Mbunge Charles Mwijage Aionesha Serikali Mbinu ya Kulinda Viwanda

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942

MHE. CHARLES MWIJAGE AIONYESHA SERIKALI MBINU YA KULINDA VIWANDA

Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini, Mhe. Charles John Poul Mwijage Akizungumza Bungeni wakati akichangia hoja kwenye bajeti ya Wizara ya viwanda na Uchukuzi Mhe. Mwijage ametumia muda huo kuionyesha Serikali mbinu hizo ambazo xitasaidia kuvilinda viwanda vya Kitanzania ili visife

"Muungano wa Twiga Cement na Tanga Cement matokeo yake ni kwamba sekta ya saruji inaweza kufa na kuishia kununua saruji nje ya nchi, pamoja na kuangalia sheria na maslahi ya wananchi, ni lazima pia tukaangalia je wanapoungana hakuna uwezekano wa sekta ya saruji nchini kufa na tukafikia hatua ya kuagiza saruji nje ya nchi?" Charles Mwijage, mbunge wa jimbo la Muleba Kaskazini

"Vigezo vya kuwa na market share (hisa za soko) stahiki vizingatiwe, kwani kwakuwa na market share stahiki kunazuia watu wengine kupanga bei na hatimaye kuwaumiza washindani wengine wadogo wanaoukua katika biashara husika" Charles Mwijage, mbunge wa jimbo la Muleba Kaskazini.

FvRzHzeWwAAMJP5.jpg
 
Back
Top Bottom