Mwili wa mtoto mkiristo wafukuliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwili wa mtoto mkiristo wafukuliwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mgomba101, Oct 4, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mtafaruku umezuka Wilaya ya Bagamoyo baada ya watu wanaodhaniwa kuwa waumini wa dini ya Kiislamu wa msikiti wa Majani Mapana kuvamia makaburi ya kiislamu ya Tandika Kata ya Magomeni kwa lengo la kutaka kubomoa kaburi moja la mtoto Aruina Rolan Mitaban.

  Watu hao walitaka kubomoa kaburi hilo wakidai kuwa mtoto aliyezikwa katika makaburi hayo ni Mkristo, hivyo haruhusiwi kwa kuwa si muumini wa dini ya Kiislamu.

  Tukio hilo limetokea juzi wa Jumapili na waumini hao baada ya kulibomoa kaburi hilo, waliwataka ndugu wa marehemu kufukua mwili wa mtoto huyo kabla wao hawajachukua hatua za kufukua.

  Walisema kitendo cha Wakristo kwenda kuuzika mwili huo katika makaburi hayo na kuujengea kwa marumaru na kuweka msalaba ni uchokozi kwa waumini wa dini ya Kiislamu.

  Kutokana na tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, alilazimika kuitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Ulinzi na Usalama suala hilo ili kulipatia ufumbuzi.

  Kipozi aliwataka waumini wa dini zote mbili kujenga tabia ya kuvumiliana wanapokuwa na matatizo badala ya kuendekeza jazba na hasira ambazo haziwezi kuleta tija.

  Mwili wa mtoto huo baada ya kufukuliwa na ndugu wa marehemu walikwenda kuuzika upya jijini Dar es salaam.
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mwili wa mtoto tena malaika unafukuliwa kwa tofauti ya kiimani tuu! Hizi mbegu za udini alizapanda nani?? Au ni ukosefu wa elimu dunia??
   
 3. N

  NnyaMbwate JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,398
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 280
  Ama kweli njia ya kwenda mbinguni ni nyembamba!
   
 4. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,329
  Likes Received: 2,632
  Trophy Points: 280
  Thamani ya mwili wa binadam huondoka pindi tu uhai umtokapo...
  Zipo dini na imani zinazotukuza sana maiti, makaburi na vyote vilinganavyo na hayo....
   
 5. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2012
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  mnhhhhh...i can see now baada ya makanisa sasa ni sehemu za kuzikana/ malazi ya milele.... wenzetu wanahitaji kupata elimu zaidi hasa ya mahusiano na uvumilivu na kutatua migongano ya kijamii inayojitokeza kwa njia ya maongezi..jazba na maamuzi ya haraka mara nyingi huwa hayana tija.

  changamoto kwa watu wa mipango miji...makaburi yawe yanagawanywa kulingana na imani za dini...waislam watazikwa kinondoni wakristo mbagala..hii itapunguza misuguano kama hii..masuala ya kuchangia makaburi na tofauti kuwa misalaba na mashahidi ndio yanapelekea mitifuano hii isiyo na kichwa wala mkia.
   
 6. I

  Ikunda JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2012
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 722
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii Tanzania sijui tunaelekea wapi????? Mwenyezi Mungu atunusuru
   
 7. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  HuoNAomba nijibu bila kuweka jazba! hivi katika akili ya kibinadamu unaona kabisa hili eneo ni la imani fulani, na wewe unakwenda na imani yako ambayo inakinzana kabisa na imani ile, je huo si uchokozi wa makusudi? vitu vingine nadhani vinapitiliza, waislamu wana imani tofauti na imani nyingine katika mazishi vile vile wakirisito pia wana imani tofauti , hivi ni haki mtu kuingilia imani ya mtu mwengine!

  Hawa wenzetu wana tabia hizi na kupenda kujiingiza katika makaburi ya waislmau kwa kutumia gear ya mtoto, imeshatokea sehemu nying sana za pwani! NYINGI SANA! utakuta wenyeji wa hapo ni waislmu atakuja mtu amefiwa na mtoto kuomba kuzika, na wakiruhusiwa huwa ndio wao wamiliki wa eneo hilo kwanini wasizungumze na serikali ikawatengea eneo lao ambalo watazika na kuabudu kwa imani yao! nachukulia tendo hilo ni la kichokozi na kweli haliwezi kuvumiliwa, vitu vingine mnapenda kushadadia ilhali wenyewe mnauanza uchokozi, siwezi kufikiri hata siku moja, musialmu ataenda eneo ambalo mkirisito amezikwa akataka na yeye aulaze mwili wa ndugu yake wa kiislamu labda huy haijui dini yake!

