Muke Ya Muzungu
JF-Expert Member
- Jun 17, 2009
- 3,444
- 265
ASKARI wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA), wanatuhumiwa kumpiga na kumsababishia kifo, Musa Amiri Lihonga, Mkazi wa Mbezi-Makabe, jijini Dar es Salaam, katika msitu wa Mambwepande.Tukio hilo linadaiwa kutokea Januari 5, mwaka huu, baada ya askari hao wa TANAPA kumkuta Musa Amiri Lihonga akiokota kuni katika msitu huo.
Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu aliyejitambulisha kuwa ni Abdul Lihonga, siku ya tukio, ndugu yao alikwenda kutafuta kuni lakini alikamatwa na askari wa Tanapa, wakamtuhumu kuwa anachoma mkaa. Alisema baada ya kumkamata, walikwenda nyumbani kwa marehemu kupekua lakini hawakukuta mkaa zaidi ya kiasi kidogo tu kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na kumpeleka kituo cha polisi Mbezi.
Ndugu huyo alisema mara tu baada ya kufikishwa polisi, ndugu yao alianza kuugulia maumivu makali, ikidaiwa ni matokeo ya kipigo alichokipata kutoka kwa askari wa Tanapa, walipomkamata msituni Mabwepande.
Hali ya marehemu ilizidi kuwa mbaya, jambo lililowafanya polisi kumpeleka katika Hospitali ya Mwananyala na kulazwa wodi namba 5, lakini siku moja baadaye alifariki. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela alipohojiwa juu ya jambo hili aliomba muda aweze kufuatilia na kulitolea ufafanuzi.
Hata hivyo, uchunguzi wa Tanzania Daima Jumamosi, umebaini kuwa askari watatu wa Tanapa wanashikiliwa kuhusu tukio la kifo hicho.