Tanzania Wema Sepetu ambaye alijiunga na chama hicho siku kadhaa zilizopita.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara amesema hatishwi na vitendo vya Rais Magufuli kuwashambulia wabunge wa vyama vya upinzani kwenye ziara zake.
Mwita amesema kitendo cha Rais kumshambulia Mbunge wa CUF jimbo la Lindi, kimewadhalilisha wabunge wote wa upinzani na kwamba hatamvumilia iwapo atamdhalilisha jimboni kwake atapambana naye.
Kuhusiana habari za Mbunge wa Lindi, soma=> Mbunge Vedasto Ngombale (CUF) ''ahenyeshwa" na Magufuli Somanga