  Ndugu zangu msipende malumbano ya dini hayatupeleki kotote na badala yake yanazidi kutuweka mbali mbali watu ambao tumekuwa tukiishi kwa upendo na kuvumiliana hili tusilikubali jamani ndugu zangu ! mbona linafika mbali sasa? kila moja awe na imani yake na tusilete dhihaka katika imani baadae tuseme fulani wana kasumba hii kumbe dhihaka imeanzishwa na wenyewe !
   
 8. j

  joely JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,030
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  jambo la msingi ni kujua kwanini mkristo alizikwa sehemu ya waislaam,

   
 9. M

  MKUU WA KAYA JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2012
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 201
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Dini zote mbili zinafuata maandiko takatifu ya vitabu vinavyoongoza yaani Biblia na Quran.Labda wanajamii tufahamishane hili jambo la kukataza kuzikana dini tofauti eneo moja liko kwenye vitabu au ni umbumbu tu wa dini fulani?
   
 10. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  na mie nimejiuliza swali hilo......inawezekana aliyetoa kibali cha eneo la kuzika alikosea...... ukisoma jina la marehemu kidogo linachanganya
   
 11. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  sawa sawa....
   
 12. mpalu

  mpalu JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 2,490
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  tunaanza taratibu....siku si nyingi...dukaa la waislam,kisima au bomba la wakristu, gari ya waislam,soko la wakristu..tutafika tu huko.....hii midini ya watu inatupa shida sana bora wangebaki nayo wenyewe huko kwao.....:sorry:.....
   
 13. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwa kweli mi ningependa 2 kujua kwa nini kama ni mkristo alizikwa hapo kwa nini?je hao wakristo waliruhusiwa na nani? Na je walijua ni eneo la waislamu?
   
 14. Nokla

  Nokla JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 2,121
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  waswahili usema 'AANZAE HAVUMI'
   
 15. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Tatizo letu Binadamu tunaweka ushabiki wa dini mbele na huku hata dini yenyewe hatuijui.

  Uislamu na Ukrsito wote ni ndugu moja katika maandiko ipo hivyo.

  SOMA MAANDIKO:
  Sote tu watoto wa Ibrahimu, Waislamu wanatokana na upande wa uzao wa Mjakazi wa Ibrahim baada ya Sara kumruhusu kuzaa na mjakazi wake kwa kuwa Sara alikuwa mgumba.

  Wakristo wanatokana na uzao wa Sara kwa mtoto Isaka.

  Sasa hawa wote ni watoto wa Ibrahim, je uhasama unatoka wapi.

  Kwa Muislamu au Mkristo anayejua dini yake hawezi kudharau moja ya dini hizi mbili.

  Ni wakati umefika kwa BAKWATA kutafuta jinsi ya kutafsiri kitabu cha Quaran katika lugha za mahalia ili kuwezesha waumini kujua maandiko. Lugha ya Kiarabu mfano kwetu Watanzania hatujui isipokuwa tunaimba tu na hatujui kilichandikwa.

  Ni sawa kama Kitabu cha Biblia kingeliandikwa kwa Kilatini au kiebrania, sidhani kama wangelijua kilichoandikwa. Lakini kwa kuwa kipo katika lugha mahalia ndio maana kinaeleweka.

  tuweke pembeni ushabiki wa kijinga. Kaburi la mkristo na Kaburi la Muislamu yote ni sawa mbele ya Mwenyezi Mungu.


  "MUNGU AWASAMEHE wote WALIOHISIKA na KITENDO HIKI KWA SABABU HAWAKUJUA WALITENDALO"
  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 16. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Dahh, hii kali. Yaani watu wanagombea hadi sehemu ya KUZIKA?

  Itafika siku watagombea hadi Vyoo vya Wakrito na Waislaam.

  Mbona tukifa tunazikana wote bila tatizo? Waislaam wataingia hadi kanisani kwenye Ibada ya Marehemu.

  Mie nusu ya familia ni Waislaam na huwa wanakuja kuzika bila shida. Imeshatokea hata baadhi ya ndugu wa Kiislaam kufia nyumbani kwetu na tunaita Waislaam wenzake waje wamfanyie Ibada ya kumzika. Hakuna anayefanya Big Deal. Sasa hili jitu linalopandikiza Udini Tanzania sijui lina malengo gani?

  Mwisho, kama kweli Waislaam waliamua kumpa kijieneo huyo mtoto apewe Mapumziko mema kwa sababu tu Waislaam huko ni wengi, wangelifanya busara ya kuwatengea kijieneo kabisa ili huko mbeleni wasije wakaanza kukosana. Ila inavyoonekana wote walikosa BUSARA kwa hili.

  AMA KWELI DINI ZILIZOLETWA NA MELI, hahahaaa.........
   
