Mwili wa binadamu ni kama gari

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Unaambiwa usiku mwili hautakiwi ule ushibe sana halafu ukalale ni sawa na gari ujaze mafuta full tank halafu ukapaki

Unaambiwa mazoezi siyo adhabu asubuhi baada ya ufanya mazoezi hutakiwi kujipongeza kwa kulala usingizi kama ishara ya kupumzika ni sawa na gari uliwashe na kupiga mares kibao vuum vuuum vuuum halafu ukapaki tens

Unaambiwa zingatia mlo kamili na kunywa maji safi na salama ya kutosha, ni sawa na gari kulizoesha mafuta ya kidebe

Unaambiwa hakikisha wakati unapofanya mazoezi jizuie kuwaza mambo mengine mfano, Chakula, njaa, mapenzi, madeni, miadi n.k kwa sababu huchangia kuondoa umakini, ni sawa na dereva anaeshangaa wapita njia badala ya ku-drive

Unaambiwa mazoezi ya kukaa chini na kunyanyuka nyanyuka au kichura chura au push-up ndiyo kipimo cha kuubeba mwili wako. Inasemekana kuna baadhi ya watu hawawezi kunyanyuka chooni hadi washike ndoo au ukuta ni sawa na gari kufa shock-up kwenye mashimo inaingia nzimanzima!

Unaambiwa unatakiwa kufanya mazoezi ya kukata kiuno japo Mara moja kwa wiki hii ni sawa na gari kukosa grisi kwenye CV au Ball Joint
Mazoezi siyo lazima uwe na eneo kubwa hata chumbani unaweza kufanya.
 
Back
Top Bottom