TBC kuna mchungazi kwenye msiba wa Judge Nsekela anashusha nondo msikilizeni. Siamini masikio yangu, msikilizeni mchungaji.
Pia, Soma=>Kamishna wa Maadili, Jaji Harold Nsekela afariki dunia
========
WASIFU WA MAREHEMU NSEKELA
Kuzaliwa: 29 Oct 1944
Alisoma shule ya msingi na kati Mpuguso, Rungwe kati ya mwaka 1951 na mwaka 1958 kisha akaendelea na masomo ya shule ya sekondari Malangali kati ya mwaka 1959 na mwaka 1962. Mwaka 1963 alijiunga na shule ya sekondari wavulana Tabora na kuhitimu mwaka 1964.
Alihitimu Shahada ya sheria chuo kikuu cha Afrika Mashariki mwaka 1968 na mwaka 1970 alihitimu shahada ya uzamili chuo kikuu cha Yale nchini Marekani.
AJIRA
1968-1970: Mhadhari msaidizi kitivo cha sheria chuo kikuu cha Afrika Mashariki
1971-1974: Mhadhiri chuo kikuu cha Dar es Salaam
1975-1976: Mhadhiri chuo kikuu cha usimamizi wa fedha
1976-1997: Alifanya kazi katika nafasi mbalimbali kwenye shirika la sheria Tanzania
Mei 1997: Aliteuliwa kuwa Jaji wa mahakama kuu ya Tanzania
Februari 2003: Aliteuliwa kuwa Jaji wa mahaka ya rufaa Tanzania
Novemba 2006: Aliteuliwa kuwa Jaji wa mahakama ya Afrika Mashariki
Julai 2008: Aliteuliwa kuwa makamu wa Rais wa mahakama ya Afrika Mashariki
Novemba 2008- June 2014: Rais Mahakama ya Afrika Mashariki
Mei 2014: Mjumbe wa Taasisi wa waamuzi(Tanzania Institute of Arbitrators)
Disemba 2016: Aliteuliwa kuwa kamishna wa maadili na amekuwa katika nafasi hiyo hadi mauti yalipomkuta Disemba 6, 2020 saa mbili asubuhi.
NDOA NA FAMILIA
Marehemu alifunga ndoa na mke wake Subilaga Nsekela Julai 9, 1977. Marehemu ameacha watoto wanne na wajukuu watatu.
UGONJWA NA KIFO
Marehemu aliugua kwa muda mfupi na kufariki tarehe 06/12/2020 saa mbili asubuhi.
NENO LA SHUKRANI(FAMILIA)
Andende Kisye Nsekela(Mtoto wa marehemu): Natanguliza shukrani zangu binafsi na familia nzima kwa waganga wote wa hospitali ya mission ya DCMC iliyopo Ntyuka, waganga wote wa hospitali ya Dodoma, wafanyakazi wote wa tume ya maadili Tanzania, wafanyakazi wote wa mahakama zote Tanzania, serikali kwa ujumla wote. Kipekee ningependa kumshukuru mheshimiwa Rais Magufuli ambae alimuamini baba yetu na kuweza kumpatia kazi ya kutumika nae katika Taifa.