Mwisho wa enzi ya Lipumba ndani ya CUF

Mwisho wa enzi ya Lipumba ndani ya CUF

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,743
Reaction score
2,599
DSC_0786.JPG

Profesa Ibrahim Lipumba akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Muembe Yanga Temeke Dar es Salaam Machi 11, 2012.

======

Waswahili wanasema “Mpanda ngazi hushuka” na “kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho.” Hivyo ndivyo aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba alivyomaliza utawala wake wa miaka 27 ndani ya chama hicho.

Hata hivyo, Profesa Lipumba ameondoka madarakani bila kupenda, baada ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuagiza uchaguzi uliomrejesha madarakani Desemba 19, 2024 urudiwe, jambo ambalo hakukubaliana nalo.

Msajili alitoa agizo hilo Februari 13, 2026 baada ya kuwepo kwa malalamiko ya uchaguzi yaliyowasilishwa tangu Desemba 2024.

Sasa kwa nini malalamiko hayo hayakufanyiwa kazi tangu wakati huo, yaje yafanyiwe kazi baada ya mwaka mmoja na miezi mitatu baadaye?

Huo ndio mwisho wa Profesa Lipumba kama mwenyekiti wa CUF, kwani sasa chama hicho kimepata mwenyekiti mpya Mirambo Yusuf aliyechaguliwa Februari 22, 2026 kupitia mkutano mkuu wa dharura uliofanyika kwa agizo la Msajili wa Vyama vya Siasa.

Safari ya Profesa Lipumba ndani ya CUF imejaa furaha, mapambano, usaliti na majonzi.

Safari ya siasa

Akiwa Profesa wa uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Lipumba aliingia madarakani mwaka 1999, akimrithi Musobi Mageni aliyekuwa mwenyekiti wakati huo.

Alikuwa tumaini jipya katika chama hicho kilichokuwa miongoni mwa vyama vikubwa wakati huo.

Ilikuwa imepita miaka mine tangu ulipofanyika uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi, 1995 baada ya mfumo huo kurejeshwa, ambapo mwenyewe aligombea urais kwa mara ya kwanza kupitia chama hicho akipambana na Hayati Rais Benjamin Mkapa wakati huo.

Katika uchaguzi huo, chama kikuu cha upinzani kwa upande wa Bara kilikuwa NCCR Mageuzi na kwa Zanzibar kilikuwa CUF chini ya Maalim Seif Sharif Hamad.

Hata hivyo, NCCR Mageuzi ilipata pigo baada ya kuzuka mgogoro wa viongozi uliomhusisha aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Augustine Mrena na katibu wake mkuu, Mabere Marando, hali iliyokidhoofisha chama hicho hadi kufikia 1999, ambapo Mrema aliondoka na kujiunga na TLP.

Kwa hiyo upepo wa upinzani ukahamia CUF chini ya Profesa Lipumba. Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, CUF ilikuwa ngangari kila kona na kwa kweli CCM walipata taabu sana kupambana na chama hicho, japo chama hicho kilikuwa hakijapata nguvu kubwa upande wa Bara.
lipumba-maalim-pic-data.jpg

Katika uchaguzi huo, upande wa Zanzibar mambo yalikuwa moto, ambapo CUF waliendeleza malalamiko yao ya kudhulumiwa ushindi. Maalim Seif naye alikuwa na ushawishi mkubwa kwa Wazanzibari akawashawishi wawakilishi wateule na wabunge wateule kususia vikao.

Ikumbukwe katika uchaguzi wa mwaka 1995, Maalim Seif aliwaagiza waliokuwa wawakilishi na wabunge kususia vikao vya Baraza la wawakilishi na Bunge, mpaka yalipofanyika mazungumzo ya mwafaka chini ya aliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Madola, Chief Emeka Anyaoku.

Kwa hiyo mwaka 2000, malalamiko yale yale yakajirudia, basi safari hiyo ikawa sio kususia tu vikao, yakapangwa maandamano ya Januari 27, 2001. Japo Jeshi la Polisi liliyapiga marufuku, lakini CUF ilisisitiza yatakuwepo na yalifanyika.

Hapa Dar es Salaam, Profesa Lipumba ndiye aliyeongoza maandamano hayo kuanzia Posta ya zamani, lakini kabla hawajafika mbali, polisi waliwashambuliwa kwa mabomu ya machozi na walimkamata Profesa Lipumba na wafuasi wengine.

