Mwingine adakwa kwa kumkashifu Rais Magufuli kwenye mtandao wa "WhatsApp"

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
Sheria ya Makosa ya Kimtandao inaendelea kushika kasi, mwingine tena aingia matatani baada ya kubainika kutumia Lugha mbaya dhidi ya Rais kwenye mtandao wa WhatsApp.

Hapa cha muhimu ni kujuwa sheria hii inafanya kazi, inakamata, inahukumu na kufunga wananchi. Tutumie lugha ya staha, vijana hamko salama kwenye fb, twitter na WhatsApp...sheria ya mitandao ipo na inazunguka kama Simba aungurumae akitafuta mawindo.
=========

Leonard Mulokozi Kyaruzi amefunguliwa mashtaka kwa kumkashifu Rais John Pombe Magufuli kupitia mtandao wa WhatsApp tarehe 2 Juni 2016.

Kyaruzi anatuhumiwa kutenda kosa hilo akiwa jengo la Tanzanite jijini Dar es Salaam ambapo aliandika "Hivi huyu Pombe ni kwamba hana washauri? Hashauriki? Au ni zuzu? Bwege sana huyu jamaa, he doesn't consider the law in place before opening his mouth!. Au na yeye anaumwa ugonjwa wa Mnyika?" Ilisema sehemu ya hati ya mashtaka.
Barua.jpg


Hukumu yatolewa, habari zaidi soma=>Makosa ya Mtandao: Mwanasheria Leonard Mulokozi Kyaruzi apatikana na hatia kumkashifu Rais Magufuli
 
Hivi hiyo sheria ni kwa wanaomdhihaki JPM pekee? Mbona tunashuhudia wanasiasa na watu wakawaida wengi tuu wakitukanwa lakini hakuna hata zinachukuliwa? Nani hajaona matusi anayopewa Eddo mitandaoni na watu wanaofahamika? Mbowe, Slaa, Nape nk?
Kumbe ilitungwa kwa ajili ya mtu mmoja tuu
 
Jaman kuandika jina au kutoandika haisaidii kujificha kama utaenda mrama na kwenye ujumbe wa kukashifu au kutukana tukifanya ufuatiliaji wa sms zetu tunaona kila kitu kuhusu usajili wa namba cha msingi tujitahidi kuandika kiungwana na kama una hasira tulia kwanza pamoja tuzingatie sheria hata kama zinatubana tumezipitisha na Zina fanya kazi
 
Hivi wakitaka kutudaka na sisi hapa jf wanaanzia kwa mods Kwanza ili wajue majina halisi, maana hapa Facebook twitter na whatsapp ndio wanadakwa sana ina maana humu watu wastaarabu sana?
JF full fake hakuna mwenye Jina Lake humu
Kifaa unachotumia katika kupost maneno yako kina utambulisho maalum ndiyo maana kwa sasa simu zinatakiwa kuwa registered na pia kinaonyesha sehemu uliyokuwa wakati unapost kwenye mtandao.

Kwa sasa jeshi la polisi liko mbioni kuboresha zaidi huduma zake kiasi kwamba hata ukipiga tu polisi emergency number bila kuongea, polisi watakuja haraka sehemu ambayo namba hiyo ilipigwa.

Ukitumia computer pia itafahamika sehemu ambayo maneno uliyopost yametokea kwa sababu kila computer ina unique identification na sehemu/eneo ilipo.

Kumbuka hata kama utafuta maneno uliyopost utakuwa unapoteza muda kwa sababu yatakuwa bado yapo ndani ya simu au computer internal hard drive kama polisi wataipekuwa simu yako au komputa yako.

Cha muhimu ni kujaribu kutovunja sheria hata kama sheria ni kandamizi.

Jamiiforums moderators wanajitahidi sana kufuta maandishi yenye matusi kwa faida ya mtu aliyeandika tusi/matusi.
 
Back
Top Bottom