GE2025 Mwinyi: Wakulima msiwe na wasiwasi wa soko

GE2025 Mwinyi: Wakulima msiwe na wasiwasi wa soko

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Mgombea wa urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema serikali itaendelea kutekeleza mikakati ya kuinua sekta ya kilimo kwa kujenga skimu mpya za umwagiliaji, kuongeza upatikanaji wa zana za kisasa, na kujenga maghala ya kuhifadhia mazao ili kudhibiti bei ya mchele nchini.

Akizungumza na wakulima wa mpunga, mwani na wavuvi katika uwanja wa Marumbi, wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, Dk. Mwinyi amesema serikali inatambua changamoto zinazowakabili wakulima wa mpunga, ikiwemo uhaba wa zana za kilimo na pembejeo, na kwamba hatua madhubuti zimeanza kuchukuliwa ili kuboresha sekta hiyo.

“Serikali inaendelea kuhakikisha tunapanua skimu za umwagiliaji ili kuongeza uzalishaji wa mpunga. Tunajua tunahitaji zana za kisasa, na ahadi yetu ni kuleta matrekta makubwa, ‘powertillers’, pamoja na mashine za kuvunia. Vifaa hivyo vitasaidia kuongeza tija na kupunguza gharama za uzalishaji,” amesema Dk. Mwinyi.

Soma pia: Dkt. Mwinyi: Miaka 5 ijayo tutajenga soko kubwa Kinyasini

 
Back
Top Bottom