Kule Zanzibar, hususani kisiwa cha Pemba hali ilikuwa mbaya, kwani watu waliitikia kwa wingi kuandamana, hivyo walimbana na kipigo cha polisi. Lakini nao hawakubaki nyuma, kwani walimchinja askari polisi mmoja aliyekuwa katika kituo cha polisi cha Mkoa wa Kaskazini – Wete.

Kwa mujibu wa CUF, jumla ya watu 46 walikufa kwa kupigwa risasi, huku wengine wakijeruhiwa na wengine kubaki wajane na yatima.

Baadhi ya wananchi Kisiwani Pemba walipanda mitumbwi na kukimbilia Mombasa nchini Kenya na kuwa wakimbizi.

Pamoja na misukosuko hiyo, CUF ilizidi kuimarika na kuwa chama kikuu cha upinzani, huku kikiendelea kukita mizizi upande wa Bara.

Mwaka 2005 Jakaya Kikwete akigombea urais kwa mara ya kwanza CCM. Polisi nao hawakubaki nyuma kama kawaida yao. Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wakati huo (IGP) Omari Mahita alidai kwamba kuna shehena ya visu imeingizwa nchini na chama kimoja. Japo hakukitaja chama hicho, lakini visu vyenyewe vilikuwa na rangi za bendera ya CUF.

Mahita aliibua msamiati mwingine wa Kiswahili, akisema kama CUF ni ngangari, basi Polisi wao ni ngunguri. Yote hiyo ilionyesha kuwa CUF ndio kilikuwa chama cha upinzani chenye nguvu wakati huo.

Kikwete alishinda uchaguzi ule kwa zaidi ya asilimia 80.28, huku profesa Lipumba akipata asilimia 11.68 na aliyefuatia alikuwa Freeman Mbowe wa CHADEMA aliyepata asilimia 5.88.

Makosa ya Profesa Lipumba

Wakati hayo yakiendelea, Profesa Lipumba hakulifanyia kazi kwa makusudi kwa kwa kutojitambua, ni dhana iliyokuwa ikienezwa na CCM kwamba CUF ni chama cha kidini ndio maana viongozi wake wote wa juu ni Waislamu.

Haikushangaza chama hicho kuwa na nguvu upande wa Zanzibar na maeneo ya pwani, huku maeneo mengi ya Bara kikiwa dhaifu. Hivyo ndivyo CHADEMA walivyopata nguvu upande wa Bara.

Kosa la pili ambalo Profesa Lipumba hakulitambua au aliamua kulipuuza makusudi ni kwamba, wakati ni ukuta, ukishindana nao utaumia mwenyewe.

Ni wazi kwamba mpaka 2010, umaarufu wa Profesa Lipumba ulikuwa umepungua na hivyo alipaswa kutafuta mbinu mpya za kuendelea kulinda heshima yake ndani ya chama hicho na hata kwa kambi ya upinzani nchini.

Mwaka 2010, halikadhalika, Profesa Lipumba aligombea urais kwa mara ya nne mfululizo. Lakini wakati huu tayari CHADEMA ilikuwa imeshaanza kujimaarisha upande wa Bara na tayari ikaanza kuipita CUF.

Aliyekuwa Katibu mkuu wa CHADEMA, Dk Wilbrod Slaa alipata asilimia 27.05 dhidi ya Rais Kikwete aliyekuwa akigombea muhula wa pili akipata asilimia 62.83. Profesa Lipumba alipata asilimia 8.23.

Uhasama wake na Profesa Safari

Licha ya Profesa Lipumba kuwa na urafiki na Profesa Abdallah Safari, urafiki huo uliingia shubiri mwaka 2009 wakati wawili hao waliposhindania nafasi ya uenyekiti.

Profesa Safari aliwahi kulieleza gazeti la Mwananchi kuwa, awali alikuwa akimtetea sana Profesa Lipumba.

Ametaja kisa cha mwaka 1999, ambapo, Profesa Lipumba alitipitisha muda wa miutano wa hadhara uliofanyika Mbagala Zakheim Dar es Salaam, ndipo polisi walipomkamata na kupiga hadi kumvunja mkono.

Ameeleza jinsi alivyojitokeza kumtetea mahakamani, hadi akafukuzwa kazi serikalini.

Tatizo lilianza pale Profesa Safari alipowania nafasi ya uenyekiti wa CUF mwaka 2009, hapo ndipo vitimbi vilianza.

Profesa Safari ameeleza kuwa katika kampeni za uchaguzi huo, alifanyiwa udhalilishaji na wapambe wa Profesa Lipumba, ikiwa pamoja na kumzomea na kumuuliza maswali ya kipuuzi.

Katika uchaguzi huo, Profesa Lipumba alishinda kwa asilimia 98, akimbwaga vibaya Profesa Safari.

