Mwijage tena alia na TRA wasimharibie kazi

Krinika ndo nini?
Hii ni malighafi(raw materials) ya kutengenezea portland cement. Kikemical hii ni calcium silicate
Hii hupatikana kwa "kuchoma"(heat) limestone na clay soil. Huwa katika mfumo wa viduara vidogo vidogo hii ndio husagwa kwenye mtambo pamoja na mambo mengine ili kupata cement.
Maeneo ya Tanga hii kitu inapatikana ya kutosha sana
 
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutomfukuzisha kazi kwa uzembe wao uliopelekea nchi kupigwa na kupata hasara kutokana na watu kuingiza cement kutoka nje ya nchi wakidai ni krinka.

Waziri Mwijage alisema hayo jana kupitia kipindi cha HOTMIX na ambapo alitumia nafasi hiyo kupiga marufuku Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kukagua krinka yoyote kutoka nje ya nchi.

"Mtu anatengeneza Krinka anauza Kenya, sasa kama mtu anatengeneza Krinka Tanga anauza Kenya wewe unafuata nini Pakistan? Hakuna krinka inatoka nje ya nchi ile ni Cement iliyokamilika TRA wanashindwa kufanya kazi yao.

Narudia kusema hakuna krinka inaingia nchini kutoka nje ile ni Cement kamili na anayepinga aje aniambie mimi, na kuanzia leo TBS wasikague krinka yoyote kutoka nje ya nchi waingize ndani ya nchi bila TBS kukagua, TBS ipo chini yangu sasa kama mimi naambiwa sitoshi na wa TBS ajiangalie" alisema Mwijage
Aidha Waziri Mwijage alidai kuwa watu wa Cement walikubaliana na DR Meru kununua hizo Krinka hapa hapa nchini.

"Watu wa Cement walikubaliana hapa na Dr. Meru Twiga Cement ananunua Krinka Simba Cement mwingine nani ananunua krinka nyingine kutoka wapi, watu wanaleta cement iliyokamilika wanasema Krinka sasa kuanzia leo TBS hawezi kukagua krinka yoyote kutoka nje ya nchi, mpaka mamlaka iliyopo juu yangu sasa kama TRA walizembea tukapigwa juu yao kwanini wanataka kuharibiana kazi, eti bwana wanataka kuniharibia kazi mimi" alisisitiza Waziri Mwijage.
Post yako imelenga nini?
Mbona hujakamilisha alichozungumza Waziri juu ya kupoteza ajira za watanzania iwapo tutaendelea kununua clinker kutoka nje na kuacha zinazozalishwa hapa kwetu?

Kwa hili la kulinda ajira za Watanzania na utumiaji wa clinker inayozalishwa na kiwanda chetu namuunga mkono Mwijage.

Wengi wanaoponda ama kwa kutoelewa au kwa makusudi ( Maana wapo wanaolipwa na wenye agenda ya kuchafua na kutia doa kila jema linalofanywa na Serikali hii) ndoi hao hao wangetoa mapovu kulalamika tunauziwa Cement ya nje kuuwa viwanda vya ndani.
 
Hii ni malighafi(raw materials) ya kutengenezea portland cement. Kikemical hii ni calcium silicate
Hii hupatikana kwa "kuchoma"(heat) limestone na clay soil. Huwa katika mfumo wa viduara vidogo vidogo hii ndio husagwa kwenye mtambo pamoja na mambo mengine ili kupata cement.
Maeneo ya Tanga hii kitu inapatikana ya kutosha sana
Tayari ni cement. Hata wewe ukipewa clinker unatumia vizuri tu. Unaisaga( grounding) na kuchanganya na gypsum kidogo ili isikauke haraka baada ya kutia maji
 
Post yako imelenga nini?
Mbona hujakamilisha alichozungumza Waziri juu ya kupoteza ajira za watanzania iwapo tutaendelea kununua clinker kutoka nje na kuacha zinazozalishwa hapa kwetu?

Kwa hili la kulinda ajira za Watanzania na utumiaji wa clinker inayozalishwa na kiwanda chetu namuunga mkono Mwijage.

Wengi wanaoponda ama kwa kutoelewa au kwa makusudi ( Maana wapo wanaolipwa na wenye agenda ya kuchafua na kutia doa kila jema linalofanywa na Serikali hii) ndoi hao hao wangetoa mapovu kulalamika tunauziwa Cement ya nje kuuwa viwanda vya ndani.
Silielewi neno "biashara huria" lina maana gani, unawea kunielewesha?
 
Silielewi neno "biashara huria" lina maana gani, unawea kunielewesha?
Biashara huria si kigezo cha kukiuka makubaliani na kufanya udanganyifu.

Na labda wewe unaelewa nini maana ya Viwanda kukubaliana kununua clinker inayozalishwa hapa nchini halafu mmoja anakiuka na kununua cement na kuwatumia TBS kuidhinisha kuwa ni clinker? Tena na hiyo bado ni nje ya makubaliano ya ambako angestahili kununua?
 
Viwanda kukubaliana kununua klika kwenye soko moja inatafsiri moja tu kuwa consumers "CONSPIRACY"

Mabei ya saruji kwa miaka nenda rudi yako juu kupita maelezo!

Klika ya nje iruhusiwe ili wananchi wafaidi utaifa wao kwa kuishi maisha reasonable.
 
Mwijage afanye kazi aache kuogofya kutumbuliwa... Kama kuna waziri wa kwanza kukosa kazi kuanzia sasa ni yeye..... Kwanza ameudanganya umma wa Tanzania eti pwani kuna viwanda 300.... A kaenda Tanga akamtibua mtumbuaji mpaka akawatukana kuwa ni wapumbavu.

Nakushauri: ili usiwe na waswas Iba hela ya kutosha. Nenda kwa wachina hapo kkoo ndo wizara yako inapopatia kula. Chukua hela ya kutosha wekeza kuepusha uoga.
 
Krinka ni cement ambayo haijasagwa kuwa powder. Inakuwa katika shape ya "pebbles" vijiwe/vikokoto vidogo ambavyo ni smooth. Ukisaga krinka au "clinker" ndiyo unapata cement unayoijua huko mtaani
asante mkuuu clinker ndo nimeielewa vizuri nilifikiri aliataka labda kusema makinikia
 
Back
Top Bottom