Mwili wa bondia Ibrahim Najim aliyefariki baada ya kuanguka ulingoni, kuzikwa Kyela

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
bondia-pc.jpg

Mwili wa bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Ibrahim Najim unatarajiwa kuzikwa wilayani Kyela Mkoani Mbeya.

Najum alianguka ulingoni jumapili iliyopita baada ya kumalizika kwa pambano lake la raundi nne dhidi ya bondia Laurent Segu wa Dodoma na kuwahishwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General).

Katika pambano hilo, Najim alipigwa kwa pointi na inadaiwa alifanyiwa upasuaji mdogo wa kichwa hadi asubuhi ya jana hali yake ilizidi kuimarika kabla ya kufikwa na mauti mchana wa jana

Bondia huyo alikuwa amecheza mapambano matatu ya ngumi za kulipwa pamoja na la Jumapili iliyopita, ambapo ameshinda moja na kupoteza mawili.

Kaka wa marehemu Richard Chawinga amesema wapo njiani wakielekea Kyela kwa ajili ya mazishi ya mabondia huyo na wakifika watakaa kikao kujua anazikwa lini.

“Tupo njiani tukielekea Mbeya tukifika ndio tutajua utaratibu wa mazishi upoje maana kuna ndugu zetu wanatusubiria kule, ila tutamhifadhi nyumbani Kyela”amesema Chawinga.

Chanzo: Mwanaspoti
 
Huu mchezo sijawahi kuupenda

Mchezo wa kupigana una raha gani sasa

Football raha yake pass, mikimbio, vyenga, mashuti na upanguaji wa mashuti lakini huu eti ngumi za kichwa ndio raha yake na mashabiki wake wanashangilia mwanadamu mwenzao kudundwa so sad

RIP
 
Huu mchezo sijawahi kuupenda

Mchezo wa kupigana una raha gani sasa

Football raha yake pass, mikimbio, vyenga, mashuti na upanguaji wa mashuti lakini huu eti ngumi za kichwa ndio raha yake na mashabiki wake wanashangilia mwanadamu mwenzao kudundwa so sad

RIP
Siku kama utapata bahati ya kushuhudia live,hutarudi..
Watu wanachapana ngumi hasa..
Unaona kabisa hii ngumi kali,kaponea chupuchupu.
 
Siku kama utapata bahati ya kushuhudia live,hutarudi..
Watu wanachapana ngumi hasa..
Unaona kabisa hii ngumi kali,kaponea chupuchupu.
ngumi za kitaani napitaga mbali nipo tayari nibadilishe njia ili mradi kukwepa ugomvi wa watu njiani

sembuse hao wa kulipia siwezi abadani
 
Back
Top Bottom