Mwisho wa Daudi Ballali

Upuuzi mtupu tutafanyana wajinga hadi lini?
Kwani kuwepo kwa kaburi lililoandikwa Ballali haimaanishi aliyezikwa humo ni yeye, kwa hili mnatufanya tuhisi kuna uchafu mwingi alifanya ambao serikari imeukalia . imeendelea
 
Muda ukiwadia ykweli utajizithiirisha tu.
Kwani kwa teknolojia iliyopo sasa ni jambo dogo sana kuweza kuthibitisha kama ndiye yeye balali au la aliyezikwa kwa kuchukua na kupima sampuli ya mabaki ya mwili wa marehemu hata kama ni mifupa tu ndio iliyosalia.
 
Waishio nje wakifia huko huwa miili yao inasafirishwa kuja kuzikwa nyumbani, au hata kama watazikwa huko, basi huwa hakunaga usiri kwenye mazishi na taratibu zake, toka mwanzo hadi mwisho... SEMBUSE GAVANA WA BoT.... Pelekeni hukooo uwongo wenu..

Mficheni tu, ila mjuwe huko aliko atazeeka na SIKU MOJA NAFSI ITAMSUTA NA ATAYASEMA YOTE.... time will tell

Some people think that the truth can be hidden with a little cover-up and decoration. But as time goes by, what is true is revealed, and what is fake fades away.
By Ismail Haniyeh
 
Yaani uwepo wa kaburi ndiyo uthibitisho wa kifo? Bado mimi siamini. Yawezekana kabisa kaeneo kalinunuliwa na kujengwa kinachoonekana hapo.Na mambo mengine yanaendelea.Kiukweli,suala la Balali lina maswali mengi kuliko majibu.

Hivi watanzania lini tutaacha kuwa watu wa ajabu .... mmeambiwa mtu kafa maana yake amekufa. Marekani hakuna shortcuts za kijinga na usanii kama Tanzania ... eti ooh kumejengewa jina tu, tutajuaje aliyezikwa hapo ni yeye, kwa nini azikwa marekani, etc ..... Kwa kifupi waulizeni ndugu au marafiki zenu walioko marekani ni nini kinatokea mtu akifa, hata kifo cha kawaida hampati mwili mpaka uchunguzi ufanyike. Maziko yenyewe si bei rahisi ndio maana kuna watu wanachomwa moto kwa kushindwa kupata gharama za maziko. Wageni wengi tu huzikwa marekani kwa hiyo Balali hakuwa wa kwanza na wala hatakua wa mwisho kuzikwa marekani! labda ndio yalikua maamuzi yake na mke wake. kwenye maamuzi kama hayo ya maziko Marekani anasikilizwa mtu mwenye power of attorney, kwa hiyo hata mje jumuia nzima tunataka kwenda mzika Tanzania lakini mke wake akaamua azikwe marekani maana yake ni atazikwa marekani...mke wake angesema achomwe moto, angechomwa moto. MAREKANI HUENDESHWA KWA SHERIA HAKUNA SHORTCUTS ZISIZO NA CONSEQUENCES!
 

Unywele tu unatosha kuthibitisha
 

No comment
 
Alikimbia moto wa Dr.Slaa na Tundu Lissu.
 
Mmenikumbusha maigizo ambayo Mtuanakufa kesho unamwona mitaani uku kukiwa na maandishi alizaliwa lini na alikufa lini.
Hawa maigizo yamefadhiliwa na serikali na kuigizwa na Gazeti Mwananchi.
Wahusika CCM na Matajiri wa EPA
 
Maswali ni mengi....





Siku ya tatu, Mwandishi wa Mwananchi alilazimika kuomba msaada wa Ofisi ya Makaburi ya Gate of Heaven, ambayo ilimsadia kuonyesha eneo lilipo kaburi hilo, hivyo kuwezesha kupata picha zake.

Kaburi lake liko katika msitari wa mwisho kabisa na Ukanda wa Kijani wa miti iliyozunguka
makaburi ya Gate of Heaven,"

mbona kwenye picha kwenye kaburi moja tu, au ballali ndio mtu wa mwisho kuzikwa hapo.
nmepata mashaka sana na uhandishi wako unaobase upande mmoja ,halafu unauita wa kichunguzi.

yaani hata ndugu wa ballali hawajui kaburi la ndugu wao lilipo.
sorry hivi nauli ya kwenda huko alikulipia nani .?
 
Seriously?
Yan umeenda USA kutazama kaburi?
Halafu umeridhika kwamba aliyemo ndan ni Balal?
 
Nafurahi hii 'issue' kuibuliwa tena tunapoelekea 2015. Kama ilikuwa imesahaurika vile wakati halikuwa tukio la kawaida nchini. Mtatujibu vizuri ni kwa nini kifo chake mlikifanya usiri mkubwa....
 
Siku moja Serikali Makini itafukua mwili wa huyo anayehisiwa kuwa ni Ballali na kuufanyia DNA test, ili kutendea haki waTanzania na kuridhisha umma wa walipa kodi, as part of good governance. Huyu jamaa "alikufa" akiwa alleged kuwa criminal, kama wataruhusu fununu na bla bla hizi ziendelee, they are setting a very bad precedence!
 
Kwamba mtu aliyekuwa na hadhi ya Gavana wa Benki Kuu anafariki Marekani halafu hata maofisa wa Ubalozi wetu,wawakilishi wetu katika mashirika makubwa ya kifedha yaliyoko US wote wanashindwa kuhudhuria hata kwa uchache wao?
Hata mchawi hakosi mtu wa kumzika na kuwadhibitishia watu kuwa huyo mtu kafa na kuzikwa.
Mwandishi kutueleza kaona kaburi limeandikwa jina eti ndio anakuja kutuambia ni habari za uchunguzi? Basi angeanzia uchunguzi wake katika historia ya matibabu,daktari aliye saini hati ya kifo na mengineyo angeonyesha kweli kafanya kazi.
Watu wangapi wanaokotwa wamekufa na majina yao hayafahamiki? Akizikwa na mkaamua kulipa jina hilo kaburi mfano MSALANI bin so and so hivyo itakuwa yule aliyepo humo ni huyo mwenye jina wakati MSALANI yupo Lumumba anaendelea kutupia post JF na anavuta mpango wake wa buk7 bila wasiwasi?


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mie nasubiri Mzee Mamvi wamnyime kuwakilisha Ccm ktk nafasi ya urais ili amlete Ballali make anajua aliko!!
 
Upuuzi mtupu tutafanyana wajinga hadi lini?
Kwani kuwepo kwa kaburi lililoandikwa Ballali haimaanishi aliyezikwa humo ni yeye, kwa hili mnatufanya tuhisi kuna uchafu mwingi alifanya ambao serikari imeukalia . imeendelea

Kama unajua alipo toa taarifa mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…