Mwinjilisti apinga maaskofu kuhusu siku ya uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwinjilisti apinga maaskofu kuhusu siku ya uchaguzi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, May 28, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  MWINJILISTI wa Kanisa la Penuel Healing Ministry, Alphonce Temba amewataka wachungaji na maaskofu kuacha kushinikiza kubadilishwa kwa siku ya kupiga kura na badala yake kuwataka watumie siku hiyo kuliombea taifa na kupiga kura.

  Jumanne iliyopita Jukwaa la Wakristo Tanzania liliiomba serikali kubadilisha siku ya uchaguzi kutoka Jumapili hadi siku nyingine ya katikati ya wiki, likieleza kuwa Jumapili ni siku ya kuabudu na hivyo isitumiwe kuamua mustakabali wa nchi.

  Jukwaa hilo ni chombo kipya kinachoundwa na Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec), Baraza la Maaskofu wa Pentekoste( PCT) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), ambayo inahusisha makanisa ya Kiprotestanti.
  Lakini Mwinjilisti Temba alisema haoni sababu ya viongozi wa chombo hicho kuanza kuhamasishana kuipinga siku ya Jumapili, akisema kila siku ni siku ya kuabudu kwa kila aliye hai.
  Alisema viongozi hao walipaswa kuwahimiza waumini wao wajiandikishe kabla na kisha waitumie siku ya Jumapili ya uchaguzi kufanya maombi maalumu, ili taifa liondokane na majanga na baadaye wapige kura kama watu walio na upako.

  "Sioni kama kuna tatizo, sioni kwa sababu kila aliye hai, ni lazima amche Mwenyezi Mungu kila siku... na Jumapili imetengwa rasmi kwa ajili ya wote tuwe ndani ya ibada," alisema mwinjilisti huyo ambaye kanisa lake lipo Ubungo Kibangu.
  "Kwa maoni yangu kama Mungu anasema mamlaka zote ameziweka yeye na tusizipinge, basi tungetumia hiyo siku ya Jumapili kufanya maombi maalumu na ibada ihusu uchaguzi halafu tukaenda kupiga kura," alisema.
  "Kama wachungaji, maaskofu na wainjilisti wangeweza kufanya maombi nchi nzima; wakaliombea taifa kwa ajili ya uchaguzi na baada ya hapo wakaenda kupiga kura, wasingepoteza lolote.
  "Mwaka 2006 nilienda DRC ambako kulikuwa kunafanyika uchaguzi mkuu kwa mara ya kwanza wa kidemokrasia na kulikuwa na hofu nyingi sana, lakini nchi nzima ilihamasishwa na walifanya ibada kuanzia asubuhi mpaka saa 4:00... ibada ilikuwa maalumu kwa ajili ya kuombea uchaguzi; kuombea taifa liwe na amani na baadaye watu wakaenda kupiga kura.
  "Ni siku nzuri kwa sababu tunataka majanga mbalimbali kama udanganyifu yaondoke."
  Juzi mwinjilisti huyo alimtembelea Rais Jakaya Kikwete kwenye Ikulu ndogo ya mjini Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kumtia moyo wakati huu ambao uchaguzi mkuu unakaribia.
  "Nilifanya hivyo sababu kama mtumishi wa Mungu, kamisheni yangu mimi ni kufanya maombi kwenye jambo lolote lile. Sisi ni watu tunaopeleka matatizo ya waumini kwa Mungu kwa kuwa Biblia inazungumza wazi katika Warumi 13:13," alisema akifafanua kuwa Wakristo wote wanapaswa kuzitii mamlaka kuu za nchi kwa kuwa zimewekwa na Mungu.
  "Mwaka 2005 tulifanya naye maombi na magazeti yaliandika kwamba ni chaguo la Mungu na nisingeweza kuacha kurudi tena," alisema.

  Mwinjilisti apinga maaskofu kuhusu siku ya uchaguzi
   
 2. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  hpo kwenye nyekundu nafikiri panatosha kumjibu huyu Mwinjilisti kuwa hicho ndio wanachokitaka Maaskofu hao kifanyike kuwa siku hii iwe huru kwa maombi tu na sio biashara nyingine. Na nilichopenda mimi ni kuwa Maaskofu hawa wamependekeza iwe kati ya Jumatatu-Alhamisi? Unajua kwanini?
   