Baada ya hapo Profesa Safari alijitoa CUF na kuhamia CHADEMA.

Asaliti Ukawa, CUF

Mwaka 2012, Rais Kikwete alianzisha mchakato wa Mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji Joseph Warioba. Baada tume yake kutafuta maoni kwa wananchi, liliundwa Bunge Maalum la Katiba mwaka 2014, ambapo viongozi mbalimbali wa upinzani akiwamo Profesa Lipumba walihusishwa.

Katika bunge hilo, hoja mbili ikiwemo ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na hoja ya madaraka ya Rais iliwagawa wajumbe. Ndipo wapinzani wakasusia bunge hilo wakatoka nje. Vyama vilivyosusia ni pamoja na CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi na NLD. Vyama hivyo vikaanzisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Pamoja na bunge lile kutoka na rasimu ya Katiba inayopendekezwa, lakini Serikali ilisema muda hautoshi kuingia kwenye kura ya maoni, hivyo, mchakato ukawekwa pembeni, ili kujiandaa na maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Wakati huo ndani ya CCM kulikuwa na fukuto la wagombea urais na mmoja wao alikuwa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa. Katika kinyang’anyiro hicho, Lowassa alikatwa mapema tu na mchakato ulipoendelea, wakampata John Magufuli.

Kwa CHADEMA hiyo ikawa ni fursa, wakamshawishi akajiunga nao. Kwa Hiyo, chama hicho kikaviomba vyama vya UKAWA vimuunge mkono mgombea wao. Hapo ndipo utata ulipoanza.

Ndani ya CHADEMA kwenyewe, Dk Slaa aliyekuwa Katibu mkuu akapinga kupokelewa kwa Lowassa, akajitoa kabisa kwenye chama hicho. Nje ya CHADEMA, Profesa Lipumba naye akapinga, akakataa hata kuhudhuria vikao vya kumjadili Lowassa. Lakini wakati huo huo, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif akaunga mkono.

Agosti 7, 2015 Profesa Lipumba alitangaza kujivua uenyekiti wa CUF na kisha akasafiri kwenda kusikojulikana, lakini mashuhuda walisema walimwona akipanda ndege ya shirika la ndege la Rwanda Air.

Kwa hiyo chama kikabaki na Maalim Seif, ambaye aliweka makubaliano na CHADEMA, kwamba mgombea mwenza atokee CUF na ndipo akateuliwa Juma Duni Haji.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, Lowassa alileta upinzani mkali kwa CCM, ambapo licha ya kushindwa, alipata asilimia 39 ya kura nyuma ya Rais John Magufuli aliyepata Zaidi ya asilimia 58.

Wakati CHADEMA ikipata wabunge 44, kwa mara ya kwanza CUF ilipata wabunge 10 upande wa Bara.

Juni 14, 2016 Profesa Lipumba akiwa amerudi nchini, alianzisha mchakato wa kukirejea cheo chake cha uenyekiti. Akizungumzia kurejea kwake kwenye uongozi Profesa Lipumba alisema katiba ya chama cha CUF inamruhusu kwa vile barua yake ya kujiuzulu aliyoandika kwa katibu mkuu na kwa baraza la uongozi la chama hazikujibiwa mpaka sasa anapochukua uamuzi huo na hivyo baada ya kuombwa na watu mbalimbali ameamua kurejea kwenye uongozi wake.

Licha ya suala hilo kupingwa na upande wa aliyekuwa Katibu Mkuu, Maalim Seif, lakini Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ilibariki kurejea kwa Profesa Lipumba.

Suala hilo liliibua mgogoro kati ya upande wa Mwenyekiti Profesa Lipumba na upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif. Kama hiyo haitoshi, Kundi la Maalim Seif lililokuwa na watu wengi kutoka Zanzibar lilipinga uamuzi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kumtambua Profesa Lipumba, wakafungua kesi.

Hata hivyo, upande wa Maalim Seif ulishindwa kwenye kesi hiyo, ambapo Mahakama Kuu ilimtambua Profesa Lipumba kama mwenyekiti.

Machi 18, 2029 Maalim Seif alitangaza kujitoa CUF na kujiunga chama cha ACT Wazalendo. Licha ya Profesa Lipumba kushinda katika sakata hilo, lakini uamuzi wa Maalim Seif na kundi lake kujitoa kwenye chama hicho, kulikidhoofisha hasa upande wa Zanzibar.

Anguko la Profesa Lipumba

Kama ilivyotarajiwa, katika uchaguzi wa Desemba 2024 ambao Profesa alikuwa akigombea mara ya sita mfululizo kama mwenyekiti wa CUF, alishinda kwa kupata kura 216.

