Ukweli utabaki kuwa ukweli daima Vijana wengi wanaoingia kwenye siasa Tanzania ya leo wanaweka mbele maslahi binafsi na si masilahi ya Taifa la Tanzania,vijana wengi walioko ccm na vyama vingine wanawaza na kuthamini maslahi yao kwanza nchi baadae.Nchi haiwezi kwenda namna hii.vijana tujirekebishe itafikia hatua wanainchi wanaotudhamini watatudharau na kututupa.Leo nje ya wigo anaamka anazungumza jambo kwa kulipinga kweli kweli kesho akiwa ndani ya wigo wa kula hilohilo analikubali tena kwa mbwembwe kubwa liendelee eti kwa sababu naye leo ni sehemu ya ulaji jamani tuache unafiki.daima tuweke mbele maslahi ya taifa badala ya maslahi ya matumbo yetu.huu usaka tonge vijana unatuharibu.imefika pahala vijana leo hawajulikani wanasimamia nini awe ccm,cdm au cuf,tafadhali wajameni fijana tubadilikage nye vaa.