 17. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #17
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Kwa kauli yako basi Waliofukua watalua wanaabudu kabisa hizo
  maiti
   
 18. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #18
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  ndo upeo wa mwafrika ulipoishia, wakati wenzetu wanapambana kiuchumi na kimaendeleo sie tunabaguana kidini
   
 19. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #19
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]ALHAMISI, OCTOBA 04, 2012 04:34 NA MWANDISHI WETU, BAGAMOYO


  *Wavamia makaburi ya Wakristo, DC ashangaa
  *Kaburi lafukuliwa, mwili wazikwa upya Dar

  KUNDI la waumini wa dini ya Kiislamu (Mujjahidina), kutoka Msikiti wa Majani Mapana Tandika, wilayani Bagamoyo, mkoa wa Pwani, limefanya vurugu kubwa baada ya kuvamia makaburi ya Kiislamu na kutaka kaburi alilozikwa mtoto Aruina Rolan Mitaban lifukuliwe.

  Waislamu hao, ambao walionekana kujawa na jazba, walidai mwili wa mtoto huyo, hauruhusiwi kuzikwa katika maeneo yao, kwa sababu ni Mkristo.

  Tukio hilo lilitokea Septemba 30, mwaka huu, ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kuzikwa kwa mwili wa mtoto huyo, katika makaburi hayo.

  Tukio hilo, limeonekana kuibua hisia kali kwa wakazi wa Bagamoyo, ambao miongoni mwao walidai huo ni unyama wa kupindukia.

  “Haiwezekani kaburi la mtoto kama yule, malaika wa Mungu asiyejua kitu, linakwenda kufukuliwa kinyama vile… nadhani tunakoelekea ni kubaya sasa,” alisema Suleiman Wahid.

  “Huwezi kusambaratisha kaburi namna hii, ilitakiwa wakutane na viongozi wa makaburi kwanza, marehemu yule ana kosa gani? Watanzania tunapotea,” alisema Wahid.

  Kufuatia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, aliamua kuitisha kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha dharura ili kujadili.

  Baada ya kuitisha kikao hicho, aliziita pande mbili zinazohusika, ili kupata ufumbuzi wa suala hilo.

  Kipozi aliwataka waumini wa dini hizo na wakazi wa wilaya hiyo, kujenga tabia ya kuvumiliana pale kunapokuwa na matatizo, badala ya kuendekeza jazba na hasira ambazo haziwezi kuleta tija.

  Mara baada ya kikao hicho cha kamati ya ulinzi na usalama, upande wa marehemu huyo wakiongozwa na baba wa marehemu, Rolan Mitaban, Oktoba 2, mwaka huu walilazimika kwenda kufukua mwili huo wa marehemu na kwenda kuuzika upya jijini Dar es Salaam.

  “Tukio hili limetokea, nikalazimika kuitisha kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama, na pande zote zinazohusika.

  “Moja ya maazimio tuliyokubalina ni kwamba, kaburi lile lisibughudhiwe na mtu yeyote na ndugu zao walijengee kama yalivyojengewa makaburi mengine.

  “Lakini katika hali ya kushangaza, nimesikia jana baba mzazi wa marehemu akiwa na ndugu zake, waliamua kwenda kufukua mwili wa marehemu na kwenda kuuzika Dar es Salaam,” alisema Kipozi.

  Kutokana na tukio hilo, DC Kipozi alitoa wito kwa viongozi wa dini, kuhakikisha wanawasiliana na ofisi yake, ili kushughulikia matatizo ya aina hiyo yanapojitokeza, ili kuepusha madhara ambayo yanaweza kutokea.

  Baadhi ya ndugu wa marehemu, ambao waliomba majina yao yahifadhiwe, walisema kitendo kilichofanywa na waumini wa dini ya Kiislamu si cha kiungwana, kwani kama kulikuwa na tatizo hilo, walipaswa kuwataarifu wahusika ili waweze kwenda kushughulikia kwa kufuata sheria.

  Hii ni mara ya pili kutokea kwa vurugu katika makaburi ya Tandika, itakumbukwa mwanzoni mwa mwaka huu, kuliibuka uvumi kuwa kuna joka kubwa la kishirikina katika makaburi hayo na kupelekea mganga wa kienyeji maarufu Zoazoa, kwenda kuweka matambiko ambayo hayakuzaa matunda.

   
 20. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #20
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Jamani Familia ya Rais; including PRINCE wote wako CCM-NEC wakiiwakilisha BAGAMOYO, kwanini

  wasiingilie
  Suala hilo na kulitatua? Kwanini basi wako kwenye SIASA kama Masuala ya Maeneo ya

  BAGAMOYO wanashindwa
  Kuyatatua ? au wanataka tu hizo 10% ???

  Wapo 3 toka BAGAMOYO CCM-NEC
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...