Mwingereza mmoja, awauzia hewa safi Wachina

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485

Maeneo mengi ya Uchina, hasa miji mikubwa, yamekuwa yakitatizwa na uchafuzi wa hewa. Hili limekuwa faraja kwa Mwingereza mmoja ambaye ameanza kuuza hewa safi huko.

Leo De Watts, 27, hutoa hewa yake maeneo ya mashambani Uingereza ambayo hayajachafuliwa, kuipakia kwenye chupa na kuisafirisha hadi miji ya Shanghai na Beijing.
Huko huwauzia matajiri hewa hiyo.

Chupa moja ya hewa safi ya mililita 580 huwa anauza £80 ($115).

Ameanzisha kampuni kwa jina Aethaer na hutoa hewa yake maeneo yenye upepo mwingi ya Dorset, Somerset, na Wales.

Anasema baadhi ya wateja hutaka hewa ya kiwango fulani na wakati mwingine humbidi kutoa hewa maeneo ya milima, na wakati mwingine bondeni ili kupata aina ya hewa inayohitajika na wateja.

"Linaonekana kama wazo la kushangaza sana kwetu hapa Uingereza kwa sababu tuna hewa safi. Hapa mtu anayeishi karibu na ziwa akianza kupakia hewa safi kwenye mikebe na kuuza, marafiki zake watadhani amerukwa na akili,” alisema Bw Watts alipohojiwa na Stephen Nolan wa BBC 5 Live.

“Lakini huko hakuna hewa safi na inathaminiwa sana.”

Viwango vya uchafuzi wa hewa Uchina vilifikia viwango vya juu sana hasa mwezi Desemba, na katika baadhi ya maeneo kusababisha shule kufungwa.

Li Tianqin ni mmoja wa walionunua mkebe wa hewa safi kutoka Rocky Mountains, nchini Canada.

Kampuni ya Vitality Air, inayovuna hewa hiyo Rocky Mountains, imekuwa ikiuza mkebe mmoja wa hewa kwa kati ya $14 na $20.

Chanzo: BBC
 
Nakumbuka Taiwan tulikuwa tunaenda maeneo ya misitu ya kupandwa kwa ajili ya kupata hewa safi ...huko hakuruhusiwi sigara na magari mnapaki mbali
 
Nakumbuka Taiwan tulikuwa tunaenda maeneo ya misitu ya kupandwa kwa ajili ya kupata hewa safi ...huko hakuruhusiwi sigara na magari mnapaki mbali
Ni kweli kabisa. Hata sisi kule kwa mtogole na Manzese kwa mfuga mbwa kuna kipindi tulikua usiku tunalala nje ili tupate hewa safi, ila kwa siku hizi huwa tunakwenda kule coco beach kupata hewa safi.
 
Ni kweli kabisa. Hata sisi kule kwa mtogole na Manzese kwa mfuga mwa kuna kipindi tulikua usiku tunalala nje ili tupate hewa safi, ila kwa siku hizi huwa tunakwenda kule coco beach kupata hewa safi.
Hapana sababu ni kwamba nyumba mlizokua mnakaa hazina madirisha ya kutosha...unakuta nyumba dirisha linatazama bafuni kwa mtu unategemea nini... miaka nenda rudi madirisha hayafunguliwi...lazma mlale nje
 
Halafu makolokolo kibao
 
1455016103581.jpg
 
Back
Top Bottom