Lakini ushindi huo ulikuwa umeshuka mno, kwani kura hizo zilikuwa sawa na asilimia 36, wakati kanuni za uchaguzi zinamtaka ashinde kwa zaidi ya asilimia 50.

Kilichofanyika ni kulishawishi Baraza Kuu la Uongozi kubadilisha kanuni na kutengua kifungu kinacholazimisha ushindi wa asilimia 50, ndipo akashinda.

Aliyemfuatia kwa kura alikuwa Hamad Masoud aliyepata kura 181, huku aliyekuwa Makamu mwenyekiti wa CUF bara, Maftah Nachuma (sasa amehamia ACT Wazalendo) ndiye akipata kura 102 na Wilfred Rwakatare akipata 78.

Hata hivyo baadhi ya wagombea walipeleka malalamiko kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa tangu Desemba 2024, lakini hayakufanyiwa kazi hadi Februari 2026, Msajili alipokitaka chama hicho kurudia uchaguzi huo baada ya kukubaliana na hoja za walalamikaji.

Kulikuwa na juhudi za kundi la Profesa Lipumba kutaka kuzuia uchaguzi huo kwa kufungua kesi mahakamani, lakini njia hiyo ilikwama.

Februari 20, 2026 liliitishwa Baraza Kuu a Uongozi na kupitisha majina matatu ya wagombea akiwamo aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Tanzania Bara, Othman Omar Dunga, Mirambo Camil Yusuf na Nkunyunyika Siwale.

Usiku wa kuamkia Februari 22, Mkutano mkuu wa dharura ukamchagua Mirambo kuwa Mwenyekiti kwa kura 257 akiwashinda Othman Omar Dunga aliyepata kura , 177 na Nkunyunyika Siwale, aliyepata kura 6.

Kilichomponza

Kama wanavyosema Waswahili, ukila na kipofu usimshike mkono, kuna kila dalili kwamba Msajili wa Vyama Vya siasa alimezea mate matokeo yaliyomweka madarakani Profesa Lipumba Oktoba, lakini mwenyewe akajisahau akaanza kuchokoza mbwa aliyelala.

Novemba 5, 2025 Profesa Lipumba alikuwa kiongozi wa kwanza wa upinzani aliyelalamikia uchaguzi wa Oktoba 29, 2025 akihoji ushindi wa Rais Samia Suluhu Hassan, akisema uhsindi wa asilimia 97.6 ni mkubwa ambao haujawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini.

"Matokeo yaliyotangazwa hayawakilishi uhalisia wa kura zilizopigwa, ni matokeo ya kupikwa yamevunja misingi ya haki, uwazi na uhalali wa kidemokrasia serikali imepoteza kabisa imani kwa wananchi ndani na nje ya nchi," alisema Profesa Lipumba katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam.

Kama hiyo haitoshi Januari 27, 2026 katika maadhimisho ya miaka 25 ya Kumbukizi ya Mauaji ya Wanachama wa CUF Zanzibar yaliyotokea Januari 27, 2001 jijini Dar es Salaam, Profesa Lipumba alikosoa uchaguzi wa Oktoba 29, 2025.

“Mwaka jana 2025 matukio mengine makubwa ya watu kuuliwa na vyombo vya Dola yalitokea, tena yametokea siku ya uchaguzi wenywe; na bila haya, tume ikaeleza kwamba kati ya wapiga kura waliomo ndani ya Daftari kama 37 milioni Zaidi ya milioni 32 walijitokeza kupiga kura, jambo ambalo ni uongo.

“Inatisha wakati majaji wa Mahakama Kuu kwa shinikizo la CCM wanaeleza uongo wa wazi na mama Samia (Suluhu Hassan) anarejea anasema anaishukuru Tume ya uchaguzi kwa kuwa na weledi wa hali ya juu, watu wakajitokeza kwa wingi wakapiga kura haraka haraka, ilipofika saa 5 wote wameshamaliza kupiga kura hata yale machafuko yalipoanza tayari wameshapiga kura,” alisema Profesa Lipumba.
 
Attachments

  • lipumba-pic-data.jpg
    lipumba-pic-data.jpg
    77.2 KB · Views: 3
Kongole kwake kwa kustaafishwa kwa lazima na kwa fedheha:1Head:
 
View attachment 3547614

View attachment 3547613

Ukiwa sii kubebwa na chama kilicho asisi vyama mamluki angepotea tangy enzi za kufarakana na Maalim Seif a.k.a enzi za Mzee ya buguruni!
 
Back
Top Bottom