Mwili wa Alphonce Mawazo wageuzwa kuwa suala la kisiasa

Hivi chadema mkishamzika Mawazo mtabaki na hoja gani ya kusikilizwa? Mnamtesa marehemu ili mpate umaarufu wa kisiasa mzikeni tu kwani akizikwa kifamilia haitoshi mpk mkazungushe mikono. Justice for Mawazo
 
Nadhani arguments za kusema ukawa wanatumia msiba huu kupata umaaru wa kisiasa ni mawazo ya kitoto. Ni ya kitoto kwasababu watu wa kwaza kuhusika na kupata uchungu wa marehemu Alphonce ni familia yake kwanza halafu Chadema(Ukawa) taasisi iliyofanya naye kazi kwa karibu sana na kwa muda wake mwingi kuliko taasisi nyingine. Haya makundi mawili ndiyo wahanga haswa. Kwa desturi ya misiba yote katika jamii hii ndio ilivyo na hawa ndio huupa msiba joto(faraja kubwa kwa familia husika).

Sasa wale wasioguswa na msiba, wasioona uchungu wa mpendwa wao ni kawaida tu. Mafisiem wanaimba kwaya ya kushangilia, furaha kama vile ni harusi ya kuoa au kuolewa. Wakati Ukawa wanaimba nyimbo za harusi ya tatu ya msiba, majozi, huzuni. Hamuwezi ku-argue pamoja hata siku moja. Bahati mbaya mafisiem na mihili yake na vibaraka wengine ndo wameshikamana kuhakikisha wanatumia kila njia kuwaminya Ukawa bila sababu za msingi.

Naomba niishie hapo. Nitaendelea kutoa mawazo yangu.............
 
Kutafuta Umaarufu kwa Njia kama Hizi ni Upuuzi mkubwa sana.. Sina Hakika kama Akili Za Viongozi zinawatosha... Hili la umaarufu wanalolitafuta litageuka kuwa laana

Nadhani kuzuia watu kumuaga mpedwa na ndugu yao ni upumbavu na uwendawazimu
 
Nilikuwa miongoni mwa watu wa awali kupinga uamuzi wa RPC wa Mwanza, kwa kushinikizo la Mkuu wa Mkoa huo, kupiga marufuku wafuasi wa Ukawa na wananchi wengine kuuaga mwili wa Alphonce Mawazo. Kwa kweli sikutarajia Jaji mwenye weledi wa sheria anayezingatia mila na desturi za jamii yetu, aunge mkono marufuku hiyo haramu. Jaji Mlacha amefanya kazi yake nzuri. Tunampongeza.

Uamuzi wa RPC hata kama ulikuwa ni wa shinikizo, ulikuwa na athari kubwa kwa Rais Magufuli, ambaye tangu mapema kabisa aliahidi kuiongoza Tanzania bila kujali itikadi, kabila, dini, kanda wala hali ya mtu. Hiyo ndiyo Serikali ya Magufuli ambayo Watanzania wanataka kuiona.

Mimi si mfuasi wa vyama vya siasa, lakini linapokuja suala la haki na usawa, mara zote nimesimamia misingi hiyo; na wala siwezi kujifanya hamnazo na kuona vitu hivyo vikipuuzwa. Sasa kumejitokeza taasisi eti zinazoshangazwa na suala la msiba wa Mawazo kufanywa la kisiasa! Sijui ni kutafuta sifa, au kitu gani. Mawazo alikuwa Mwenyekiti wa chama Mkoa. Hadi anauawa, alikuwa na wadhifa huo. Ameuawa muda mfupi akitoka kwenye siasa! Ameuawa muda ambao bado moshi wa kisiasa ukiendelea kufuka huku na kule nchini kote.

Msiba wa mtu wa aina hiyo hutarajii kuona ukiishia kwenye mapambio pekee bila kuingiza neno la kisiasa. Kama Mawazo angekuwa amekufa kifo kilichosababishwa na malaria au ugonjwa mwingine, kweli hapo siasa isingekuwa mahali pake. Angekuwa ameuawa kwa ugomvi wa ardhi, kweli hapo siasa isingekuwa mahali pale! Mtu aliyeuawa katika mazingira yanayoashiria kuwa ni ya kisasa itakuwaje msiba wake usitawaliwe na hisia za kisiasa? Marafiki wakuu wa Mawazo aliokuwa karibu nao ni wanasiasa. Je, wanaopinga siasa kwenye msiba huu, wanatarajia Mbowe, Mbatia, Lowassa, na wafuasi wengine wa Ukawa, wazungumze nini kisichoshabihiana na siasa? Je, wanatarajia jeneza lenye mwili wa Mawazo lifunikwe kwa kitambaa gani zaidi ya bendera ya Chadema?

