Elections 2010 Mwingine afa ktk uchaguzi 2010

Mutu

JF-Expert Member
Mar 30, 2008
1,329
47
Ndeninsia Lisley (RCT)

WAKATI zikiwa zimesalia siku nne kabla ya uchaguzi mkuu, imedaiwa kuwa mtu anayetuhumiwa kufanya vurugu kwenye kampeni za CCM, jimbo la Kawe amefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi.

Kifo hicho cha Alfred Mushi, 35, kilichothibitishwa na Jeshi la Polisi kilitokea juzi wakati mtuhumiwa huyo akiwa mikononi mwa polisi na awali ilidaiwa kuwa baada ya kufanya fujo katika kampeni hizo za udiwani na ubunge za CCM, alikamatwa na kufikishwa katika kituo kidogo cha polisi cha Tegeta kabla ya mauti kumkuta.


Kamanda wa polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Suleimani Kova alithibitisha kutokea kwa kifo hicho akikielezea kuwa ni cha kutatanisha na kudai kuwa baada ya taarifa hiyo kutolewa kwa uongozi wa polisi wilaya ya Kawe, jalada la kifo hicho lilifunguliwa na uchunguzi kuanza mara moja ili kubaini chanzo halisi.


Alisema taarifa walizonazo ni kwamba Mushi alikuwa akijibamiza kichwa ukutani na kupiga mahabusu wengine wakati akiwa kituo kidogo cha polisi cha Kawe ambako alipelekwa na mgambo aliyemkamata na kwamba alikataa kula chakula alicholetewa na ndugu zake.


Kova aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mtuhumiwa huyo alikumbwa na mauti hayo akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa matibabu baada ya hali yake kuwa mbaya na kwamba amri ya kumpeleka hospitali ilitolewa na kamanda wa polisi na mkuu wa upelelezi wa wilaya hiyo baada ya ya hali yake kuonekana kuwa mbaya.


Kamanda Kova alisema kuwa Mushi alikamatwa Agosti 21 majira ya saa 10:00 jioni akiwa stendi ya mabasi Tegeta ambako kulikuwa na mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa udiwani wa CCM.


Kwa mujibu wa Kamanda Kova, uchunguzi wa awali ulibaini kuwa Mushi alikamatwa na mgambo aliyemtaja kwa jina la Mohamed Manjolo ambaye alipewa taarifa kuwa mtu huyo alikuwa anafanya vurugu kwenye mkutano wa kampeni.


Alidai kuwa Manjolo aliwaeleza kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na wenzake ambao walitoroka. Alisema watu hao walikuwa wakitoa lugha za matusi na kurusha mawe kwa watu waliohudhuria mkutano huo na kwamba alionekana mlevi, hivyo walimkamata na kumfikisha kituo cha polisi.


Kova alidai kuwa Mushi alikuwa akiwapiga mahabusu wengine wakati akiwa kituoni licha ya kuonekana mlevi.


"Alikuwa akijibamiza kichwa na mwili wake kwenye ukuta ndani ya chumba cha mahabusu," alisisitiza Kamanda Kova.


Alisema kutokana na vurugu hizo askari waliamua kumfunga pingu ili asiwadhuru wengine.


"Hata hivyo, mtuhumiwa huyo alijifungua pingu hiyo mkono mmoja, lakini mahabusu wenzake kwa kushirikiana na askari walimfunga mtuhumiwa huyo mikono," alisema Kova.


Alisema kutokana na hali hiyo mtuhumiwa huyo hakuweza kuchukuliwa maelezo kwa mategemeo kuwa angetulia baadaye na maelezo yake kuandikwa.


Kwa mujibu wa Kamanda Kova, mahabusu wenzake walidai kuwa Mushi alikataa chakula alichopelekewa na ndugu zake.


mwelezea mtuhumiwa huyo kuwa licha ya vurugu alizokuwa akifanya ndani ya mahabusu za kujibamiza kichwa ukutani, kujifungua pingu na kumng'ata mmoja wa mahabusu kidole cha mguu wa kulia cha mwisho lakini pia alikataa hata kula chakula alicholetewa na ndugu yake.


source: http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/5917-mtuhumiwa-wa-vurugu-kampeni-afia-mikononi-mwa-polisi
 
Kwa maana nyingine maelezo ya polisi ni kuwa huyo bwana kajisababishia kifo kama kajiua.

Ngumu kuamini ila kwa sababu ya kudumisha amani I give it benefit of doubt
 
Ni muhimu iundwe kamati huru ya kuchunguza kifo hicho. Mtuhumiwa kufia mikononi mwa Polisi si jambo dogo. Lazima waulizwe mahabusu waliokuwepo, na uchunguzi kamili wa kuangalia kuanzia mazingira ya kukamatwa hadi kufa kwake ufanyike.
 
Itakuwa polisi wenyewe wamemuua na wanajaribu kutafuta visingizio.Hapa inabidi tume huru ichunguze vinginevyo tutaamini ya kuwa ,ni polisi ndiyo waliyomuua.
 
Ni muhimu iundwe kamati huru ya kuchunguza kifo hicho. Mtuhumiwa kufia mikononi mwa Polisi si jambo dogo. Lazima waulizwe mahabusu waliokuwepo, na uchunguzi kamili wa kuangalia kuanzia mazingira ya kukamatwa hadi kufa kwake ufanyike.
siungi mkono kamati huru wala tume... hazijawahi kuleta tija kwani taarifa zo either ni za kupika au hata zikiwa kweli hakuna kinachofanyika

ili haki iwe recognised, sacrificekama za mushi ni lazima
 
Polisi nendeni sasa mkamkate mgombea ubunge wa ccm kwa sababu zilezile mlizotumia kwa shibuda kwamba
anaweza kuwa anahusika kwa maana waliousika kumpiga marehemu ni wananchama wake wa ccm. Polisi na hasa
manumba ambaye alikimbilia maswa harakaharaka aje na hapa sasa na atangaze kuwa mtu huyu alipigwa na
wafuasi wa ccm kabla ya kupelekwa polisi.
 
Kamanda Kova ni vigumu sana kuamini jeshi letu la polisi kwa sababu matukio kama hayo ni ya kawaida kwenu. CCM through Green Guards wameingilia sana kampeni za vyama vingine lakini polisi hawakuchukua hatua. Are you really Civil Servants au ninyi ni watumishi wa CCM? What a shameful police force!!
 
Hata Ditopile alipoua Tibaigana alisema alikuwa anagongagonga kioo cha gari ndo risasi ikafyatuka na kuua. Kova huaminiki!!
 
Utaficha ukweli wa mambo kwa mwanadamu lakini Mungu huona ukweli uko wapi, inaonyesha huyu Bwana kakerwa na kampeni ya chichiem hadi kukamatwa kwake. Kufa mikononi mwa polisi lazima watoe hesabu hiyo........
 
Yaani hata punguwani akisoma hayo maelezo ya kova utagundua kuwa ni usani mtupu....Mlevi aweze kujifungua pigu!?, alikuwa anapiga mahabusu!?, wengine halafu waka mfunga pigu nini kitatokea kama tuko mahabusu unanipiga halafu ukaja ukafungwa pigu...Kova iko siku ukweli tutaupata na si siku nyingi
 
Back
Top Bottom