 3. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  NEC yang'ang'ana na Jumapili Send to a friend
  Saturday, 29 May 2010 09:14
  0diggsdigg
  Hussein Kauli
  TUME ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema haitabadili siku ya kupiga kura kutoka Jumapili hadi siku nyingine ya katikati ya wiki, ikidai kuwa imekuwa ni utamaduni uchaguzi mkuu kufanyika Jumapili.

  Nec imetoa majibu hayo siku mbili baada ya chombo kipya kinachokutanisha viongozi wa madhehebu ya Kikristo, Jukwaa la Wakristo, kupendekeza kuwa uchaguzi mkuu uhamishiwe siku nyingine kwa kuwa Jumapili ni siku ya kuabudu. Uchaguzi mkuu umepangwa kufanyika Oktoba 31, ambayo itakuwa ni Jumapili ya mwisho wa mwezi ambayo kwa kawaida hutumiwa kupiga kura katika mwaka wa uchaguzi.

  Katika taarifa iliyotolewa jana na Nec na kusainiwa na mkurugenzi wa uchaguzi, Rajabu Kiravu, kabla ya kuamua siku ya Jumapili kuwa ya kupiga kura, walipata maoni kutoka kwa wadau. "Aidha, tume imezingatia utamaduni uliojengeka kwa muda mrefu wa kupiga kura siku ya Jumapili ya mwisho ya mwezi Oktoba wa mwaka wa uchaguzi," inasema taarifa hiyo.

  Taarifa hiyo inaendelea kueleza kuwa tangu uhuru, uchaguzi mkuu umekuwa ukifanyika siku ya Jumapili, isipokuwa mwaka 2005 wakati tume hiyo ilipolazimika kuahirisha uchaguzi kutokana na kifo cha mmoja wa wagombea wa nafasi ya makamu wa rais.

  Aliongeza kuwa kwa wakati wote huo, wapiga kura waliweza kutumia fursa hiyo kupia kura bila ya kuwepo matatizo. "Kwa kawaida vituo vya kupiga hufunguliwa kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni, hivyo mpiga kura anaweza kuweka utaratibu wa wakati gani atakwenda kupiga kura katika siku hiyo," inasema taarifa hiyo.

  Taarifa hiyo ilifafanua kuwa katika mkutano wa viongozi wa dini wa Mei 13 hadi 14 mwaka huu, suala hilo lilijadiliwa kwa kirefu kufikiwa makubaliano. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, makubaliano yaliyofikiwa ni kuwa katika uchaguzi mkuu ujao, ratiba iliyotangazwa na Nec itaendelea kama ilivyopangwa.
   
 4. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  tunatakiwa kwenda kupiga kura tu, hamna shida. hatubishani, na huwa hatuna desturi ya kugombana. so this is not a problem for us christians..labda ingekuwa kwa watu wengine ndo wangeshaanza kuandamana. tutavunja tu siku hiyo ya ibada, na tutapiga kura kwa moyo mmoja dhidi ya chama fulani hivi....sitaki kukitaja jina...kinajijua chenyewe...
   
 5. P

  Paul S.S Verified User

  #5
  May 31, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kama nec wemeona nivyema kwa siku hiyo ni sawa tutaangalia jinsi ya ku balance muda. amani maridhiano upendo kuvumiliana daima ndio utamaduni wetu
   
 6. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  :brushteeth:hata mimi sioni shida hiyo siku ya j.Pili kupiga kura. Kwanza pengine inasaidia kuwabadilisha watu mioyo maana wanakuwa wametoka kusali na kutubu huenda ndio wakafanya uamuzi sahihi. maana wenye hasira zao zinakuwa zimepoa, wenye viburi wanakuwa wamevisahau kwa Muda na wenye fitina wanamua kuziacha na wenye huruma wanakuwa na huruma kwa sababu wanakuwa wametoka kusali na wengine wanakuwa wanafikiria kwenda kusali so hawawezi kufanya mambo ya ajabu ya uhatarisha amani.
   
 7. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,856
  Likes Received: 2,017
  Trophy Points: 280
  Sure, majadiliano sio kufarakana ila kupatana hata kama hamkukubaliana
   
 8. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hata mimi nafikiri jpili ni siku nzuri ya kuwaadhibu hawa mafisadi
   
Loading...