Huu ni mtazamo wangu ambao hauna vimelea vya kiitikadi, isipokuwa mimi ni katika wale wanaoamini kuwa kuusema ukweli kutatuweka huru; na kwa njia hiyo tutakuwa tunashiriki kuijenga Tanzania yenye Haki na Usawa. Kuzuia Siasa kwenye msiba wa Mawazo ni sawa na kumtaka Padre au Sheikh asimtaje shetani wakati wa ibada; kitu ambacho hakiwezekani aslani.
 
Kifo cha Mawazo ni cha kisiasa....wadhifa wake ni wa kisiasa ...hapo utakwepa vipi msiba wake kutokuwa wa kisiasa?
 
You are absolutely right Manyerere Jackton huu msiba haukwepi siasa sababu alikuwa kiongozi wa kisiasa, akioa/olewa au akifariki mwanajeshi mambo ya kijeshi hayakwepeki hivyo kupinga siasa katika msiba wa marehemu Mawazo ni kupenda sifa za kijinga na kujitoa ufahamu tu
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo RPC ana nguvu kuliko Rais?

Why yeye Magufuli alipoona RPC anaenda kinyume na misimamo yake hakuingilia kati?

Why mpaka watu waende mahakamani wakati ilikuwa ni kazi ya dakika moja kwa Rais
kumpigia simu IGP na kumpa maelekezo?

Why mmeanza 'kibarua ' cha kumtetea Rais bila kuombwa?

cc Nyani Ngabu....
 
Last edited by a moderator:
Kwa hiyo RPC ana nguvu kuliko Rais?

Why yeye Magufuli alipoona RPC anaenda kinyume na misimamo yake hakuingilia kati?

Why mpaka watu waende mahakamani wakati ilikuwa ni kazi ya dakika moja kwa Rais
kumpigia simu IGP na kumpa maelekezo?

Why mmeanza 'kibarua ' cha kumtetea Rais bila kuombwa?

cc Nyani Ngabu....
haya maswali majibu huwezi kupata,, na ukipata yatakuwa ya kisiasa
 
Leo Manyerere huna chama mhhhh makubwa haya. Pia hamna sintofahamu Tanzania Bara uchaguzi umeisha na Rais ameishapatikana ni KaziTu Iliyobakia. Rais wenu wa Monduli arudi akachunge Ng'ombe na yule Mpemba arudi kwao akauze rojo na mishikaki. Zilizobaki ni siasa za matukio tu kama harusi na misiba
 
manyerere umeongea ukweli ila inaonekana kama vile unajipendekeza kwa magufuri eti hausiki na issue hii wakati huyo rpc anatenda kwa niaba yake, ndio watu kama nyie mnasemaga eti jk alikua kiongozi bora tatizo watendaji wake!
 
Subiri wakishazika kama watakuwa na habari na family yake tena, mbona mtoi na chacha wange wamesahaulika wao mpaka family zao? Hizi siasa za kujibust tu hakuna uchungu wowote,
 
Vizuri nimekuelewa.

Ila niulize tu hapo kwenye red; hivi shetani ni jina muhimu kwenye ibada?

Swali tamu sana hilo! Katika maisha ya kiroho kuna majina makuu mawili la Shetani ni mojawapo japo liko in the negative side. Kusema hakuna Shetani hakuna tofauti na kudharau kazi ya ukombozi aliyoifanya Mungu mwenyewe; na kudharau ukombozi ni kumdharau yeye mweneywe.
 
Kwa hiyo RPC ana nguvu kuliko Rais?

Why yeye Magufuli alipoona RPC anaenda kinyume na misimamo yake hakuingilia kati?

Why mpaka watu waende mahakamani wakati ilikuwa ni kazi ya dakika moja kwa Rais
kumpigia simu IGP na kumpa maelekezo?

Why mmeanza 'kibarua ' cha kumtetea Rais bila kuombwa?

cc Nyani Ngabu....
Una dalili zote za ushoga
 
Vizuri nimekuelewa.

Ila niulize tu hapo kwenye red; hivi shetani ni jina muhimu kwenye ibada?

Ndiyo, lengo ni kumwabudu Mungu na kuachana na shetani na makando kando yake! Ukisikia pakihubiriwa Mfuate Mungu, maanake mwache shetani!
 
Back
Top Bottom